Utafiti: Wataalamu wanasema kubadili mwenendo wa kulala na kuamka ndio suluhisho

Asleep in bed Haki miliki ya picha Getty Images

Kubadili mwenendo wa kulala kunaweza kubadilisha mfumo wa mwili wa mwanadamu hali ambayo inasaidia kuimarisha afya, wanasema wanasayansi wa Uingerez na Australia.

Utafiti wao uliangazia zaidi ndege aina ya "bundi", ambao mfumo wa miili yao' huwezesha kuwa macho usiku kucha .

Mfumo huo unaweza kutumiwa kwa kuhakikisha mtu analala wakati mmoja kila siku, kuepukakunywa vinywaji vilivyo na caffeine kama vile chai na kupata mwanga wa jua hasa saa za asubuhi.

Watafiti wanasema mpangilio huo unaonekana kuwa wa kawaida lakini ni muhimu kwasababu unaweza kubadilisha maisha ya watu.

Kila mtu ana saa zake za kulala ambao unaambatana na kuchomoza na kuzama kwa jua. Ndio maana tunalala usiku.

Lakni mfumo wa miili ya watu wengine inatofautiana na watu wengine.

Kuna wale wanao amka mapema, lakini hawawezi kukaa macho kwa muda mrefu wakati wa usiku; na wengine wanaoweza kukaa macho kwa muda mrefu nyakati za usiku wakati kila mtu amelala.

Watu hao wanasemeka huenda wakapata matatizo ya kiafya

Image caption Walala mapema au kuchelewa?

Wanasayansi waliwafanyia uchunguzi watu 21 ambao"hukaa macho bila kulala hadi usiku wa manane na kulala hadi saa nne asubuhi.

Walipewa maagizo yafuatayo:

  • Waamke saa 2-3 mapema kabla ya saa zao za kawaida na wapate mwangaza wa kutosha saa za asubuhi
  • Wale kiamsha kinywa mapema kadri iwezekanavyo
  • Wafanye mazoezi nyakati za asubuhi pekee
  • Wale chakula cha mchana wakati mmoja kila siku na wasile chochote baada ya saa moja usiku
  • Waache kutumia vinywaji vilivyo na caffeine baada ya saa tisa mchana
  • Wasilale baada ya saa kumi
  • Walale saa 2-3 kabla ya saa zao za kawaida na kujiepusha na sehemu zilizo na mwangaza saa za jioni
  • Wahakikishe wanalala wakati mmoja na kuamka wakati mmoja kila siku

Baada ya wiki tatu, watu hao walibadili mfumo wa mwili wao wa kulala, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliyofanywa na Vyuo vikuu vya Birmingham, Surrey na Monash.

Matokeo ya utafiti huo ulichapishwa katika jarida la matibabu, ulionesha kuwa watu wanaweza kulala wakati mmoja kila siku.

Lakini pia iliripoti viwango vya chini vya usingizi na msongo wa mawazo huku uchunguzi zaidi ukionesha kuwa hali yao ya afya pia iliimarika.

"Kufuata mwenendo rahisi wa kufanya mambo kunaweza kuwasaidia watu walio na tatizo la kulala kuimarisha afya yao ya kiakili ," alisema Prof Debra Skene kutoka Chuo kikuu cha Surrey.

"Ukosefu wa usingizi unaweza kunaweza kuathiri mfumo wa mwili wa mwanadamu, hali ambayo inaweza kumweka mtu katika hatri ya kupata maradhi kama vile ya Moyo, Saratani na Kisukari."

Haki miliki ya picha Getty Images

Kuwa na tatizo la kutolala na kuamka wakati mmoja kunaweza kuvuruga mfumo wa mwili wa mtu hali inayojulikana kama (circadian rhythm).

Mfumo wa kulala na kuamka kwa wakati mmoja kila siku unaweza kutumiwa kuwasaidia watu kuimarisha afya zao.

Watafiti hata hivyo hawakuweza kubaini ikiwa wale walio na tatizo sugu la kukesha usiku wakati wenzao wamelala wanaweza kunufaika na tiba hiyo rahisi.

"Bila shaka haja kuu ni ikiwa mtu ana tatizo sugu la kulala, anaweza vipi kubadili hali hiyo?" Dr Andrew Bagshaw, kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, aliiambia BBC.

"Hivi ni vitu vya kawaida ambavyo kila mtu anaweza kufanya ana ambavyo vinaweza kuleta mabadiliko makubwa, na kwangu hivyo ni vitu vinavyo nishangaza.

"Kuwa na uwezo wa kusaidia watu bila kwa kutumia mfumo huu rahisi wa tiba ni jambo la kutia moyo sana ." alisema.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii