Shirika la IAEA lathibitisha Iran imeongeza uzalishaji wa madini ya uranium

Rais wa Iran Hassan Rouhani (Wa 3 kushoto) akioneshwa teknolojia ya nyuklia mjini Tehran, Iran (Aprili 9, 2019)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mwezi uliopita Iran ilisema kuwa itaongeza mara dufu uzalishaji wa madini ya uranium ambayo hutumiwa kutengeza silaha za nuklia

Mkuu wa shirika la kudhibiti uundaji wa silaha za nyuklia duniani amethibitisha kuwa Iran imeongeza uzalishaji wa madini ya uranium.

Lakini mkuu huyo wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA,Yukiya Amano, amesema haijabainika wazi kama watafikia kilichokubaliwa katika mkataba wa Kimataifa wa mwaka 2015.

Mwezi uliopita Iran ilitangaza kuwa itajiondoa katika mkataba wa nuklia kama hatua ya kulipiza kisasi vikwazo ilivyowekewa na Marekani.

Bw. Amano pia amesema anahofu kuhusu taharuki iliyopo sasa kuhusu suala la mpango wa nuklia wa Iran na kutoa wito wa kufanywa kwa mashauriano.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif baadae alisema hali ya taharuki inaweza kupunguzwa kwa kukomesha kile alichokitaja kuwa "vita vya kiuchumi vya Marekani".

"Wale wanaoendeleza vita kama hivyo wasitarajie kuwa watakua salama," aliwaambia wanahabari mjini Tehran wakati wa ziara ya mwenzake wa Ujerumani, Heiko Maas.

Bw. Maas ameonya kuwa hali katika eneo hilo inaendelea kuwa "tete" na kwamba huenda ikasababisha makabiliano ya kijeshi kati ya Marekani na Iran.

Matukio yalivyojiri

Rais wa Marekani Donald Trump aliindoa taifa hilo katika mkataba wa nuklia mwaka jana na kuiwekea upya vikwazo iliyokuwa imeiondolea Iran ili kudhibiti shughuli zake za nuklia.

Maelezo ya video,

Hormuz: Kwa nini eneo hili linaweza kuathiri maisha yako duniani

Alafu mwezi uliopita akakamilisha tathmini ya Marekani kuwekea vikwazo mataifa yanayonunua mafuta kutoka Iran.

Hatua hiyo ililenga kulemaza sekta ya mafuta ya Iran, na kuzuia serikali kukusanya kodi kutokana na bidha hiyo.

Siku kadhaa baadae, Rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kuwa taifa lake linarejelea kufanya baadhi shughuli zilizokuwa zimedhibitiwa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia.

Bw. Rouhani pia aliyapatia mataifa yaliyoshirikiana kufikiwa kwa mkataba hao - Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, China na Urusi- hadi mwezi Julai kulinda uuzaji wa mafuta ya Iran dhidi ya vikwazo vya Marekani.

La sivyo Iran itakiuka vipengee vya mkataba huo hasa kile kinachopinga uimarishaji wa madini uranium.

Wakati huo,White House ilituma ndege yake iliyokua imebeba mabobu aina ya , B-52 na makombora ya ulinzi katika eneo la Ghuba katika hatua iliyoashiria "kuongezeka kwa hali ya taharuki" iliohusishwa na uamuzi wa Iran.

Kwa nini kuna mvutano?

Mgogoro ambao umekuwepo baina ya nchi hizo mbili tangu mwaka jana wakati rais Trump alipojitoa katika mkataba wa kimataifa wa mwaka 2015 uliolenga kumaliza mpango wa nyuklia nchini Iran.

Jambo la kuona makubaliano hayo kuwa na kasoro, Trump aliamua kuweka vikwazo.

Iran iliamua kuacha kutekeleza kile ambacho ilihaidi kufanya mwanzoni mwa mwezi wa Mei na kutishia kuanza kutengeneza tena nyuklia.

Meli na ndege za jeshi zilizotumwa nchini Iran ambazo wafanyakazi wake sio wa dharura wametakiwa kuondoka.

IAEA imesema nini?

Sikiu ya Jumatatu, mkuu huyo wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA,Yukiya Amano alithibitisha kuwa Iran imeongeza uzalishaji wa madini ya kutengeneza silaha.

Lakini alikataa kutoa maelezo zaidi kuhusiana na suala hilo japoa liongeza kuwa hawajabainisha ikiwa madini iliyozalishwa kufikia sasa imepita kiwango kilichowekwa.

Aliiambia Bodi ya usimamizi ya IAEA kuwa ni vyema Iran ihakikishe inatekeleza mkataba wa kimataifa wa nyuklia kikamilifu.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mkuu wa IAEA Yukiya Amano ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na mvutano uliopo kuhusu mpangow anyuklia wa Iran

Tahadhari ya ndege na meli

Wakati viongozi kutoka pande zote mbili wamesisitiza kuwa hawataki vita itokee, lakini bado mvutano ni mkubwa.

Wanadiplomasia kutoka Marekani wametoa tahadhari kuhusu ndege za kibiashara ambazo zinaenda katika maeneo hayo kuwa ziko hatarini.