Shambulio la kigaidi Garissa: Mahakama Kenya yawapata 3 na hatia
Mahakama nchini Kenya imemuachilia huru mtu mmoja aliyetuhumiwa kutekeleza shambulio la 2015 katika chuo kikuu cha Garissa lililosababisha vifo vya takfriban watu 150.
Washukiwa wengine watatu waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio hilo mbali na kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa Al-shabab ambalo lilihusika na shambulio hilo katika chuo hicho kilichopo kaskazini mashariki mwa Kenya.
Miongoni mwa waathiriwa wa mkasa huo uliosababisha majonzi makubwa nchini Kenya ni Anastacia Mikwa aliyepigwa risasi mara kadhaa na maisha yake hayajawahi tena kuwa ya kawaida.
Shambulio la chuo kikuu cha Garissa Kenya: Mtanzania mmoja ni miongoni mwa washukiwa watatu waliopatikana na hatia
Raia mmoja wa Tanzania ni miongoni mwa washukiwa watatu wa ugaidi nchini Kenya waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio la mwaka 2015 katika chuo kikuu cha Garissa lililosababisha mauaji ya takriban wanafunzi 148.