Lionel Messi: Kwanini nyota huyu wa Argentina amekua akikabiliwa na mkosi katika soka ya Kimataifa

Lionel Messi Haki miliki ya picha Getty Images

Argentina inafahamu fika kuwa Lionel Messi ni mchezaji wa kipekee ambaye ni kiungo muhimu sana kwake.

Lakini miaka 14 baada ya kushiriki soka ya kimataifa nyota huyo hajafanikiwa kuonesha umahiri wake uwanjani huku miaka yake ikiendelea kuyoyoma.

Jinamizi hilo limemuandama hata katika kuiwakilisha nchi yake Messi, ambaye hivi karibuni anatimiza miaka 32.

Kila shindano linakuja na matarajio makubwa na baadae yanageuka kuwa usumbufu wa kiakili kwake.

Mwaka wa 2007 alishinda kombe la Dunia kwa wachezaji wa chini ya miaka 20 na mwaka mmoja baadae akashinda dhahabu katika mashindano ya Olympiki ya Beijing lakini hajawahi kushinda taji kubwa la kimataifa.

"Nitajitahidi nijaribu tena , haijalishi nitanguka mara ngapi. huu ndioa ujumbe wangu kwa watoto, sio kwa kandanda peke yake bali pi akwa mambo mengine maishani, lakini nataka kustaafu nikiwa nimeifanyia kitu Argentina," Messi alisema hayo mwezi iliopita.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kabla ya Argentina kucheza na Croatia katika mechi ya makundi ya Kombe la Dunia, Messi alionekana kupata usumbufu

Huku michuano ya Copa America ikitarajiwa kuanza nchini Brazil, Nahodha Messi anajua kuwa itakuwa nafasi yake ya mwisho kuishindia Argentina taji kuu.

Messi ni mfungaji bora wa mabao(67) wa Argentina lakini hajafikia kiwango cha kuvikwa taji la kuishindia taifa hilo katika michuano ya hadhi ya kimataifa. Amecheza mara 130, ikiwa ni 17 chini ya mchezaji Javier Mascherano aliyestaafu.

Katika mashindano 8 ambayo ameiwakilisha Argentina (Kombe la dunia mara 4, Copa America mara 4) yaliibua maswali: Ikiwa huyo ni mchezaji yule yule ambaye Wargentina wanafurahia kumuona uwanjani akiichezea Barcelona ?

Kumekuwa na dhana kwamba kuna Messis wawili. Yule ambaye anang'ara katika klabu ya Barcelona ambayo ameicheza na marafiki zake Andres Iniesta na Xavi tangu akiwa mdogo akiwa katika chuo cha Barca cha soka ya vijana.

Upande mwingine, anaonekana kama mgeni aliyejawa na kiburi na majigambo anayechezea timu ya taifa na ambaye amecheza mechi 16 zaidi ya miaka miwili bila kufunga bao, kati ya mwaka 2009 na 2011.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gabriel Batistuta (kushoto) na Diego Simeone (katikati) walikua miongoni mwa wachezaji nyota wa Argentina katika michuano ya mwaka 1993 ya Copa America

Alijipata akikosolewa katika kila shuindano la Copa America na kila shindano la Kombe la Dunia aliloshiriki lilitia dosari hatma yake ya siku zijazo katika soka ya kimataifa.

Lakini nyota huyo hata baada ya kukosolewa na kuachwa na machungu ya kuikosesha nchi yake ushindi - Messi, alirejea Uhispania na kuonesha umahiri wake uwanjani jambo ambalo linamsaidia kupona maumivu ya moyoni aliopata akiiwakilisha timu ya taifa ya Argentina.

Barca ni mahali ambap, hofu yake kuhusu uwezo wa kucheza mpira ilitokomea na kumwezesha kuchukua usukani wa uongozi katika fani ya soka.

Kwanini iwe huko na sio hapa?

Hayo ni maswali ambayo yamekuwa yakiwaumiza vichwa wasimamizi wa soka nchini Argentina.

Wamekuwa wakijiuliza tunafanya kosa gani, anahitaji nini? n akila wakijaribu kupata ufumbuzi wa maswali hayo wanapata matumaini zaidi.

Kadri wanavyomshirikisha katika timu ya taifa ndivyo wakosoaji wake wanavyozidi kuongezeka hali inayojirudia katika kila mashindano ya kimataifa.

Lakini sasa mambo yamebadilika na jinamizi la Messi kushindwa katika timu ya taifa sasa linaonekana kuelekea Barcelona.

Hatua ya Liverpool kuiondoa Barcelona katika micuano ya klabu bingwa barani Ulaya iliwashangaza wengi kwasababu klabu hiyo ilikuwa imeondolewa katika mashindano hayo kwa mwaka wa pili mfululuzo.

Pia kulikuwa na kisa cha kushindwa katika fainali ya michuano ya Copa del Rey, ambapo Valencia walichukua ushindi.

Barca huenda walishinda La Liga, lakini matarajio yalikuwa juu kulingana na vyombo vya habari Messi na rafikia yake Luis Suarez walitofautiana vikali katika chumba cha kubadilisha nguo.

Hali itakua vipi endapoArgentina, hatimae itageuka kuwa kliniki ya kutuliza maumivu ya Messi kushindwa katika klabu yake ya Barcelona?

Mara ya mwisho Argentina kushinda taji kuu la soka ya kimataifa ni mwaka 1993 ilichukuwa ubingwa wa michuano ya Copa America.

Kutoka wakati huo wamshindwa fainali ya Copa America mara nne (2004, 2007, 2015, 2016) na fainali ya kombe la dunia (2014). Katika mashindano hayo matano, Messi alicheza mara nne na hukufunga hata bao moja.

Matumaini ya Argentina kupata ushindi soka ya kimataifa yanakabiliwa na mgawanyiko wa mashabiki hali ambayo inatilia shaka ikiwa taifa hilo litawahi kukabiliana na ukame wa miaka 26.

Baadhi ya mashabiki wanamchukulia Messi kama mkombozi, wengine wanamsubiri kumuona akifeli, ili wapate nafasi ya kumshambulia tena.

Huku hayo yakijiri mjadala kuhusu utenda kazi wa nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, umeanza tena taifa hilo linapojiandaa kushiriki michuano ya kimataifa.

Kwa kizazi cha sasa,Messi ni kama mungu wao. Kwa kizazi cha kale umahiri wa Diego Maradona - hauwezi kulinganishwa na Messi kwani kamwe hawezi kuwa Diego.

Kwao Mesi hawezi kushinda kombe la dunia peke yake, kama alivyodaiwa kwafanya Maradona mwaka 1986. Na pengine akifanya hivyo kiwango cha Messi hakitawahi kumfikia Maradona.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii