Shambulizi la meli ya mafuta katika Ghuba: Iran yasema madai ya Marekani hayana msingi

Shambulio la meli ya mafuta ambalo marekani inasema lilitekelezwa na Iran

Iran imesema kuwa imepuuzilia mbali madai ya Marekani kwamba ndio iliotekeleza shambulio dhidi ya meli mbili za mafuta katka Ghuba ya Oman.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo aliilaumu Iran kwa kutekeleza shambulo hilo siku ya Alhamisi.

Aliongezea kwamba Marekani iliamua kuchukua uamuzi huo kutokana na ujasusi kuhusu silaha zilizotumika.

Lakini Iran ilipinga madai hayo kama yasio ya msingi. Afisa mmoja mwandamizi kutoka Iran awali alikuwa ameambia BBC kwmba Iran haihusiki na mashambulio hayo.

Makumi ya wafanyikazi wa meli hizo waliokolewa baada ya milipuko hiyo katika meli zinazomilikiwa na Japan ya Kokuka Couregeous na Front Altair inayomilikiwa na kampuni ya Norway.

Katika taarifa iliotolewa siku ya Ijumaa, Ujumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa ulisema: Iran inapinga madai hayo ya Marekani ikizingatia shambulio la tarehe 13 mwezi Juni na kulishutumu kwa hali na mali.

Muda mfupi baada ya kukana , afisi kuu ya jeshi la Marekani lilitoa kanda ya video iliosema inaonyesha jeshi la Iran la IRG likitoa bomu ambalo halikulipuka kandakando ya meli ya Kokuka Courageous kufuatia shambulio hilo.

Mlipuko huo unajairi mwezi mmoja baada ya meli nne za mafuta kuharibiwa katika shambulio ambalo halijadaiwa kutekelezwa na upande wowote katika bahari ya UAE . Wakati huo Marekani iliilaumu Iran -lakini Tehran ilikana madai hayo.

Bei ya mafuta ilipanda kwa asilimia 4 baada ya kisa hicho cha Alhamisi katika Ghuba ya Oman, ambayo iko kaitika eneo moja muhimu la meli ambapo mamia ya madola ya mafuta yanapitia.

Muungano mkubwa wa meli duniani BIMCO, umesema kuwa hali ya wasiwasi katika eneo hilo iko juu licha ya kuwa hakuna vita vinavyoendelea.

Wakati huohuo waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza alionya kuwa iwapo Iran imehusika- ni hatari kwa udhabiti na usalama wa eneo hilo

Mike Pompeo alisema nini?

Ni maono ya Marekani kwamba taifa la Iran linahusika na shambulio hili , alisema waziri hyo katika mkutano na vyombo vya habari mjini Washington.

"Uchunguzi huo unatokana na ujasusi , silaha zilizotumika, utaalamu wa hali ya juu uliotumika kutekeleza shambulio hilo, mashambulio kama hayo yaliotekelezwa na Iran katika siku za hivi karibuni dhidi ya meli na ukweli kwamba hakuna kundi linlotekeleza operesheni zake katika eneo hilo linaweza kutekeleza shambulio hilo kwa kiwango cha juu .

Hatahivyo Pompeo hakutoa ushahidi wowote.

''Hili ni shambulizi la hivi karibuni miongoni mwa msuuru wa mashambulio yaliotekelezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na washirika wake dhidi ya Marekani na washirika wake. Mashambulio hayo ynayonyesha wazi tishio la amani na usalama wa kimataifa-ikiwa ni unyanyasaji wa biasharavza meli mbali na kuwa ni kampeni isiokubalika inayosababisha hali ya wasiwasi'', alisema Pompeo.

Tunajua nini kuhusu mlipuko huu?

Mamlaka ya baharini nchini Norway ilisema mapema siku ya Alhamisi kwamba meli ya Front Altair ilishambuliwa na kwamba kulikuwa na milipuko mitatu ilioikumba.

Wu I-fang, msemaji wa Taiwan COP Corp Oil Rifiner , ambayo inamiliki Front Altair , ailisema kuwa inabeba tani 75,000 za naptha na ilidaiwa kushambuliwa na Torpedo ijapokuwa hilo halijathibitishwa.

Ripoti nyengine ambazo hazijathibitishwa zilidai kwamba shambulio hilo linatokana na bomu.

Mmiliki wa meli hiyo, Frontline, alisema kuwa meli hiyo ilishika moto lakini akakana ripoti kutoka kwa vyombo vya habari vya Iran kwamba ilikuwa imezama.

Mmiliki wa Kokuka Couregeous, BSM Ship Management alisema kuwa wafanyikazi wake waliondoka katika meli hiyo na wakaokolewa na chombo kilichokuwa kikipita.

Maelezo ya picha,

Wafanyikazi 21 katika meli hiyo ya Courageous kushoto na wengine 23 kutoka kwa meli ya 23 kutoka kwa meli ya Front Altair wameokolewa

Kwa nini kuna hali ya wasiwsai kati ya Marekani na Iran

Mwaka 2018, Marekani ilijiondoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran ulioafikiwa 2015 ambao lengo lake ulilenga kupunguza vitendo vya kinyuklia vya Iran.

Hatua hiyo ilikosolewa na mataifa mengi , ikiwemo washirika wa karibu wa Marekani.

Mnamo mwezi Mei rais Donald trump aliimarisha vikwazo dhidi ya taifa hilo-vikilenga sana sekta yake ya mafuta.

Iran baadaye ilitangaza kwamba ilikuwa inakiuka baadhi ya makubaliano chini ya mkataba wa nyuklia.

Katika miezi ya hivi karibuni Marekani iliimarisjha jeshi lake katika eneo la Ghuba likisema kuwa kuna hatari ya kushambuliwa na Iran.

.

Imetuma meli ya kubeba ndege za kivita na ndege aina ya B-52 katika eneo hilo.

Ikijibu hatua hiyo , Iran imeshutumu Marekani kwa tabia yake ya uchokozi.

Wasiwasi huo ulizuka baada ya shambulio la mabomu katika meli nne UAE

Je ujasusi unasema nini?

Ni uamuzi wa haraka uliotolewa na Pompey lakini kufikia sasa ni maelezo machache yaliotolewa kuhusu ujasusi na kiwango cha tathmini ya uharibifu uliofanyika katika meli hizo mbili ukizingatia maelezo ya setlaiti ama vifaa vyovyote vinavyofuatilia mwenendo wa chombo chengine chochote kile.

Wengine wanahoji kwamba kuna hatari ya kutoa uamuzi kama huo.

Lakini ni wazi kwamba iwapo Marekani inataka kujibu hilo kupitia jeshi lake basi mataifa mengi -ikiwemo hata wale marafiki zake watataka kuonyeshwa ushahidi wa ujasusi wa Marekani.