Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 01.06.2019 : Sarri De Ligt, Rodri, Gundogan, Ramos, Hazard, Eriksen, Pogba, Mane, Ozil

Maurizio Sarri Haki miliki ya picha Getty Images

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri amekubali kuwa kocha mkuu wa Juventus na ameitaka Chelsea kumuondoa kwenye mkataba wake (Goal)

Sarri amemueleza Marina Granovskaia uamuzi wake walipokutana siku ya Ijumaa na Mkurugenzi wa the Blues ameahidi kujadiliana kuhusu mustakabali wake na mmiliki wa klabu Roman Abramovich. (Sky Italy - in Italian)

Barcelona wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 26 kama klabu zinazomuhitaji kama vile Man U au Chelsea zitafika dau (star)

Manchester United inajiandaa kumnyakua mshambuliaji Joao Felix ,19 kwa kitita cha pauni milioni 100.(Correio de Man via Mirror)

Stoke wanahitaji pauni milioni 30 kumuachia mlinda mlango Jack Butland, 26, anayetakiwa na Bournemouth and Crystal Palace. (Express)

Mchezaji wa Ajax Matthijs de Ligt, 19,atatoa uamuzi wake kwa Manchester United kuhusu kuahamia Old Trafford siku zijazo. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Reuters

Manchester City imesema kiungo wa kati anayekipiga Lyon Tanguy Ndombele, 22 na kiungo wa kati anayechezea Real Madrid Marco Llorente, 24 ndio machaguo yao iwapo watashindwa kupata sahihi ya kiungo wa kati wa Atletico Madrid Rodri, 22.(Manchester Evening News)

Ilkay Gundogan atasalia Manchester City msimu ujao hata kama mkataba wake utakwisha msimu ujao wamajira ya joto. (Mail)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ameingilia kati mwenyewe kuhakikisha kuwa mchezaji Sergio Ramos, 33 haondoki Bernabeu. (ESPN)

Real inaweka jitihada kumnasa kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard. (Marca)

Real wako na mpango wa kufanya mazungumzo na Chelsea kupata sahihi ya Hazard. (Mail)

Na Real pia itatupa karata uake kwa kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek, 22 au kumnasa Christian Eriksen, 27, wa Tottenham, watashindwa kumpata kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 26. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images

Wakati huo huo, Juventus wamesema kiungo wa kati wa Empoli ya Italia Hamed Traore ni mbadala wa Pogba.(Calciomercato)

Arsenal na Leicester wanamwangalia kwa karibu winga wa Valencia Ferran Torres ambaye anaweza kuuzwa kwa kitita cha pauni milioni 25.(Mail)

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, 27, amesema ilikua nusura ajiunge na Manchester United baada ya kuzungumza na meneja Louis Van Gaal, kabla ya simu ya Jurgen Klopp kubadili mawazo yake.(Mirror)

Kocha wa Arsenal Unai Emery yuko tayati kumuachia kiungo wa kati Mesut Ozil, 30 kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu wa joto. (Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images

Aston Villa wanataka kumchukua Gary Cahill wa Chelsea, wakimkutanisha na mchezaji mwenzake wa zamani wa Bues John Terry.(Sun)

Villa iko mbioni kumnasa kiungo wa kati wa Birmingham City Jota, 27.(Express and Star)

West Brom watajaribu kumpata kocha wa Sheffield United Chris Wilder kuwa kocha wao mpya. (Express and Star)

Klabu ya Schalke iko mbioni kumchukua mchezaji wa Everton Jonjoe Kenny kwa mkopo msimu huu. (Sky Sports)

Mada zinazohusiana