Iran yatangaza itakiuka makubaliano ya nyuklia na kuongeza urutubishaji wa Uranium Juni 27

Iranian President Hassan Rouhani (3rd Left) is shown nuclear technology in Tehran, Iran (9 April 2019) Haki miliki ya picha EPA
Image caption Iran limesema limeongeza mara nne uzalishaji wa madini ya uranium

Iran imetangaza kwamba itakiuka kiwango cha urutibishaji wa madini ya Uranium Juni 27, kilichowekwa katika makubaliano ya nyuklia ya mnamo 2015 yalioidhinishwa na mataifa yenye nguvu duniani.

Shirika la nishati ya atomiki nchini Iran limesema limeongeza mara nne uzalishaji wa madini hayo yanayotumika kutengeneza nishati lakini pia silaha.

Lakini limeongeza kwamba bado "kuna muda" kwa mataifa ya Ulaya kuwajibika kwa kuilinda Iran dhidi ya vikwazo vilivyoidhinishwa upya vya Marekani.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeionya Iran dhidi ya hatua hiyo inayokwenda kinyume na makubaliano hayo.

Zimesema hazitokuwa na namna ila kuidhinishia upya vikwazo, ambavyo zilikubali awali kuviondoa iwapo Iran itatii masharti yaliowekwa katika mpango wake wa nyuklia.

Iran imelalamika kwamba mataifa hayo yameshindwa kutii uwajibikaji wao katika kutatua athari za vikwazo vya Marekani vilivyoidhinishwa baada ya rais Donald Trump kujito akatika mpango huo mwaka jana.

Trump anataka kuilazimisha Iran kujadili upya makubaliano hayo na ikubali kusitisha mpango wake wa nyuklia na isitishe shughuli zake katika enoe la mashariki ya kati.

Hatua hii ya sasa inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi mkubwa katika eneo, huku Marekani ikituma jeshi na kuishutumu Iran kwa kuhusika katika mashambulio yanayoshukiwa yaliosababisha magari mawili ya mafuta kuteketea moto siku ya Alhamisi.

Iran inakana tuhuma hizo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kinu cha Arak chenye madini ya plutonium yalio na uwezo wa kuunda mabomu.

Kwanini Iran imeongeza viwango vya urutubishaji?

Mapema mwezi Mei, Trump aliweka shinikizo zaidi kwa Iran kwa kuidhinisha upya marufuku kwa matiafa yanayonunua mafuta kutoka kwa Iran.

Hatua hiyo ilinuiwa kusitisha kipato kikuu kwa serikali ya Iran.

Rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kuwa nchi yake inarudi nyuma katika ahadi zake katika makubaliano hayo.

Hii ikiwa ni pamoja na kutotiii sheria kuhusu akiba yake ya urutubishaji mdogo wa madini ya Uranium kiwango kilichowekwa kikwa ni - 300kg na tani 130 - na kusitisha uuzaji wa akiba ya ziada katika mataifa ya nje.

  1. Kwa nini Iran ishambulie meli za mafuta Ghuba ya Oman?
  2. Iran: Marekani inatusingizia
  3. Iran yaongeza uzalishaji wa madini ya kutengeza silaha za nyuklia

Rouhani pia ameyapatia mataifa hayo ya Ulaya siku 60 kulinda mauzo ya mafuta ya Iran. Iwapo yatashindwa kufanya hivyo , Iran itakiuka masharti ya urutubishaji Uranium na kusitisha uundwaji upya wa kinu cha Arak, ambacho mafuta yake yaliotumika yana plutonium yalio na uwezo wa kuunda mabomu.

"Katika siku 10 zijazo' ... tutaongeza kiwango cha urutubishaji ," Behrouz Kamalvandi amesema.

"Hii inatokana na kifungo 26 na 36 ya makubaliano ya nyuklia na hili litasitishwa iwapo tu pande nyingine zitawajibika,"ameongeza akitaja vifungu vinavyoeleza namna Iran na washirika wengine watakavyojibu ukiukaji.

"Muda bado upo kwa mataifa ya Ulaya ... lakini mataifa hayo yameeleza sio moja kwamoja kushindwa kwao kuwajibika. Yasifikirie kwamba baada ya siku 60 kutakuwana siku nyingine 60 za ziada ."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii