Tahadhari ya shambulizi la kigaidi Tanzania ina maana gani?
Huwezi kusikiliza tena

Tahadhari ya tishio la ugadi lina maana gani kwa Tanzania?

Mkuu wa polisi Nchini Tanzania Simon Sirro amenukuliwa akisema kua jeshi lake lilipata fununu za shambulizi hilo hata kabla ya ubalozi wa Marekani nchini humo kutoa tahadhari

Katika tangazo lake Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari kuwa kuna fununu za mipango ya mashambulizi jijini Dar es Salaam.

Hii ina maana gani hasa kwa Tanzania na usalama wake?

Mwandishi wa BBC Scolar Kisanga amezungumza na mchambuzi wa masuala ya Kiusalama Kutoka Nchini Kenya George Musamali.

Mada zinazohusiana