Kanisa katoliki lahoji utambulisho wa wapenzi ya jinsia moja

Waraka wa kanisa Katoliki umetolewa wa wakati wapenziwa jinsia moja wakiendelea na sherehe za mwezi wa kujivunia jinsia zao Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waraka wa kanisa Katoliki umetolewa wa wakati wapenziwa jinsia moja wakiendelea na sherehe za mwezi wa kujivunia jinsia zao

Uongozi wa makao makuu ya kanisa katoliki umetoa waraka wa mwongozo unaopinga dhana ya kisasa juu ya utambulisho wa jinsia.

Mwongozo huo wenye kurasa 31 za mafundisho, umetolewa ukiwa na kichwa cha taarifa ''Mungu aliumba Mke na mume''

Mwongozo huo unazungumzia "mzozo wa mafundisho" na kuongeza kuwa mjadala wa sasa kuhusu jinsia unaweza "kupotosha dhana asilia " ya jinsia na kuyumbisha familia.

Waraka huo ambao umetolewa wa wakati wapenziwa jinsia moja wakiendelea na sherehe za mwezi wa kujivunia jinsia zao , umekosolewa mara moja na makundi ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadilisha jinsia zao LGBT.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kanisa katoliki limesema jinsia ya mtu haimriwi na watu binafsi bali huamriwa na Mungu pekee na kwamba maandiko matakatifu yamefichua busara ya Mungu ya mtindo wake wa uumbaji ,ambaye alimpatia binadamu kazi ya mwili , kazi ya mwanamme na mwanamke

Waraka huo wa kanisa katoliki umetolewa na kongamano la Katoliki la Elimu kama mwongozo wa mafunzo kwa wale wanaohusika na masuala ya watoto.

Waraka huo haukutiwa saini na Papa Francis mwenyewe, lakini uliinukuu kauli yake na maandiko ya biblia kuhusiana na jinsia zilizoumbwa na Mungu kulingana na kanisa katoliki.

Waraka unasemaje?

Waraka unatoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo, lakini unatoa mwongozo juu ya masuala kadhaa yakiwemo yanayohusu jamii ya watu wanaobadilisha jinsia yao.

Unakosoa vikali uelewa wa kisasa kuhusu jinsia na kulifanya suala la jinsia kuwa gumu kuliko ilivyo kawaida ambapo kuna wanaume na wanawake.

Waraka huo umeendelea kusema kuwa nadharia za kisasa "zinapinga maumbile halisi " na badala yake " linakuwa ni swala la hisia za binadamu ".

Waraka huo unasema pia kwamba utambulisho wa jinsia "mara nyingi hauna msoingi wowote isipokuwa ni dhana potofu ya mkanganyiko wa uhuru wa hisia za mtu na vile anavyotaka yeye kuonekana na kutambulika ".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwongozo wa umetolewa wakati wapenzi wa jinsia moja wakisherehekea mwezi wa kujivunia jinsia yao

Waraka huo unaendelea kusema kuwa jinsia haiamriwi na watu binafsi bali huamriwa na Mungu pekee: " Maandiko matakatifu yamefichua busara ya Mungu ya mtindo wake wa uumbaji ,ambaye alimpatia binadamu kazi ya mwili , kazi ya mwanamme na mwanamke ."

Image caption Wapenzi wa jinsia moja

Waraka huo unasema kuwa taasisi zinapaswa kufundisha jamii kwa usawa juu ya "asili ya kweli ya wanadamu"kwa kuzingatia "elimu ya historia na tabia ya maendeleo ya binadamu kwa uwazi na kwa njia inayoaminika ".

Image caption Wapenzi wa jinsia moja katika moja ya matembezi ya kujivunia jinsia zao. Matembezi haya hufanyika kila mwaka katika nchi mbali mbali hususan za magharibi

Hata hivyo, waraka huo unasema kwamba waoto na vijana wanapaswa kufundishwa kumuheshimu kila mtu ili asiwepo hata mmoja atakayeumizwa na matusi au ubaguzi wa aina yoyote ile

Kundi la New Ways, lenye makao yake nchini Marekani ambalo linatetea wapenzi wa jinsia moja Wakatoliki, limeelezea waraka huo wa kanisa katoliki kama '' zana hatari'' ambayo itatumiwa "kuwadunisha na kuwadhuru watu waliobadilisha jinsia zao, pamoja na wapenzi wa jinsia moja wakike na wakiume ".

Mkurugenzi New Ways- Francis DeBernardo, amepinga vikali dhana kuwa watu "huchagua jinsia zao".

Katika taarifa iliyojibu waraka wa kanisa katoliki ,Francis DeBernardo , alisema kuwa waraka huo ''utawakanganya wale wanaohangaika kutafuta jinsia yao " na akaelezea kuwa Vatican imekuwa "katika kipindi cha giza " kuhusiana na suala la utambulisho wa jinsia.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii