Utoaji Damu: Ukweli kuhusu nani anaweza kuchangia damu

damu Haki miliki ya picha UniversalImagesGroup

Kuna masharti mengi yanayoambatana na kutoa au kuchangia damu kuwasidia wagonjwa wanaohitaji.

Lakini pia kuna imani nyingi potofu na mambo yasio ya kweli ambayo watu wanayaamini.

Je masharti ni yapi ya kuchangia damu?

Watu wasiokula nyama hawapaswi kuchangia damu

Kumekuwa na imani potofu kuhusu utoaji damu na kumefanywa utafiti kulibaini hili ikiwemo fikra kuhusu watu wasiokula nyama kuwa hawawezi kutoa damu.

Wasiwasi unatokana na kiwango cha madini ya iron - kiini kikuu cha damu mwilini - na wasiwasi kwamba wasiokula nyama hawapati madini haya ya kutosha.

Iwapo damu yako haina madini ya kutosha, hauwezi kuruhusiwa kutoa damu kutokana na usalama wako.

Haki miliki ya picha YASUYOSHI CHIBA

Lakini ni kwamba kama unakula lishe bora yenye virutubisho vizuri, basi bila shaka utapata madini ya kutosha ya iron mwilini.

Kama una michoro ya tattoo au umetobolewa mwili, sio marufuku

Unaweza kuchangia au kutoa damu hata kama una michoro ya tatoo au umetobolewa mwilini, tofauti na baadhi ya watu wanavyoamini.

Hatahivyo kuna sheria: N lazima usubiri kwa miezi minne kutoka siku uliochorwa tatoo au kutobolewa mwilini kabla ya kuweza kutoa damu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hakikisha unaifahamu tarehe ulipochorwa tatoo ya mwisho kabla ya kutoa damu

Na iwapo umetoa damu kwa kati ya miezi minne na mwaka mmoja baada ya kuchora tatoo au kujitoboa mwili, huenda ukafanyiwa ukaguzi wa ziada katika kituo cha kutoa damu.

Usihofu hakuna kiwango cha mwisho cha damu mwilini

Mtu mzima yoyote ana kiasi cha painti 10 za damu mwilini.

Unapotoa mchango wa damu huwa unatumia kama painti moja, na mwili hufanya kazi kurudisha seli na maji uliopoteza mwilini. Damu uliochangisha kwa kawaida inarudi mwilini baada ya siku moja.

Kama ni mgonjwa, huenda unahitaji kusubiri muda zaidi

Kwa kawaida mtu anastahili kupoa kikamilifu baada ya maambukizi ya aina yoyote angalau siku 14 kabla ya kutoa damu - na iwapo umekuwa ukinywa dawa za antibiotic inabidi usubiri siku 7 baada ya kumaliza kunywa dawa ndipo uweze kuchangia dawa.

Kama unatumia dawa maalum, uliza katika kituo kilicho karibu na wewe kujua iwapo unaweza kuchanga damu.

Sheria za kushiriki ngono hazitatizi

Unaweza kutoa damu wakati wowote isipokuwa iwapo...

Wewe ni mwanamume aliyeshiriki ngono na mwanamume mwingine katika miezi mitatu iliyopita.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kuna sheria kwa wapenzi wa jinsia moja wanaume inayofanya kuwa vigumu zaidi kwao kuchangisha damu

Umeshiriki ngono na mpenzi ambaye anatumia dawa zozote katika miezi mitatu iliyopita.

Wewe ni mfanyabiashara ya ngono - licha ya kwamba unaweza kukubaliwa iwapo hujalipwa au kutumia madawa kushiriki ngono katika miezi mitatu iliyopita.

Kwa ujumla, unaweza kuchangia damu iwapo...

  • Una nguvu na afya
  • Una uzito wa kati ya Kilo 50 na kilo 160
  • Una umri wa kati ya miaka 17 na 66
  • Una umri wa zaidi ya miaka 70 na umewahi kutoa damu katika miaka miwili iliyopita

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii