Jose Antonio Reyes afariki kwa ajali ya gari

Jose Antonio Reyes Haki miliki ya picha AFP

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Jose Antonio Reyes amefariki kwa ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 35, klabu ya Sevilla imetangaza.

Reyes mwenye asili ya Uhispania alijiunga na Gunners akitokea Ligi ya La liga mwezi Januari mwaka 2004.

Baadae aliichezea Real Madrid kwa mkopo mwaka 2006-2007, ikashinda ligi ya la liga.

Reyes ameelezwa kuwa ''mkongwe'' mmoja kati ya wachezaji wa thamani katika historia ya soka.

Reyes ameacha mke Noelia Lopez, ambaye alimuoa mwezi June mwaka 2017, na watoto watatu , wasichana Noelia na Triana na wa kiume Jose Antonio Jr .

Haki miliki ya picha Noelia Lopez Instagram

Salamu za pole zimetolewa

Arsenal imetoa salamu zake kwa mchezaji wake wa zamani, ikisema ''wameshtushwa na taarifa kuhusu kifo chake''.

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry, ambaye alicheza sambamba na Reyes kati ya mwaka 2004-2007, amemuita ''Mchezaji mahiri, mchezaji mwenza mzuri na binaadamu wa kipekee.''

''Ninaombea familia na marafiki waendelee kuwa na nguvu ya kuhimili kipindi hiki kigumu. aliongeza kwenye ukurasa wa twitter.

Sarri aondoka kwa 'hasira' kwenye mazoezi

Chelsea yailaza Arsenal na kushinda kombe la ligi ya Europa

Freddie Ljungberg aliwahi kucheza na Reyes ambaye amesema '' nimepigwa na butwaa kutokana na taarifa za kifo cha Antonio Reyes.''

Klabu aliyokuwa akiichezea hivi karibuni Extremadura UD ilitangaza taarifa za kifo cha mchezaji huyo.

Mada zinazohusiana