Jonas Savimbi:Kiongozi wa zamani wa Unita azikwa tena baada ya miaka 17 ya kifo chake nchini Angola

Sherehe za maziko ya Jonas Savimbi nchini Angola Haki miliki ya picha AFP

Kiongozi wa zamani wa waasi wa Unita nchini Angola, Jonas Savimbi, anazikwa tena miaka 17 baada ya kifo chake.

Maelfu ya wapiganaji wa zamani wa Unita waliokuwa wamevalia T-shirt nyeupe zenye picha ya bwana Savimbi walihudhuria sherehe hizo katika kijiji yalipokuwa makazi yake Lopitanga.

Kifo chake mwaka 2002 ndio kilisababisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa muda mrefu kukoma.

Mabaki ya mwili wake yalikabidhiwa kwa familia yake siku ya Ijumaa baada ya kutokea hali ya sintofahamu mwanzoni mwa juma.

Kiongozi wa waasi Rwanda amekamatwa vipi?

Wahamiaji 150 waondoshwa Libya

Unita imesema shughuli ya maziko itakua ni hatua muhimu katika kufikia mapatano ya kitaifa katika nchi hiyo iliyo na utajiri wa mafuta.

Hata hivyo, hakuna afisa yeyote aliyefika kwenye sherehe hizo, ripoti ya shirika la habari la Ufaransa,AFP limeeleza.

Jeneza lake lilifunikwa kwa bendera ya Unita yenye rangi ya kijani na nyekundu.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe viligharimu maisha ya watu 500,000.

Haki miliki ya picha AFP

Alishutumiwa kuchochea mauaji lakini alikua ni kiongozi aliyekua akiheshimiwa na maelfu ya watu.

Aliuawa na wanajeshi wa serikali mwaka 2002 na akazikwa haraka haraka katika makaburi ya mji wa Luena.Kaburi lake likiwekewa msalaba wa chuma kwenye udongo mwekundu, AFP imeripoti.

Sasa atazikwa karibu na baba yake.

Familia yake na maafisa wa Unita walitaka kumzika tena kwa miaka mingi bila mafanikio.

Mrithi wake Joao Lourenco, alikubali ombi lao na mwili wake ulifukuliwa mwanzoni mwa mwaka huu, wakisaidiwa na vipimo vya vinasaba (DNA) ili kumtambua

Durão Sakaíta mmoja kati ya watoto wakubwa wa Savimbi ameliambia shirika la habari la Lusa kuwa sasa familia ''hatimaye itakua na amani'' baada ya kuzikwa kwake tena.

Mada zinazohusiana