Mahujaji  kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wazuiwa kuingia Uganda Kuhiji
Huwezi kusikiliza tena

Mahujaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wazuiwa kuingia Uganda kwa hofu ya Ebola

Waumini wa Kikristo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika na duniani wamemiminika kwenye madhabahu ya Mashahidi wa Uganda ambapo watashiriki katika ibada maalum ya kila mwaka asubuhi ya leo.

Hata hivyo mahujaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameelezea kuhusu changamoto walizopata walipokuwa wakivuka kuingia nchini Uganda.

Hii ni kufuatia hatua ya mamlaka za Uganda kuwadhibiti kuhusiana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Mwandishi wa BBC mjini kampala Isack Mumena alizungumza na baadhi yao.