Kwanini wanawake wanakataa kufanyiwa upasuaji huu?

In West Africa, 4.1% of births involve a Caesarean section, below the 5% recommended rate by WHO (Credit: Getty Images) Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption 4.1% ya wanawake Afrika magharibi hujifungua kupitia upasuaji, chini ya 5% kiwango kilichopendekezwa na WHO

Wakati Alice Ogbara alipolifungukia kundi la akina mama kuhusu alichokipitia katika upasuaji wa kujifungua mtoto wake, haikuwa kama hadithi nyingine ya kawaida wanavyoelezana marafiki alikuwa anafanya jambo ambalo baadhi wangelifikiria ni la hatari.

Hiyo ni kutokana na kuwa alikuwa anazungumzia upasuaji ambao wanawake wengi wanaweza kukataa kufanyiwa, wacha hata kuuzungumzia, hata kama wanafahamau kwamba ni upasuaji unaoweza kuyaokoa maisha yao.

"Nilipotembea kuelekea katika chumba cha upasuaji niliona kila kifaa ambacho walikuwa watakitumia mwilini mwngu, na nililia," Ogbara aliwaambia wanawake wenzake.

Anasema alikuwa anaogopa ataharibiwa mwili na usiweze kurekebishika. Kisha akafunikwa shuka tumboni mwake.

"Nilichokisikia baada ya hapo ni mwanangu akilia," anakumbuka - na wanawake waliomzunguka wakampigia makofi ya hongera.

Huenda Ogbara hawezi kufunguka kiasi hichi nje ya kundi hilo la wanawake.

Wasiwasi kuhusu usalama wa upasuaji wa kujifungua, pamoja na masuala ya kidini na ya kijamii inamaanisha upasuaji wa C-sections unakabiliwa na unyanyapaa Nigeria.

Hii husababisha wanawake wengi kukataa kufanyiwa upasuaji - au kujificha wakati wanapokubali kufanyiwa upasuaji huo.

Ogbara alilazimika hata kuificha familia yake wakati alipokua anakwenda kufanyiwa upasuaji huo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mkutano huo wa wanawake uliandaliwa na shirika lisilo la serikali Nigeria liitwalo Mamalette. Linawasaidia wanawake waja wazito na linawajibika kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua huko Lagos.

Sehemu ya jitihada hiyo ni pamoja na kukabiliana na unyanyapaa dhidi ya njia za akina mama kujifungua ambazo zinazuia wanawake kufikia huduma zinazoweza kuwaokoa maisha.

Kote nchini Nigeria, wanawake 58,000 hufariki wakati wa kujifungua kila mwaka, na kuifanya nchi hiyo kuwa ya nne duniani katika zenye viwango vya juu vya akina mama wanaofariki wakati wa kujifungua.

Sehemu ya tatizo ni idadi ndogo ya upasuaji wa CS: 2% tu. Kiwango cha dunia ni 21%. wakati huo huo kuna daktari mmoja pekee anayewashughulikia watu 6000 nchini.

Huwezi kusikiliza tena
Mfuko wa uzazi unao nusuru maisha ya akina mama Nigeria

Utofuati wa mataifa duniani

Katika mtazamo wa kimataifa katika maeneo ambako upasuaji wa C-section unaongezeka sana, Takwimu za Nigeria zimesimama kivyake.

Kati ya 2000 na 2015, viwango vya upasuaji wa C-section viliongezeka karibumara dufu duniani.

Afrika magharibi, wastani wa 4.1% owa visa vya akina mama wanaojifungua huwa ni kupitia upasuaji wa C-section, na kiwango cha Nigeria ni nusu ya hiyo.

Kuzuia vifo vya akina mama wakati wa kujifungua kiwango cha upasuaji hakipaswi kushuka chini ya 5%, Shirika la afya duniani linasema. Hiyo ni kutokana na kwamba upasuaji huo ni muhimu kuzuia mtoto kukwama katika hali ambapo mwanamke ana fupa dogo la kiuno, au wakati mtoto akiwa amekaa vibaya tumboni au ni mkubwa sana kwa uzito kuweza kutoka katika njia ya uzazi.

Pasi kuwepo usaidizi, mtoto aliyekwama anaweza kukipasua kizazi na kusambabisha kifo cha mama anayejifunguaau kusababisha mpasuko unaoweza kuchangia kuvuja damu kwa wingi.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Nadhani ni kiashiria katika afya kilicho na utoafuti mkubwa ya matumizi ya kupita kiasi na matumizi ya chini kupita kiasi," anasema Carine Ronsmans, mtaalamu katika chuo cha London School of Hygiene and Tropical Medicine na mhariri wa ripoti za hivi karibuni zinazoeleza ongezeko la upasuaji wa C section duniani.

Kiwango kikubwa cha C-sections kinaweza kutia wasiwasi kwasababu upasuaji huo unaweza kuongeza hatari ya matatizo ya kwa mfano kupasuka kwa kondo la nyuma inayoweza kusababisha kuvuja damu kwa wingi.

Nchini Nigeria wanawake wengi wanaoishi katika maeneo ya mashambani huapat atabu kufikia huduma hiyo , ambapo 58% ya wanawake wanaojifungua hufanya hivyo kwa usaidizi wa wakunga wasio na ujuzi wa kisawasawa.

Imani kwamba mwanamke kujifungua kwa njia ya kawaida na pasi usaidizi wa mtu ni jambo linaloendekezwa na kusifiwa kwa heshima kubwa ya uzazi nchini humo.

Hospitali nyingi hukabiliwa na visa vya wanawake - walio na hofu ya kuziaibisha familia zao wanaishia kukataa kufanyiwa upasuaji.

Kwa kawaida mwanamke hana uwezo wa kudhibiti namna atakavyoishia kuzaa, utafiti mmoja Nigeria umedhihirisha kuwa 90% ya visa, wanawake huamini wanaume ndio wanaopaswa kutoa ridhaa ili waweze kufanyiwa upasuaji wa C-section - na kuwapa uamuzi huo wanaume.

Katika mataifa mengine kama Uingereza na Marekani, hali huenda sio mbaya sana. Lakini wanawake wanakabiliwa na unyanyapaa wanapoamua kufanyiwa upasuaji.

Haki miliki ya picha Getty Images

Suluhu zisizo rahisi

Lakini linapokuja suala la afya ya uzazi, kukabiliana na vikwazo vya kijamii na kitamaduni dhidi ya upasuaji wa C-sections haitoshi.

Utafiti wa hivi karibuni umefichua kwamba katika matiafa yaliopo kusini mwa jangwa la Sahara, upasuaji wa C-sections unaweza kusababisha vifo mara 50 zaidi ya inavyoshuhudiwa katika mataife yenye kipao kikubwa.

Hilo kwa ukubwalinatokana na wanawake kutoshughulikiwa ipasavo wanapovuja damu au matatizo yanayozuka wakati wa mama kupotezwa fahamu ili afanyiwe upasuaji anasema Salome Maswime, daktari wa wanawake na mhadhiri wa chuo kikuu cha Witwatersrand, aliyehusika katika utafiti huo.

Gharama ya huduma ya afya ni changamoto pia katika kupata huduma ya upasuaji Nigeria.

Baadhi ya mataifa yamejaribu kuliimarisha hili kwa kutangaza upasuaji huo wa bure.

Nchini mali na Benin kwa mfano kuondosha malipo hayo kumedhihirisha ongezeko la wanawake kujifungua hospitali na kuchangia matokeo mazuri ya afya kwa wanawake na watoto wachanga.

Mabadiliko kama hayo yanajitokeza: serikali ya jimbo la Lagos kwa mfano hivi karibuni imetangaza uzinduzi wa bima mpya ya afya itakayohakikisha upasuaji wa C Section ni wa bure.

Iwapo ni Nigeria, Uingereza,tatizo la msingi na suluhu ni sawa anasema Amy Gibb. "Mara nyingi haki ya mwanamke kufanya maamuzi yanayomhusu mwenyewe hupotea," anesema "Njia ya kulifikia hili ni kuwapatia wanawake nafasi ya kutoa maamuzi kuhusu huduma kwao."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii