Roboti zinadaiwa kuchukua nafasi kubwa ya kazi za watu

Raia wa Saudi Arabia roboti Sophia akiwa kwenye maonyesho mjini Toronto ,Canada Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Roboti Sophia amepewa uraia na Saudi Arabia

Mitambo inayojiendesha imeshika kasi katika miji ya uzalishaji.Kwenye miji hiyo, idadi ya watu wanaofunga ndoa inapungua, uhalifu unaongoza, idadi ya vifo inaongezeka kutokana na vitendo vya kujiua, na matumizi ya vilevi na madawa anaeleza Dokta Carl Frey.

Mtafiti kutoka chuo cha Oxford ameelezea mazingira ya viwanda nchini Marekani, kwa jina la Rust Belt-miji kama Flint, Detroit na Cleveland ndio iliyoongoza kwa uzalishaji.

Dokta Frey anasema wafanyakazi kwenye miji hii wanapoteza kazi zao kwa roboti.Je nini kitatokea ikiwa mashine zitafanya kazi badala yetu?

Kodi

Kama wafanyakazi wako nje ya kazi, hawatalipa kodi na katika nchi nyingi za Magharibi wataweza kudai mafao yao ya kutokuwa na kazi.Hii ingekua hasara mara mbili kwa nchi.

Nchini Marekani, kwa mfano, asilimia 48 ya mapato ya nchi inatoka kwenye mapato ya mmoja mmoja na asilia 35 kutoka kwa bima za jamii-asilimia 9 pekee kutoka kwenye kodi za makampuni.

Kufidia upotevu wa mapato kutoka kwenye kodi ya mapato, wengi wametaka roboti ilipe kodi.

Teknolojia

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekua msaada lakini pia yamekua yakivuruga.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mabadiliko katika viwanda yalitusaidia kuondoka kwenye matumizi ya nguvu za mwanadamu, mapinduzi ya pili yalileta uzalishaji mkubwa kwa njia umeme.

Nyakati za matumizi ya Kompyuta yalileta ufanisi mkubwa na usambazaji wa taarifa.

Mapinduzi ya nne ya viwanda-yaliyokwenda sambamba na intelijensia ya bandia (AI) na robots inategemewa kubadili kwa kiasi kikubwa mifumo ya uzalishaji,usimamizi na utawala.

Wigo,kasi na kina cha mabadiliko haya havina mfano wa kihistoria.

Kukosolewa

Mwaka 2013, Daktari Frey alitoa tathimini yake akisema kuwa takribani asilimia 50 ya ajira nchini Marekani zinaweza kuwa hatarini katika kipindi cha miaka thelathini kutokana na maendeleo ya AI na roboti.

Ajira zitakazopotea ni pamoja na za viwandani, waendesha malori na makarani wa mahakama.

''Hatujaona pingamizi dhidi ya matumizi ya mitambo inayojiendesha yenyewe,kama ile tuliyoona dhidi ya utandawazi.Waendesha malori kupatikana China lakini yanaweza kujiendesha yenyewe,'' Carl Frey alikiambia kipindi cha Business Daily.

Je, kutoza kodi roboti kunaweza kuondoa pingamizi?

Kodi

Miaka miwili iliyopita bilionea na mwanzilishi wa Microsoft, Bill Gates alikuja na wazo la kodi ya roboti katika mahojiano na jarida la Quartz

Haki miliki ya picha Getty Images

''Hakika kutakuwa na kodi zinazohusu vyombo vinavyojiendesha vyenyewe.Sasahivi,mfanyakazi binaadamu anayefanya kazi ya kustahili dola 50,000 kwenye kiwanda, fedha hiyo hukatwa kodi na kupata kodi ya mapato,makato ya mifuko ya Jamii, hivyo vyote.Ikiwa roboti anakuja kufanya kitu hichohicho, utafikiria kumkata kodi kwa kiwango kilekile,'' alisema Gates.

Bilionea Elon Musk pia amezungumza akiunga mkono roboti kukatwa kodi.

Hoja ni rahisi:roboti wakatwe kodi na fedha zitumike kusaidia katika masuala ya afya na elimu,au hata kusaidia kutoa kipato cha kila mtu.

Biashara lengwa

Lakini unawezaje kukata kodi roboti?

Haki miliki ya picha Getty Images

''Haina haja ya kwenda kutafuta roboti.unaweza kuwa na kodi kwa vif vinavyojiendesha vyenyewe.Biashara zinazotoa ajira kwa kiasi kidogo zinapaswa kulengwa.Wakati huohuo serikali zipunguze kodi kwa wafanyakazi,''anaeleza Ryan Abbott,Profesa wa sheria na huduma za afya katika Chuo kikuu cha Survey nchini Uingereza.

Kama ilivyo kwa wengine,haongelei kutoza kodi kwa roboti kama za binaadamu isipokuwa kwa ujumla matumizi ya intelijensia bandia.

Wataalamu wa masuala ya kodi wanasema mapato zaidi yanaweza kusaidia programu za kuendeleza ujuzi na kupunguza uwezekano wa kutokea kwa hali ya kutoelewana ndani ya Jamii ambako kunakuwa kumesababishwa na ukosefu wa ajira.

Sera

Hii ndio namna ambayo Korea Kusini inafanya.Mwaka 2017,ikawa nchi ya kwanza kuanzisha kuondolewa kwa kodi kwenye mitambo inayojiendesha yenyewe kusaidia kupunguza kasi wakati ambapo teknolojia ndio imeshika kasi kwenye soko la ajira

Haki miliki ya picha Getty Images

Ndani ya Umoja wa Ulaya, mapendekezo ya kuanzisha kodi ya roboti hivi karibuni ilipingwa kwenye Bunge la Umoja wa Ulaya,ambalo badala yak likachagua kuwepo na sheria kudhibiti ongezeko la roboti.

Na nchini Marekani suala hili limepata kutolewa kisiasa.

Mgombea wa urais wa chama cha Democratic Andrew Yang anataka mitambo inayojiendesha yenyewe itozwe kodi.

''Takribani asilimia tatu ya watu wanafanya kazi kwenye sekta ya usafirishaji. Wigo wa mitambo hii unaweza kusababisha mvutano.

Kufunzwa tena na kutoa faida ni jambo muhimu.Ikiwa Serikali Hawana mapato yatokanayo na kodi kufanya hivyo, hali itakuwa mbaya zaidi anasema Ryan.

Wazo baya

Lakini si kila mtu anakubali

Haki miliki ya picha Getty Images

''kutoza kodi roboti si suluhisho kwa sababu makampuni makubwa wataondosha makampuni kukwepa sheria hizi.Makampuni madogo, ya ndani yatapata taabu,'' anaeleza Dokta Janet Bastiman,ofisa mkuu wa idara ya sayansi katika kampuni ya teknolojia ya habari,Story Stream.

Binaadamu wanahamia kwenye kazi nyingine na si lazima kubaki kwenye viwanda.

Faida ya viwanda inaongezeka hivyo vinaeza kukatwa kodi,'' anaeleza.

Kuzitoza kodi roboti na mifumo inayofanya kazi na intelijensia bandia, anasema , ''itafanya watu waache kuwa wagunduzi wa mambo mapya''.

Ulrich Spiesshofer, aliyekuwa mmiliki wa Swiss engineering major ABB, havutiwi na hoja ya roboti kukatwa kodi.

Wakati akijibu hoja ya Bill Gates, alisema,'' ukitazama uchumi na kiwango kidogo cha watu wasio na ajira duniani wakilinganisha na roboti:

Ujerumani, Japan ,Korea Kusini ina kiwango kikubwa cha roboti kukiwa na roboti 300 kwa kila wafanyakazi 10,000 na zina idadi ndogo ya watu wasio na ajira .

Kupoteza kazi

Haki miliki ya picha Getty Images

Ingawa Carl Frey anasema anasimamia kwenye utabiri wake wa mwaka 2013, utabiri uliofanywa na kampuni ya Pwc mwaka jana ilibaini kuwa nchini Uingereza,ajira zilizopotea kwa sababu ya machine zinazojiongoza zenyewe wataweza kufidiwa kwa uanzishaji wa ajira mpya.

Mfano wake unaweza kutazamwa kwenye ulimwengu wa michezo.

Matumizi ya teknolojia yamesaidia kuimarisha ubora wa ufanyaji wa maamuzi kwa kuondosha makosa ya binaadamu.

Hali hii imesaidia kutengeneza ajira kwa mafundi.Lakini upotezaji wa ajira kwenye kiwanda ni hadithi tofauti.

Bado hakuna makubaliano katika kutoza kodi roboti, lakini wanasiasa wanazidi kuzingatia hilo kama namna ya kukabiliana na mabadiliko yaliyoletwa na maendeleo ya teknolojia.