Ulimwengu mwingine chini ya bahari
Huwezi kusikiliza tena

Viumbe vya kipekee vilivyopo baharini - lakini mpaka lini?

Leo ulimwengu unaadhimisha Siku ya Bahari - siku iliyotengwa kusherehekea viumbe hai majini na kuhamasisha jamii kuhusu hatari inayowakabili viumbe hao.

Bahari ni makaazi ya karibu viumbe 200,000 vya majini waliyotambuliwa.

Lakini wanasayansi wanashuku huenda kuna mamilioni ya viumbe hao chini ya maji.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), karibu 40% ya mazingira ya bahari duniani yameathiriwa na shughuli za binadamu ikiwemo uvuvi, ambazo zinahatarisha maisha ya viumbe hai wa kipekee wanaokabiliwa na tishio la kuangamia.

Mada zinazohusiana