Trump afichua mpango kuhusu uhamiaji alipopunga karatasi hiyo mbele ya wanahabari

Donald Trump Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Donald Trump akiwa ameishika karatasi iliyoandikwa makubaliano yake na Mexico

Rais wa Marekani,Donald Trump kwa bahati mbaya ameweka wazi sehemu ya waraka wa makubaliano kati ya Marekani na Mexico kuhusu uhamiaji.

Alikataa kuzungumza na waandishi wa habari akisema kuwa, makubaliano hayo yalikua ''siri''.

Lakini alisema hayo huku akiionyesha karatasi ambayo ilikua na maandishi kuhusu makubaliano hayo -ambayo yalipigwa picha na wana habari.

Rais Trump amefaya suala la mpaka kati ya Marekani na Mexico kuwa sehemu kubwa ya kampeni yake kwenye makubaliano hayo akitishia kuwekea ushuru Mexico.

Trump atishia kufunga mpaka kati ya Marekani na Mexico

Marekani yatoa dola $1b kujenga ukuta kati yake na Mexico

Kwenye karatasi hiyo kulisomeka maneno kuwa Mexico iliridhia muda uliowekwa kuhakikisha kuwa inafanikiwa kupambana na suala la wahamiaji.

Ikiwa Marekani itajihakikishia kuwa hatua zilizochukuliwa ''hazikuzaa matunda'', Mexico italazimika kuchukua hatua kali zaidi za kisheria kushughulikia suala la uhamiaji.

Mexico imesema nini kuhusu makubaliano hayo?

Waziri wa mambo ya nje wa Mexico, Marcelo Ebrard imethibitisha kuwa Mexico ilikuwa na siku 45 kuonyesha kuwa ina uwezo wa kudhibiti wahamiaji wanaoingia Marekani kwa kuimarisha usalama katika mpaka wake wa kusini.

Kwa sasa imepeleka askari 6,000 katika mpaka wake na Guatemala.

Haki miliki ya picha Reuters

''Unapokenda kusini, jambo la kwanza kujiuliza ni: 'mpaka uko wapi?' Hakuna kitu, ''alisema siku ya Jumanne. ''Mpango ni kufanya mpaka wa kusini uwe kama wa kaskazini haraka iwezekanavyo.''

Ikiwa mpango huu hautafanikiwa,waziri wa mambo ya nje amesema, Mexico ilikubali kuwa nchi ya tatu itakayolazimu wanaotafuta hifadhi Marekani kwanza kuomba hifadhi Mexico, mpango ambao Marekani ilipendekeza lakini ulikataliwa vikali na Mexico.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji kutoka Honduras wakijaribu kuvuka mto wa Rio Bravo ili kwenda kuomba hifadhi El Paso,Texas

Ikiwa Mexico itashindwa kushughulikia suala la uhamiaji katika kipindi cha siku 45, nchi nyingine zitahusishwa kwenye sakata hilo.

Mazungumzo yatahusisha pia Brazil,Panama na Guatemala- nchi ambazo kwa sasa hutumiwa kama vituo vya kupitishia wahamiaji.Nchi hizo ambao watagawana jukumu la kushughulikia madai ya watu wanaotafuta hifadhi.

Bwana Ebrard pia amesema wapatinishi wa Marekani walitaka Mexico ikomeshe kabisa wahamiaji kuvuka lakini ''mpango huo haukuwezekana''.