Mtu mmoja amekamatwa nchini Uhispania baada ya kukusanya fedha za ufadhili kwa IS

Wakutwa na hatia kujiunga na Isalmic State Haki miliki ya picha Reuters

Mwanaume mmoja raia wa Syria anayeshutumiwa kufadhili kundi la kigaidi la IS amekamatwa mjini Madrid, polisi nchini Uhispania wameeleza.

Mtu huyo ambaye hajatajwa kwa jina, anashukiwa kuwa sehemu ya watu wanaoliwezesha kifedha kundi hilo la kigaidi na anashutumiwa kutuma pesa kwa wapiganaji nchini Syria.

fedha hizo zilizokusanywa Ulaya ziliwafikia wanamgambo kupitia mfumo usio rasmi unaojulikana kwa jina hawala.Polisi wameeleza.

Takriban wapiganaji 6,000 kutoka Ulaya Magharibi wamejiunga na wanamgambo wa IS nchini Syria na Iraq.

Polisi nchini Uhispania wamesema uchunguzi wake ulionesha kwa wapiganaji wameunda mtandao wao nchini Syria kwa ajili ya kuwasaidia wapiganaji wa kigeni wanaotaka kurejea Ulaya

Wanamgambo wa IS waliposhindwa kudhibiti maeneo mengi, waliwataka wafuasi wake kurejea maeneo walikotoka, polisi wameeleza kwenye taarifa yao iliyoandikwa kwa lugha ya kihispania.

Mshukiwa anayeripotiwa kuwa na miaka 43, alikua akijificha alipokua akifanya mawasiliano kwa njia ya majukwaa ya kidigitali.

Vikosi vya usalama vyapambana na wanamgambo Mogadishu

Kundi la IS 'lapiga kambi' Mashariki mwa DRC

Hawala ni mfumo usio rasmi wa kutuma fedha unaotumia mawakala walio katika nchi mbalimbali, hali inayofanya kuwa vigumu kwa mamlaka kubaini fedha zinazovushwa kwenda ng'ambo.

Hakuna fedha zinazovuka mipaka kimataifa kwa kutumia hawala.

Haki miliki ya picha Reuters

Zaidi ya watu 41,000 kutoka nchi mbalimbali duniani wanakisiwa kujiunga na wapiganaji wa IS nchini Syria na Iraq, robo yao ni wanawake na watoto.

Takriban watu 850 wanatoka Uingereza, wakiwemo wanawake 145 na watoto 50.

Wanamgambo hao wanaaminika kuuawa au kutekwa nyara.Haijulikani raia wangapi wa kigeni wamepoteza maisha.

Watafiti wanasema takriban wapiganaji 7,000 wamesafiri kurudi makwao.

Hatua hiyo imewia vigumu kwa serikali za nchi zao kukusanya ushahidi kwa ajili ya kufungua mashtaka dhidi yao.

Mada zinazohusiana