Ugaidi: Tishio la kushambuliwa ni kubwa kiasi gani Afrika Mashariki?

kenyans selling obama posters ahead of his visit Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakenya walivyojiandaa kumpokea Obama wakati wa ziara yake ya kwanza akiwa rais wa Markani wakati huo

Ikulu ya Marekani ilipotangaza mwezi Machi mwaka 2015 kuwa Barack Obama atazuru Kenya kwa mara ya akiwa Rais wa Marekani maafisa wa usalama wa nchi hiyo walijianda ya kwa miezi mitatu kabla ya ziara hiyo.

Maafisa hao walifurika hoteli ambayo Obama alitarajiwa kukaa akiwa katika ziara hiyo halia ambayo ilivutia hisia mseto kuhusu hali ya usalama nchini Kenya na Kanda nzima ya Afrika Mashari.

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi wakati huo NEvans Kidero alisema ziara hiyo ilidhihirisha wazi kuwa Kenya ni salama.

Kwa upande mwingine wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilikuwa imetoa tahadhari ya shambulio la kigaidi katika kongamano la kimataifa la Biashara ambalo Obama alitarajiwa kuhutubia

Ziara hiyo pia ilifanyika siku kadhaa baada ya Duka kubwa la Westgate lililokuwa limeshambuliwa na magaidi jijini Nairobi kufunguliwa tena.

Watu 67 waliuawa katika shambulio hilo ambalo wanamgambo wa kundi la al-Shabab walidai kulitekeleza.

Kufunguliwa tena kwa Westgate kulipongezwa na wengi kama hatua ya ushindi kwa Wakenya.

Kwa wengine hatua hiyo iliwakumbusha hatari ya ugaidi ambayo ilitokana na mashambulizi ya al-Shabab - mojawapo lile shambulio la chuo Kikuu cha Garissa ambapo watu 147 waliuawa.

Kubadilisha mbinu ya mashambulizi

Kundi la Al-Shabab linaendelea kuwa tishio kwa usalama wa kanda hii kutokana na jinsi limekuwa likibadilisha mbinu ya mashambulizi katika taifa jirani la Somalia ambalo ndio chimbuko lao.

Kundi hilo liliimarisha mashambulizi yake kufuatia hatua ya Muungano wa Afrika, kupeleka kikosi chake cha kulinda amani AMISOM, nchini Somalia kwa ushirikiano na Marekani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption watu 147 waliuawa katika shambulio la al-Shabab dhidi ya Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya

Kundi hilo lilifurushwa kutoka mji mkuu wa Mogadishu, mwezi Agosti 2011 kufuatia uvamizi uliotekelezwa na wanajeshi 22,000 wa Muungano wa Afrika na kuondoka katika bandari muhimu ya Kismayu mwezi Septemba 2012.

Wakati lilipoondolewa katika bandari ya Kismayu kundi hilo lilipoteza fedha nyingi kwa kuwa lilikuwa likijipatia fedha hizo kupitia uuzaji wa makaaa.

Marekani pia imetekeleza msururu kadhaa wa mashambulio, hatua iliosababisha kuuwawa kwa kiongozi wa kundi hilo Aden Hashi Ayro, mwaka 2008 na mtangulizi wake , Ahmed Abdi Godane.

Mwezi Machi 2017, rais wa Marekani Donald Trump aliidhinisha mipango ya Pentagon kuendeleza operesheni zake dhidi ya al-Shabab.Wanamgambo hao wakiwemo viongozi wao waliuawa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani katika eneo la Gedo kusini mwa Somalia.

Huwezi kusikiliza tena
Shambulio la kigaidi Garissa: Mahakama Kenya yawapata 3 na hatia

Kundi hilo lilipotimuliwa katika baadhi ya maeneo yalioaminiwa kuwa ngome yao kuu nchini Somalia liliamua kupanua oparesheni yao Kenya na mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Hatua hiyo ilikuwa ana athira katika mpango wa kukabiliana na ugaidi.

Kwa muda mrefu kundi hilo liliapa kulipiza kisasi oparesheni ya majeshi ya Kenya nchini Somalia- na kutoka mwaka 2011 limekua likipambana kufikia lengo hilo.

Mwaka 2013, wapiganaji wake walivamia duka la jumla la West Gate jijini Nairobi na kusababisha vifo vya takriban watu 67.

Wakati wa mechi ya kombe la dunia kati ya Uhispania na Uholanzi, lilishambulia kilabu moja ya mpira wa raga pamoja na mkahawa katika mji mkuu wa Uganda ,Kampala na kuwaua watu 74 waliokuwa wakitizama mechi hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Duka la Westgate jijini Nairobi lilishambuliwa na al-Shabab mwaka 2013

Kundi la Al-Shabab linahubiri Uislamu wa madhahabu ya Wahhabi kutoka Saudia huku raia wengi wa Somali wakiwa wa madhahabu ya Sufi.

Limeweka sheria kali za Kiislamu katika maeneo linayodhibiti, ikiwemo kumpiga mawe hadi kufa mwanamke anayetuhumiwa kuzini mbali na kuwakata mikono wezi.

Kumekuwa na ripoti kadhaa za wapiganaji wa Jihad wa kigeni wanaoelekea Somalia kusaidia al-Shabab, kutoka mataifa jirani pamoja na Marekani na Ulaya.

Kundi hilo linadaiwa kuwasajili wapiganaji wa kigeni kutoka Syria, lakini juhudi za Kimataifa za kukabiliana na ugaidi zimesaidia kudhibiti shughuli zao.

Havi karibuni al-Shabab limeanza kutumia lugha ya Kiswahili kuendesha propaganda katika mataifa ya Afrika Mashariki ambayo baadhi yanakabiliwachangamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kundi la Al-Shabab limekuwa likiwashawishi vijana kujiunga nalo

Ongezeko la itikadi kali

Nchini Kenya uwepo wa al-Shabab umechangiwa zaidi na ongezeko la vijana wa Kiislam wanaojiunga na kundi hilo katika ukanda wa Pwani.

Kuna hofu kuwa kundi hilo huenda likajipenyeza katika taifa jirani laTanzania .

Kuibuka kwa na makundi ya kihalifu- na ongezeko la ukosefu wa usalama - kunaliwezesha kundi hilo kujiunga na makundi hayo kutekeleza ajenda yake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii