Nigeria: Polisi wachunguza iwapo nyani alimeza mamilioni ya pesa

Maelezo ya picha,

Inadaiwa kuwa nyani alimeza karibu milioni saba sawa na dola elfu 19 za kimarekani zilipotelea kwenye hifadhi ya wanyama Gardens katika jimbo la Kano

Polisi katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Kano, wamethibitisha kuwa wanafanya uchunguzi kubaini vi vipi kiasi cha pesa za Nigeria (naira) karibu milioni saba sawa na dola elfu 19 za kimarekani zilipotelea kwenye hifadhi ya wanyama inayojulikana kama Kano Zoological Gardens.

Msamaji wa polisi wa jimbo la Kano, DSP Abdullahi Haruna, ameithibitishia Idhaa ya BBC Pidgin kuwa wanachunguza kisa hicho.

" Ndio ni ukweli pesa zilipotelea kwenye hifadhi ya wanyamaya Kano na pesa hizo zilitakiwa kutumika kwa ajili ya tamasha la siku tano Sallah. Hadi sasa tumekwisha wakamata wafanyakazi 10 wa hifadhi hiyo ya wanyama na wanahojiwa na idara ya upelelezi- CID.

"Miongoni mwa watu waliokamatwa ni mlinzi wa hifadhi ya wanyama, na wafanyakazi wa idara ya fedha na tunataka kufahamu ni kwanini walificha kiasi hicho kikubwa pesa kwenye hifadhi ya wanyama kwa siku tano bila kuzipeleka lkatika benki ," Alisema msemaji wa polisi katika mahojiano na Idhaa ya BBC Pidgin.

Jumatano afisa wa mapato ya hifadhi ya wanyama aliripoti kuwa naira milioni sita, laki nane na elfu ishirini zilizopatikana kupitia malipo ya kuwaona wanyama zingetumiwa katika tamasha Sallah na zimetunzwa vema.

Maelezo ya picha,

Februari 2018, mfanyakazi wa taasisi ya mitihani ya shule katika jimbo la Benue nchini Nigeria alisema kuwa nyoka aliingia ofisini na kumeza Naira milioni 36 za mitihani

Ingawa BBC Pidgin haikuweza kupata chanzo huru cha kuthibitisha madai hayo , wakazi wa eneo hilo ,kituo kimoja cha redio - Freedom Radio kilichopo jimboni Kano kiliripoti kuwa mmoja wa maafisa wa fedha wa hifadhi ya wanyama alisema kuwa " Mmoja wa sokwe wakubwa alitoroka na kuingia ndani ya ofisi na kumeza pesa hizo ."

Wakati BBC Pidgin ilipozungumza na Umar Kashekobo, Mkurugenzi Mkuu wa hifadhi hiyo ya wanyama, hakukubali wa kukataa taarifa hiyo iliyotolewa na kituo cha redio cha- Freedom Radio . Alisema kuwa swala hilo linafanyiwa uchunguzi na hapaswi kulizongumzia.

"Swala hili linafanyiwa uchunguzi kwa sasa na siwezi kusema lolote juu yake , waandishi wengi wa habari wanataka kukutana na mimi, lakini siwezi kusema lolote, msubiri ikiwa itathibitishwa kuwa pesa zimepotea." Alisema Kashekobo.

Mnamo mwezi wa Februari 2018, mfanyakazi wa taasisi ya mitihani ya shule katika jimbo la Benue nchini Nigeria alisema kuwa nyoka aliingia ofisini na kumeza kitita cha Naira milioni 36 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya ufanikishaji wa mitihani ya wanafunzi jimboni humo. taarifa hiyo iliibua hisia kali mitandaoni huku watu wakikejeli taarifa hiyo kupitia mtandao wa tweeter: Mmoja wa wao alisema kiasi cha pesa hizo ni kingi na hakiwezi kubebwa na nyoka.

Ulianzishwa hata ukurasa wa Tweeter kwa ajili ya nyoka. Ambayo ilidai, imechoka sana.

Shirika la kupambana na rushwa nchini Nigeria - pia lilituma ujumbe wake wa tweeter kuelezeahisia zake juu ya taarifa ya nyoka kuiba pesa:

Wiki chache zilizopita afisa huyo mwanamke wa mitihani na wenzake walikiri kuwa walipanga njama za kuiba pesa hizo.