Shambulio la meli za mafuta Ghuba ya Oman: Je lengo la Iran ni nini haswa?

Mojwwapo ya meli zilizoshambuliwa katika Ghuba ya Oman

Saa chache tu baada ya mashambulizi dhidi ya meli mbili za kubeba mafuta katika Ghuba ya Oman siku ya Alhamisi , Jeshi la Marekani lilitoa kanda ya video iliosema kuwa ni ushahidi kwamba Iran ndio iliohusika na shambulio hilo.

Kanda hiyo ilidaiwa kuwaonyesha wanajeshi wa Iran wakitoa bomu moja la majini ambalo lilifeli kulipuka.

Kanda hiyo ya Video ambayo bado haijathibitishwa ilikuwa na ushawishi mkubwa ikilinganishwa na madai ya awali ya Marekani kwamba Iran ndio inayotekeleza mashambulizi hayo katika eneo hilo ambayo yalikuwa hayana ushahidi.

Lakini swali muhimu ni-nini lengo la Iran?

Katika kushambulia meli ya mafuta ya Japan na nyengine ya Norway iliokuwa ikibeba mafuta kutoka Saudia na UAE kupeleka Singapore na Taiwan?

Iran imepata shinikizo kubwa la kiuchumi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, tangu rais Donald Trump alipoiondoa Marekani katika makubaliano ya mpango wa Kinyuklia wa Iran ulioafikiwa 2015 na kuiwekea baadhi ya vikwazo vikali katika historia ya sera ya kigeni ya Marekani - ikilenga biashara ya mafuta ya taifa hilo , viwanda vya nishati, kampuni za meli , benki, bima na mengine mengi.

Vikwazo hivyo vinalenga kukata tamaa za mataifa mengine kutonunua mafuta kutoka Iran ambayo ndio yanayotegemewa sana na Iran kujipatia kipato.

Na vikwazo hivyo vimeanza kufanikiwa kwa kuwa biashara ya mafuta ya Iran imeshuka kwa zaidi ya thuluthi moja.

Sera ya Subra ya Iran

Kufikia sasa Iran imekuwa ikiendeleza sera ya kuwa na subra . Lakini iwapo ndio iliohusika na shambulio la sikju ya Alhamisi kile kinachoonekana huenda imechoka.

Iran ilibadilisha mwenendo wake mwezi uliopita baada ya Marekani kuendeleza tena vikwazo vyake dhidi ya taifa hilo ambapo hapo awali ilikuwa imeruhusu baadhi ya mataifa kununua mafuta kutoka kwa taifa hilo hatua iliosukuma msumari wa malengo ya utawala wa rais Trump ya kuhakikisha kuwa Iran haiuzi mafuta yake.

Jibu la Iran lilikuwa iwapo taifa hilo halitaruhusiwa kuuza mafuta yake basi hakuna taifa jingine lolote litakaloruhusiwa kuuza.

Asilimia 30 ya mafuta yote yanayosafirishwa kupitia baharini hupitia katika mkondo wa bahari wa Hormuz , likiwa ni eneo mhumi la usafirishaji wa mafuta katika Ghuba ambalo lipo kusini mwa pwani ya Iran.

Iran imetoa vitisho kuhusiana na mkondo huo hapo awali-lakini haikuvitekeleza vitisho hivyo.

Vikwazo vya EU

Mwaka 2012 , wakati Muungano wa Ulaya ulipoiwekea vikwazo vya kuuza mafuta Iran kutokana na mpango wake wa kinyuklia , Iran haikuufunga mkondo huo wa bahari.

Hatari ya mpango huo inawezekana na kwamba iwapo Iran itatekeleza kitendo hicho huenda ikazua vita kati ya Marekani na washirika wake katika eneo hilo.

Sio hatua ambayo inaweza kutekelezwa kwa haraka ama rahisi.

Ni uamuzi ambao ni sharti uafikiwe na viongozi wote wa taasisi tofauti za kisiasa huku walinzi wa Islamic Revolution Gurad IRGC wakihusika pakubwa hususana kutokana na uwezo wao wa kuwa na habari zote za kijeshi katika eneo la mashariki ya kati, pamoja na kiongozi wa dini Ayatollah Khamenei wakiwa na usemi wa mwisho kuhusiana na maswala yote ya usalama na yale ya kimataifa.

Je viongozi wa Iran wameamuaje?

Iwapo Iran ilihusika kweli katika utekelezaji wa mashambulio hayo , ni wazi kwamba viongozi wanaotoa uamuzi wa taifa hilo wanahisi kwamba hatua za kijeshi ni muhimu kuchukuliwa.

Iran inaweza kushuku kwamba hatari ya hatua waliochukua iko chini zaidi ya walivyodhania , kwa sababu rais Trump hataki vita.

Matamshi ya hivi karibuni ya rais Trump yanaonyesha kwamba licha ya ukatili wake , yuko tayari kwa mauzungumzo na Iran bila masharti yoyote.

Hatahivyo Iran itaangazia zaidi maono ya mshauri wa maswala ya usalama wa rais Trump, John Bolton ambaye amekuwa akitaka Marekani kuishambulia Iran.

Iwapo subira ya Iran ni wazi kwamba inapungua -basi taifa hilo litahisi kuonyesha uwezo wake wa kivita ikiwemo kuharibu biashara ya mafuta.

Je inaweza kupandisha hadhi yake na Marekani na kujiondoa katika jinamizi la vikwazo vya adui wake wa jadi?