Mbinu zatumiwa na mabalozi wa Marekani kuwaunga mkono wapenzi wa jinsia moja

Ubalizi wa Marekani mjini Jerusalem ulituma picha hii ya jengo lake la Tel Aviv siku ya Alhamisi kupitia ukurasa wa tweeter
Maelezo ya picha,

Ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem ulituma picha hii ya jengo lake la Tel Aviv siku ya Alhamisi kupitia ukurasa wa tweeter

Mabalozi wa Marekani wamekuwa wakitafuta njia za ubunifu wa kuonyesha uungaji mkono wao kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja LGBTQ pamoja na mwezi wa kujivunia walivyo-Pride month -baada ya Ikulu ya White House kupiga marufuku kupeperushwa kwa bendera ya yao ya rangi saba za upinde wa mvua.

Kabla ya mwaka huu balozi zote za Marekani zilikuwa zinapeperusha bendela ya wapenzi wa jinsia moja - lakini mwaka huu walitakiwa kuomba idhini kutoka kwa wizara ya mambo ya nje, ambayo iliripotiwa kukataa kutoa idhini hiyo.

Jumanne makamu wa rais Mike Pence alisema marufuku ilikuwa ni "uamuzi unaofaa".

Alisema hakuna masharti yaliyowekwa dhidi ya bendera za wapenzi wa jinsia moja kwenye majengo mengine.

Utawala wa Trump uliwateuwa mabalozi kadhaa wanaofahamika kuwa ni wapenzi wa jinsia moja na Trump alitoa taarifa akisherehekea mwezi wa kujivunia mapenzi ya jinsia moja

Ni nini kilicho nyuma ya msimamo wa White House?

"Tunajivunia kwa kuweza kumtumikia kila Mmarekani ," Bwana Pence aliambia kituo cha habari cha NBC, lakini "inapokuja katika swala la Bendera ya Marekani na balozi za Marekani , na miji mikuu kote duniani, ni bendera moja tu ya Marekani inayopeperushwa ."

Bwana Pence, ambaye ni muhubiri wa Kikristo , anapinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja na ana historia ya kuunga mkono kupingwa kwa sheria ya mapenzi ya jinsia moja.

Maelezo ya picha,

Bendera kubwa ya kujivunia maenzi y jinsia moja ikiwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Seoul iliondolewa Jumapili

Marufukuya kupeperushwa kwa bendera ya wapenziz wa jinsia moja imeungwa mkono na muhubiri maarufu anayemuunga mkono Trump-Franklin Graham, ambaye Jumapili alituma ujumbe wa Tweeter kwamba bendera ya wapenzi wa jinsia moja ni "Ni kosa kwa wakristo na mamilioni ya watu wa imani nyingine".

Mapema mwezi huu balozi ambaye jina lake halikutajwa aliliambia gazeti la Washington Post nchini Marekani kuwa kuna "aina ya mwamko " dhidi ya marufuku ya bendera ya wapenzi wa jinsia moja.

How have US missions shown support for Pride?

Siku ya Alhamisi ubalozi wa Marakani mjini Jerusalem ulituma ujumbe wa tweeter wa picha wa ofisi ya tawi lake mjini Tel Aviv - ambayo ilikuwa ni ofisi ya ubalozi kabla rais Trump auhamishie Jerusalem, ikiwa imepambwa kwa rangi za bendera ya wapenzi wa jinsia moja yenye rangi za upinde wa mvua ,

Ilikuwa ni moja ya matayarisho kwa ajili ya kushererekea gwaride la wapenzi wa jinsia moja kujivunia kuwa walivyo mjini Tel Aviv.

Ulikuwa ni moja ya walau balozi nne zilizopambwa kwa rangi hizo - balozi nyingine ni wa Ujerumani, Brazil na Latvia - ambazo zilinyimwa ruhusa ya kupeperusha bendera ya wapenzi wa jinsia moja, limeripoti gazeeti la the Guardian.

Licha ya hayo, Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Korea Kusini Seoul na ule wa mji wa India wa Chennai zilitundika bendera kubwa kwenye majengo ya ofisi zao.

Maelezo ya picha,

Balozi mdogo wa Marekani katika mji wa Chennai Robert Burgess akiwa mbele ya jengo la ofisi yake ya ubalozi ulio na bendera wapenzi jinsia moja

Bendera hiyo mjini Seoul ilishushwa chini Jumapili , vyombo vya habari vya huko viliripoti. Msemaji wa ubalozi alisema kuwa bendera iliondolewa kwa maafikiano na tamasha la Seoul Queer Culture Festival.

hata vivyo juhusi mbali mbali za balozi za Marekani za kuonyesha ushirikiano na wapenzi wa jinsia moja haukumfurahisha kila mtu.

Mchungaji wa kikristo wa Norway Jan-Aage Torp alituma ujumbe wa tweeter wa picha ya ubalozi wa Marekani mjini Oslo, akisema kuwa bendera ya wapenzi wa jinsia moja ulifanya nyota zisinyae.

"Hii ni sawa kweli ?"aliuliza.

baadhi ya balozi na mabalozi wa Marekani pia wameelezea uungaji mkono wao kwa wapenzi wa jinsia moja pamoja na mwezi wao wa kujivunia walivyo.

Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Mongolia Ulaanbaatar ulituma picha yake kupitia ujumbe wa Tweeter wa bendera ya wapenzi wa jinsia moja iliyoning'inia kwenye uzio wa ofisi ya ubalozi

Maelezo ya picha,

Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Mongolia Ulaanbaatar ukiwa na bendera ya wapenzi wa jinsia moja iliyoning'inia kwenye uzio wa ofisi ya ubalozi

Randy Berry, balozi wa Marekani nchini Nepal, alituma ujumbe wa akisema kuwa anasherehekea mwezi wa Kujivunia wapenzi wa jinsia moja na akatoa hakikisho juu ya " jukumu la Marekani la kulinda haki za binadamu kwa wote".