Mwili wa Etienne Tshisekedi umewasili nchini DR Congo baada ya miaka miwili nchini Ubelgiji

Mwanamke anashikilia picha ya aliyekuwa waziri mkuu wa DR Congo na kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi baada ya mwili wake kuwasili katika sherehe ya kumuomboleza. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeneza la Etienne Tshisekedi likipirishwa mbele ya umma mjini Kinshasa
Presentational white space

Baada ya kuchelewa kwa miaka miwili , hatimaye mwili wa baba wa rais wa DR Congo sasa umewasili nchini humo katika makaazi yake.

Maelfu walikongamana katika uwanja wa mashidi ili kumpatia heshima ya mwisho kiongozi huyo wa upinzani aliyehudumu kwa muda mrefu Etienne Tshisekedi.

Bwana Tshisekedi alifariki nchini Ubelgiji mnamo mwezi Februari 2017 akiwa na umri wa miaka 84, lakini mwili wake ulisalia katika taifa hilo kufuatia mgogoro kati yake na aliyekuwa rais wa taifa hilo Joseph Kabila.

Hatahivyo mgogoro huo ulikwisha baada ya mwanawe kiongozi huyo wa upinzani kuwa rais mwaka uliopita.

Haki miliki ya picha AFP
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafuasi wa kiongozi huyo wa upinzani walijitokeza wengi katika uwanja huo wa mashahidi ili kuulaki mwili wa kiongozi huo.

Uwanja wa michezo wa Martyrs mjini Kinshasa ulijaa raia wa taifa hilo waliopiga vigelegele siku ya Ijumaa baada ya jeneza lililobeba mwili wa Etienne Tshisekedi kuingia kulingana na mwanadishi wa BBC Gaius Kowene.

Wafuasi wa Etienne Tshisekedi walipiga kelele na miluzi katika uwanja huo wenye uwezo wa kuwabeba watu 80,000. Marais wa Rwanda na Angola walikuwa miongoni mwa wageni waheshimiwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tshgsekedi alihudumu kama kiongozi wa upinzani kwa miongo kadhaa lakini hakufanikiwa kuwa rais

Safari ngumu

Kampeni ya kuuzika mwili wa Tshisekedi nchini alikozaliwa ilikabiliwa na vizuizi kutoka kwa mtangulizi wake rais Felix Tshisekedi , Joseph kabila.

Kwa wafuasi wake , ujio wa Tshisekedi nyumbani unawakilisha ushindi dhidi ya serikali hiyo ya zamani , kulingana na mwandishi wa BBC wa eneo hilo.

Kuchelewa kwa dakika za mwisho , pia kuliathiri usafirishaji wa mwili huo kutoka mjini Brussels hadi katika mji mkuu wa DR Congo wa Kinshasa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Usafirishaji wa jeneza lake hadi nchini DR Congo ulizuiwa na upinzani mbali na mipango yao ya ndege iliotakiwa kuubeba mwili huo kutoka Ubelgiji,

Kitengo cha habari cha Ubelgiji Belga kilisema kuwa waandalizi awali walikuwa wamepanga kukodisha ndege kubwa aina ya Airbus 330 iliokuwa na nafasi ili jeneza hilo kuandamana na na abiria 270 , wakiwemo wanachama wa kamati ya chama cha Tshisekedi, cha Union of democracy and Social ProgressUDPS).

Afisa mmoja wa serikali aliambia chombo cha habari cha AFP mpango huo ulifutiliwa mbali kutokana na maswala kuhusu maandalizi ya ndege hiyo.

Ndege moja ndogo ya kibinafsi baadaye iliusafirisha mwili huo ikiandamana na wanachama 10 wa familia ya Tshisekedi, na kuwawacha makumi ya raia wengine wakiwa wamekwama nchini Ubelgiji.

Inadaiwa kuwa ndege hiyo ilikodishwa na rais Faure Gnassingbé waTogo.

Maombolezi yanaanza

Siku ya Alhamisi jioni, ndege hiyo ilitua mjini Kinshasa na ilikaribishwa na ujumbe mkubwa ulioongozwa na rais Felix Tshisekedi.

Baadhi ya wafuasi walisubiri katika uwanja wa ndege wakiwa wamebeba mabango yaliosoma Ufaransa kuwapatia raia kipau mbele, wakati mwili wake ulipowasili siku ya Alhamisi.

Wengi walivalia nguo nyeupe ili kuashiria kwamba Tshisekedi alikuwa mweupe kama pamba na kwamba hakujihusisha na ufisadi. Mwili wake ulibebwa na gari lililopambwa rangi za bendera ya DR Congo huku watazamaji wengi waksubiri nje ya uwanja wa ndege.

Lakini kulingana na chombo cha habari cha kibinafsi cha Actualite News, mtu mmoja aliuawa na gari la maafisa wa polisi wakati ambapo msafara wake ulikuwa ukipitia eneo jirani la lamete-ngome kuu ya mkongwe huyo wa upinzani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeneza la Tshisekedi litasafirishwa ili kutazamwa na wananchi ikiwa ni miongoni mwa mwa mipango kadhaa ya uombolezaji wa kitaifa

Mipango ya maombolezi inashirikisha misa za kidini , kuonyeshwa kwa jeneza hilo lililofunikwa pamoja na mkutano wa kisiasa siku ya Ijumaa katika uwanja huo wa mashahidi.

Moss Lenga , ambaye ni msermaji wa kamati ya mazishi ya Thisekedi aliambia BBC kwamba viongozi wa kidini watauchungza mwili huo wa Tshisekedi kubaini iwapo ni yeye .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mazishi ya Tshisekedi tyatafanyika siku ya Jumamosi

Mazishi ya kitaifa yatafanyika siku ya Jumamosi katika mji wa Nsele mashariki mwa Kinshasa . Marais sita wa Afrika wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo , ikiwemo Angola, Rwanda na Congo-Brazaville.

Maisha ya mpinzani

Tshisekedi alihudumu kisiasa kwa miongo kadhaa lakini akashindwa katika jaribio la kuwa rais.

Alkuhudumu kama waziri wa maswala ya ndani katika serikali ya Mbobutu Seseko, kabla ya kujiunga na siasa za upinzani.

Baada ya kuhudumia kifungo jela , alianzisha chama cha UDPS mwaka 1982 na aliteuliwa kuwa waziri mkuu na serikali ya Mobutu licha ya kwamba wawili hao walizozana mara ka mara.

Mwaka 1997, Mobutu aling'atuliwa madarakani katika upinzani ulioongozwa na babaake Joseph Kabila, Laurent.

Tshisekedi alikuwa mpinzani wa utawala mpya wa Joseph Kabila baada ya Laurent kabila kuuawa mwaka 2001.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tshisekedi's son FĂ©lix won a bitterly contested election last year

Alisusia uchaguzi wa DR Congo wa 2006 , akidai kwamba uchgauzi huo ulikuwa umefanyiwa udanganyifu na baadaye akashindwa 2011 katika uchaguzi uliodaiwa kukumbwa na udanganyifu.

Felix Tshisekedi alishinda uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali mwaka uliopita .

Uchaguzi huo hatahivyo uliadhimisha ubadilishanaji wa uongozi tangu DR Congo ilipojipatia uhuru kutoka kwa Ubelgiji 1960.

Hatahivyo baadhi ya wachunguzi wa uchaguzi huo waliamini kwamba mgomba mwengine wa upinzani Matrin Fayulu ndiye aliyefaa kuibuka mshindi.

Tangu alipochukua madaraka, rais Thisekedi alikubali kushirikiana na aliyekuwa rais wa zamani Joseph Kabila.

Mada zinazohusiana