Watumiaji wa apps za kupata wapenzi hulazimika kutumia njia za hatari kuwa na muonekano mzuri

Mwanamke akitumia app kumpata mwenza Haki miliki ya picha Getty Images

Wanawake na wanaume wanaotumia apps ili kupata wapenzi wanaowataka , wako hatarini kutumia njia zisizofaa kiafya ili kudhibiti au kupunguza mwili, utafiti umeeleza.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani kwa watu 1,700 umebaini kujitapisha,matumizi ya dawa za kupunguza mwili na kufunga kula ni njia zinazotumika kwa wingi.

Apps za kutafuta wenza zimekua maarufu sana kutokana na kuwepo kwa mitandao ya simu na intaneti miaka ya hivi karibuni.

Watu hutumia apps kuwapata wenzi wanaofaikiri wanawafaa kwa kutazama muonekano wa miili yao pia.

Katika utafiti huu, uliochapisha kwenye jarida liitwalo Eating Disorders, watafiti wamefananisha tabia za watu wanaotumia apps kutafuta wenza na wasiotumia application hizo.

wakabaini kuwa watumiaji wa application hizo wana namna sita za kudhibiti miili yao ili kuwa na muonekano mzuri kwenye mitandao, hutumia njia ya kujitapisha, kutumia madawa ya kuharisha, kufunga kula, kutumia dawa za kujikondesha, na dawa za kujenga miili au misuli yao.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kutoka kwa watu wazima waliohojiwa 1,726,183 wanawake na 209 wanaume wamesema wanatumia apps kupata wenza.

Kwenye kundi hilo, karibu nusu ya wanaume na wanawake wameripoti kuwa wanatumia njia ya kufunga kula ili wasiwe na uzito mkubwa na mmoja kati ya wanawake watano na mwanaume mmoja kati ya watatu wanasema hujitapisha ili kuepuka kuwa na uzito wautakao.

mmoja kati ya wanawake wanne na asilimia 40 ya wanaume wanatumia dawa za kuharisha.

Dr Alvin Tran aliyeongoza jopo la watafiti amesema utafiti umebaini kuwa kuna matumizi ya hali ya juu ya njia hizi miongoni mwa watumiaji.

Homoni 'inayoweza kupunguza hatari ya kupoteza uja uzito'

Unene wa kupindukia waleta hofu Tanzania

'Muonekano wa mwili'

Dokta Tran amesema: ''Wakati hatujui kama watu kwenye utafiti huu walikua wakitumia njia hizi kabla ya kuanza kutumia apps za kuwatafuta wapenzi, tunahofu kuwa matumizi yake yanaweza kuzaa tabia hizo.

''Hapa tunapaswa kutambua madhara ya kutumia apps za wapenzi na mabadiliko ya tabia katika kudhibiti muonekano wa mwili.'' alieleza Dokta Tran

''Ni muhimu kutilia maanani kuwa utafiti huu hauthibitishi mahusiano ya moja kwa moja kati ya apps na tabia zisizofaa kiafya katika kudhibiti uzito.Hata hivyo ni muhimu kwa watumiaji wa apps ambao wanaweza kuwa hatarini kuingia kwenye tabia za kutokula vya kutosha wakapata msaada kuondokana na tabia hiyo.''