Mahakama kuu ya Botwana yafuta sheria zinazozuwia mapenzi ya njinsia moja

Huwezi kusikiliza tena
Mwanaharakati akipeperusha bendera mahakamani

Majaji wa mahakama ya juu zaidi nchini wameamua kuwa sheria zinazoyafanya mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja kuwa uhalifu zinakiuka katiba ya nchi na zinapaswa kuondolewa, katika kile kinachotajwa kuwa ni ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja barani Afrika.

Uamuzi huu ulipotangazwa mahakamani wanaharakati wa haki za mapenzi ya jinsia moja wali waliokuwa wamefurika mahakamani walililipuka kwa furaha, shangwe na vigelegele, kufuatia kupitishwa kwa sheria inayohalalisha mapenzi ya jinsia moja. Furaha yao ilionekana ndani na nje ya mahakama baada ya hukumu kutolewa:

Hatua hii ya mahakama ya Botswana inakuja mwezi mmoja tu baada ya Kenya nia ya wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja ya kurekebishwa kwa sheria inayoyazuwia kukataliwa na mahakama ya Kenya.

" Utu wa binadamu unapata madhara wakati makundi ya walio wachache yanabaki nyuma," Alisema Jaji Michael Leburu alipokuwa anasoma hukumu . " Jinsia ya mtu si mtindo wa fasheni. Ni utambulisho wa maana wa utu."

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Baadhi ya wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya walisikitika baada ya mahakama kukataa kurekebisha sheria inayopinga uhusiano huo tarehe 24 May, 2019

Hukumu hiyo ilipokelewa kwa shangwe kubwa na wanaharakati wanaoendesha kampeni za wapenzi wa jinsia moja kote barani Afrika, ambako mahusiano ya mapenzi hayo ni kinyume cha sheria za nchi nyingi. Katika baadhi ya nchi za Afrika watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja hukabiliwa na kifungo cha maisha jela au hukumu ya kifo. Baadhi walionyesha furaha zao kwenye mitandao ya kijamii kwa picha za kuunga mkono hukumu ya Mahakama ya Botswana:

Botswana inaonekana kama moja ya nchi za Afrika thabiti zilizokomaa kidemokrasia, lakini mahusiano ya kimapenzi ya watu w ajinsia moja yalikuwa ni kinyume cha sheria chini ya sheria ya nchi hiyo ya mwaka 1965.

"Taifa lenye demokrasia ni lile linalozingatia kukubali tofauti, uvumilivu na kuwa tayari kupekea mawazo ya watu tofauti, umoja wa jamii kama msingi wa kumaliza umaskini na kuharakisha maendeleo ya pamoja … taifa haliwezi kuingilia mambo ya vyumbani mwa watu ," alisema Jaji Leburu.

Kampeni za kupigania haki ya kimapenzi ya watu wa jinsia moja nchin Malawi pia ilimuhusisha Mchungaji wa kanisa la Lutheran Reverend Thabo Mampane ambaye alisema kanisa linapaswa kuwa sauti ya wasio na sauti :

Mwezi Machi, mahakama iliahirisha hukumu juu ya suala hilo baada ya mtu mmoja ambaye hakutajwa jina kupinga vipengele viwili vya sheria inayohusu mapenzi ya jinsia moja ambavyo vilisema kuwa mtu anayepatikana na hatia anaweza kukabiliw ana kifungo cha jela cha miaka hadi saba.

"Huu ni uamuzi wa kihistoria kwa wapenzi wa jinsia moja wake kwa waume, wenye jinsia mbili na waliobadilisha jinsia zao nchini Botswana," alisema Gunilla Carlsson, Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoaj wa Mataifa la ukimwi UNAids. "Sheria hii inarejesha hali ya usiri, heshima na utu kwa watu wanaoshiriki mapenzi wa jinsia moja, na ni siku ya kusherehekea utu ,huruma na upendo."

Thato Game Tsie, muhudumu wa masuala ya afya anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja, amesema kuwa kufutwa kwa sheria inayozuwia mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja kutasaidia jamii ya watu hao kupata huduama za afya na matibabu kwa urahisi zaidi . " Kuna huduma nyingi tunazoihitaji kama wapenzi w ajinsia moja wanaume ambazo baadhi ya wauguzi hawazifahamu , na kama tukienda katika hospitali za serikali wanakusimanga ," alisema Game Tsie. " Kwa hiyo tunataka tu kuwa huru kupata huduma hizi ."

Majaji wa kenya walipinga hukumu iliyotolewa na majaji wa India, iliyo halalisha kisheria ngono ya watu wa jinsia moja walio na umri wa utu uzima, pamoja na msururu wa hukumu nyingine zilizotolewa kote katika nchi wanachama wa Jumuiya ya madola na kwingineko, na wakasema Kenya inapaswa kutunga sheria zake zitakazoendana na utamaduni wake.

Ngono baina ya watu wa jinsia moja ni kosa linaloadhibiwa kwa kifo katika maeneo ya Kaskazini mwa Nigeria , Sudan, Somalia na Mauritania.

Image caption Tanzania ni moja ya chi ambazo mapenzi ya jinsia moja hayakubaliki

Sheria za Tanzania zinaweza kumsababishia anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja kufungwa kifungo cha maisha jela.

Angola,Msumbiji na Ushelisheli kwa pamoja ziliondoa sheria zinazokataza mapenzi ya jinsia moja katika miaka ya hivi karibuni.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii