'Wazazi waliponiambia niolewe niliamua kuwa DJ'

Puja Seth akiwa nyuma ya mitambo yake

Wanawake ma DJ bado ni wachache katika ulimwengu wa muziki>mpiga picha wa BBC Photographer Sayan Hazra alifuatilia maisha ya DJ Puja Seth kazini, mmoja wa wanawake wachache wanaopiga disko kusini mwa Bangalore.

"Ninapenda kuwaona watu wakiupenda muziki wangu. Kwangu mimi, ni aina fulani ya uhuru, - hunifanya nijieleze kwa dunia,"anasema Bi Seth mwenye umri wa miaka 31.

Alianza UDJ- mwaka 2014 Bangalore, mji ambao kwa kawaida unafahamika kama ''mji wa kumbi za muziki na baa'' kwa kuwa na utamaduni wa kumbi za muziki na vilabu vya pombe . Kwa miaka mingi , baa na kumbi za muziki zenye vilabu vya pombe, na vilabu vya pombe vimepanuliwa hadi nje ya kati kati mwa jiji ,na kufika hadi maeneo ya zamani, hata maeneo ya makazi ya watu.

Puja Seth

"Nilipoanza kucheza miziki yangu kwenye vilabu ,, nilikutana na maDJ wanawake ambao walikuwa wakitembelea Bangalore kutoka miji mingine duniani - lakini nilivyoelewa mimi hakuna hata DJ mmoja mwanamke aliyekuwa anafanya kazi hii Bangalore."

Aliongeza kuwa, baada ya kupiga miziki mara chache alifahamika kama ''DJ mzawa mwanamke''

Puja Seth

Lakini safari yake haikuwa rahisi. Akiwa ni mzaliwa wa kijiji cha mashariki mwa India kutoka kwa wazazi walioshikilia itikadi zao , Bi Seth anasema wakati wote amekuwa akitaka kufanya kazi ya kama DJ.

"Wazazi wangu wamemuwa kila mara niolewe-lakini sikutaka kufanya hilo."

Mkusanyiko wa picha za utotoni za Puja

Mara alipomaliza shule ya sekondari, alimua kutoroka kwao na "kufuata ndoto yake".

"Katika jamii yangu, wanawake hawaruhusiwi kufanya kazi - na wengi wao hawatoki nyumbani kwao peke yao hadi watakapoolewa. Kwa hiyo nilifahamu fika nilazima niondoke."

Puja Seth akisafisa nyumba yake

Utafutaji wake wa kazi ulimpeleka hadi Bangalore ambako alianza kufanya kazi kama muhudumu wa ndege.

Hapo ndipo alipokwenda kwenye sherehe kwa mara ya kwanza.

"Kitu cha kwanza nilichokigundua alikuwa ni DJ na ninakumbuka nilivutiwa sana ,"alisema.

Baada ya hilo, alijua ni nini anachotaka kukifanya.

Puja Seth

"Nilijenga urafiki na baadhi ya maD mjini ambao walinifundisha ujuzi wa kimsingi wa DJ. mengine nilijifunza kwa kutazama video za YouTube ."

Bi Seth amekwisha piga miziki yake katika matukio zaidi ya 450 kote nchini India kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

"Nilikuwa sijawahi kuwaona wanawake wakinywa pombe na kuvuta sigara katika kijiji changu - na sasa ninaupigia muziki umati wa watu ambao wanafanya yote hayo karibu yangu na sifungi macho."

Licha ya kupendeza , anasema, kuwa DJ-kama mwanamke ina hatari zake: "Watu husema mara kwa mara kuwa taaluma hii si ya wanawake."

Puja Seth akiwa nyuma ya mitambo yake

"Katika vilabu vya pombe watu wanalewa, na nadhani wanaweza kunifuata kila mara. Mara nyingi, huwa wananiomba namba yangu ya simu. Na wakati mwingine, ni vigumu kuwapuuza na kufanya kazi yangu - lakini huwa ninapata usaidizi kutoka kwa walinzi(mabaunsa)."

Lakini hajakubali hayo yamzuwie kufanya kazi yake.

"Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi yangu ni kuifanya hadhira i densi , kuwaona wakiuhisi muziki kama mimi. Watu huja katika muziki wangu kwa ajili ya kupata hisia hiyo ."

Picha zote na Sayan Hazra

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii