Ebola:Kwanini ugonjwa hatari unarudi mara kwa mara?
Huwezi kusikiliza tena

Je inawezekana kuviangamiza virusi vya Ebola?

Mlipuko wa Ebola katika Jamahuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao mpaka sasa umesababisha takriban watu 1, 400 umesambaa katika nchi jirani ya Uganda. Nchini Kenya, tahadhari imetolewa wakati matokeo ya utafiti ya mgonjwa aliyeshukiwa kuwa na ugonjwa huo yakisubiriwa. Waziri wa afya nchini Sicily Kariuki leo amewaambia waandishi habari Nairobi "Dalili za mgonjwa haziambatani na ugonjwa wa Ebola". Ni mlipuko mbaya kuwahi kushuhudiwa tangu 2013 na 2016 huko Afrika magharibi ambapo watu 11,000 walifariki. Basi kwanini ugonjwa wa Ebola unarudi mara kwa mara Afrika? na Je inawezekana kuangamiza virusi vya Ebola?

Mada zinazohusiana