Mgogoro wa Sudan: Jeshi lawakamata viongozi wa upinzani baada ya mkutano wa upatanishi

wanajeshi Suudan Haki miliki ya picha AFP

Vikosi vya usalama nchini Sudan vimewakamata viongozi watatu wa upinzani baada ya kukutana na waziri mkuu wa Ethiopia mjini Khartoum ili kusaidia katika mazungumzo ya amani.

Mohamed Ismat wa muungano wa upinzani alikamatwa siku ya ijumaa huku Imsail jalab na Mubarak Ardol wa kundi la waasi wa SPLM-North walikamatwa mapema sikju ya Jumamosi.

Hatua hiyo inajiri siku chache tu baada ya kuzuka kwa ghasia ambapo wafuasi wengi a Upinzani waliuawa.

Kukamatwa kwao pia kunajiri siku chache tu baada ya utawala wa jeshi nchini Sudan kusema kuwa uko tayari kwa mazungumzo na muunago wa upinzani.

Je tunajua nini kuhusu kukamatwa kwao?

Siku ya Ijumaa , waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alizuru taifa hilo ili kuzipatanisha pande hizo mbili ambazo alikutana nazo katika mikutano miwili tofauti.

Lakini saa chache baadaye , habari zilisambaa kuhusu kukamatwa kwa Mohamed Ismat -mwanachama wa muungano wa upinzani na afisa mkuu wa benki kuu nchini Sudan.

Baadaye wanajeshi wanadaiwa kumkamata afisa mwandamizi wa SPLM-North Ismail jalab na msemaji Mubarak Ardol. Kiongozi wa chama hicho Yasir Arman pia alikamatwa siku ya Jumatano.

Habari za kuzuiliwa kwa viongozi huo zitazua kutoaminika kwa baraza la kijeshi linalotawala. Makundi ya waandamanaji yanapanga kuendelea na kampeni yao siku ya Jumapili.

Bwana Esmat na bwana Jalab ni viongozi wakuu wa muungano wa upinzani Freedom for Change , mwavuli wa upinzani unaoshirikisha viongozi wa maandamano na makundi ya waasi.

Haki miliki ya picha Reuters

''Hii ni sawa na baraza la jeshi kusema kwamba linapinga juhudu za mpatanishi waziri mkuu wa Ethiopia ," alisema Khalid Omar Yousef- kiongozi wa muungano wa upinzani akizungumza na shirika la habari la Reuters kufuatia kukamatwa kwa bwana Esmat.

Baraza la serikali ya mpito TMC halijatoa tamko lolote.

Muhariri wa BBC Mary Harper anasema kuwa hatua hiyo ya hivi karibuni inaonyesha kuwa upatanishi wa waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed haukuchukuliwa na umuhimu mkubwa na jeshi.

Baraza hilo linaonekana limepata matumaini ya kisiasa na ufadhili kutoka kwa Saudia , UAE na Misri , mataifa ambayo hayatilii mkazo kuwepo kwa demokrasi nchini humo.

RSF, ambalo lilijulikana kama wapiganaji wa Janjaweed lilijipatia umaarufu wake baada ya kutekeleza vitendo vya kikatili katika eneo la Darfur 2003.

Kurudi kwa wapiganaji wa Janjaweed wanaoogopwa

Wakaazi wa Khartoum wameambia BBC kwamba wanaishi kwa hofu katika mji huo.

Baadhi ya wanawake waliokamatwa na RSF waliambia BBC kwamba walipigwa na kutishia kuuawawa.

Wanasema kuwa wapiganaji hao waliwataka kunusru maisha yao na baadaye wakawafyatulia risasi.

Waathiriwa wengine wanasema walilazimishwa kunywa maji taka ambayo yalikuwa yamekojolewa.

Je mgogoro huo unaweza kutatuliwa kidiplomasia?

Siku ya Alhamisi Muungano wa Afrika ulisitisha uanachama wa Sudan mara moja na kuonya kuichukulia hatua zaidi iwapo mamlaka hayatakabidhiwa raia.

Mwenyekiti wa tume ya Muungano huo Moussa faki mahamat alitaka uchunguzi wa wazi kufanyiwa mauaji yaliotokea.

Je Sudan ndio eneo jipya la mgogoro?

Wakati wa ziara yake mjini Khartoum , waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alizitaka pande zote mbili kuwa na ujasiri na kukubaliana kuhusu hatua zaitakazolipeleka taifa hilo katika demokrasia.

Ripoti zinasema alikuwa amependekeza kuanzisha baraza la utawala wa mpito lenye raia wanane na wanajeshi saba huku kukiwa na rais ambaye atakuwa akibadilishwa mara kwa mara.

Haijulikani pendekezo hilo lilichukuliwaje.

Je ghasia hizo zilikuwa za kiwango gani?

Wanaharakati wa upinzani wanasema kuwa kitengo kinachoogopwa sana cha RSF kiliwaua watu 108 katika msako mkali huku miili 40 ikitolewa katika mto Nile mjini Khartoum siku ya Jumanne.

Maafisa hatahivyo wanasema idadi hiyo ilifikia 46.

Kiongozi wa RSF anadai kwamba wakora na watumiaji wa dawa za kulevya ndio waliofanya ghasia hizo.