Ummy Mwalimu: Tanzania Kenya, zazindua mpango wa ukaguzi wa Ebola mipakani

@umwalimu Haki miliki ya picha @umwalimu

WaTanzania wameombwa "wasiwe na hofu" kuhusu kusambaa kwa Ebola, waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema kufuatia taarifa za Ebola kuingia Uganda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mpaka wa Tanzania unashikana na wa Congo, ambako virusi vya ugonjwa huo vimesababisha vifo vya takriban watu 1, 400.

Kauli hii inatolewa wakati Uganda imethibitisha kwamba kuna visa visaba vya watu wanaoshukiwa kuugua ugonjwa huo nchini.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, Bi Mwalimu amesema Tanzania "imekuwa ikichukua hatua za utayari wa kukabiliana na ugonjwa huu"

Hapo jana Tanzania, pamoja na Kenya, zilizindua mpango wa ukaguzi wa watu wanapovuka mipaka kuingia katika nchi hizo.

Mpango huo utawasaidia maafisa kusambaza kwa haraka taarifa kuhusu iwapo kumegunduliwa visa vyovyote vya Ebola, waziri huyo ameeleza.

Nchini Uganda mtoto wa miaka mitano aliyepatikana na Ebola alifariki hapo jana , kikiwa ndicho kisa cha kwanza kuthibitishwa nchini humo.

Huwezi kusikiliza tena
mahujaji wa DRC wazuiwa kuingia Uganda kutokana na tisho la Ebola

Wizara ya afya nchini Kenya kwa upande wake imetoa taarifa ikisema imetoa tahadhari kwa maafisa wote wa afya na umma kushinikiza hatua za uangalizi.

Wizara hiyo imeeleza kwamba inaendelea kuufuatilia mlipuko huo wa muda mrefu katika jamhuri ya Kideokrasi ya Congo ulioanza mnamo Agosi mwaka jana, kwa lengo la kuimarisha utayari na muitikio wa wa Kenya katika kukabiliana na visa vya ugonjwa huo.

Wizara ya afya nchini Rwanda imetoa wito kwa umma na mashirika yanayohusika kuimarisha hatua kuzuia Ebola kuingia ndani ya nchi hiyo.

Kuutambua ugonjwa wa Ebola

  • Ni ugonjwa unao sambaa haraka na hupelekea vifo vya asilimia 50 ya waathirika
  • Dalili za awali ni homa ya ghafla, uchovu kupita kiasi, maumivu ya mishipa na koo.
  • Dalili za hatari ni kutapika, kuharisha, na kwa kesi zingine ni kutoka damu ndani na nje ya mwili.
  • Ebola huwapata binadamu wanapo gusana na wanyama walio athirika wakiwemo sokwe mtu, popo na paa.
  • Watu wanaambukiza endapo damu zao na maye vimebeba vijidudu, na hii inaweza fika mpaka wiki saba tangu mtu alipopona.
Image caption Wataalamu wa Afya nchini DRC

Uganda imekabiliana vipi na Ebola siku za nyuma?

Serikali ya Uganda imeidhinisha matayarisho makubwa kwa hali inayoshuhudiwa sasa:

1. Ni muhimu kukubuka kwamba serikali imeidhinisha mifumo na utaalamu kukabiliana na Ebola kwa usaidizi wa taasisi za udhibiti wa magonjwa za Marekani na shirika la afya duniani. Madakatri wa Uganda wamewahi kutumwa kwenda kusaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo ulipozuka Congo na mataifa ya Afrika magharibi.

2. Ukaguzi na uthibitisho wa visa: majaribio yote hufanyika nchini Uganda katika maabara ya serikali. Iwapo serikali imeshindwa kuthibitisha sampuli nchini, basi zinasafirishwa katika makao makuu ya udhibiti wa magonjwa Atlanta Marekani.

3. Serikali ndio huthibitisha mlipuko, visa, au vinavyoshukiwa.

4. Kilichoisaidia Uganda kukabiliana na ugonjwa huu ni mamlaka ilio nayo kuhusu suala hili na kupeuka uvumi, na uzushi jambo linalochangia imani kutoka kwa umma.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii