Tamasha za muziki wa Koffi Olomide zafutwa A.Kusini

Olomide, mwenye umri wa miaka 62, ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba, alipatikana na hatia ya kumbaka mnenguaji wake mwenye umri wa miaka 15 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Olomide, mwenye umri wa miaka 62, ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba, alipatikana na hatia ya kumbaka mnenguaji wake mwenye umri wa miaka 15

Kumbi mbili zimefuta tamasha za mwanamuziki wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Koffi Olomide, ambaye hivi karibuni alipatikana na hatia ya kumbaka mmoja wa wasichana wanenguaji waliokuwa katika bendi yake wakati alipokuwa na umri wa miaka 15.

Olomide, mwenye umri wa miaka 62, ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba, alitazamiwa kucheza muziki wake katika ukumbi wa Gallagher Convention Centre uliopo nje ya mji wa Johannesburg Juni 28 na katika Shimmy Beach Club mjini Cape Town siku mbili baadaye.

Lakini upinzani dhidi yake ulianza kupitia kampeni iliyoendeshwa kwenye mitandao ya habari ya kijamii kusitisha matamasha zake kutokana na kupatikana kwake na hatia ya ubakaji.

"Tafadhari mnafahamishwa onyesho la Koffi Olomide ...halitafanyika ," alieleza mkurugenzi mkuu wa Convention Centre, Charles Wilson katika taarifa aliyoitoa Jumatano.

Shimmy Beach "ilifanya uamuzi wiki iliyopita wa kutokuwa mwenyeji wa tamasha la Koffi Olomide lililokuwa linaendeshwa na promota wa nje, kilisema kilabu kwenye ujumbe wake kupitia Twitter siku ya Jumanne.

Taarifa ya kusitishwa kwa tamasha hilo iliafikiwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Tweeter waliokuwa wameanzisha kampeni ya kumzuwia kofi Olomide kufanya matamasha nchini Afrika Kusini chini ya #StopKoffiOlomide:

Mwezi Machi, mahakama ya Ufaransa ilimhukumu Bwana Olomide kifungo cha miaka miwili jela kilichoahirishwa baada ya kesi dhidi yake ambayo hakuidhuria.

Mahakama ya Nanterre, nje ya mji mkuu Paris, pia ilimuagiza alipe faini ya kiwango sawa kwa kuwasaidia wanawake watatu wengine kuingia nchini Ufaransa kwa njia haramu.

Wakili wa Olomidé alipongeza uamuzi huo na kuutaja kuwa ushindi, akiwaarifu waandishi habari kwamba uamuzi huo utachangia kuondolewa waranti ya kimataifa wa kumkamata.

Haki miliki ya picha KTN
Image caption Mwaka 2016 Koffi Olomide alimpga teke mmoja wa wanenguaji wake mjini Nairobi Kenya

Katika kesi hiyo wanenguaji wanne waliokuwa wakimfanyia kazi waliiambia mahakama kwamba aliwanyanyasa kingono mara kadhaa kati ya mwaka 2002 na mwaka 2006. Waliieleza mahakama kuwa unyanyasaji huo ulifanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Ufaransa.

Olomidé alikimbilia Congo mnamo 2009 akiahidi kujitetea lakini alikosa kufika mahakamani Ufaransa katika kesi hiyo ambayo kutokana na ombi la walalamishi ilifanyika faraghani.

Lakini ilimuondolea mashtaka ya kupiga na utekaji nyara wa wanawake katika nyumba yake karibu na jiji la Paris kati ya mwaka 2002 na 2006.

Olomide alifungwa kwa muda mfupi DR Congo mnamo mwaka 2016 baada ya kumpiga teke mmoja wa wanenguaji wake, na akahukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela mwaka 2012 kwa kumpiga mzalishaji (producer)wa muziki wake.

Mwanamuziki huyo maarufu wa miziki ya Rhumba alisafirishwa kwenda mjini kinshasa kutoka Nairobi baada ya kukamatwa na polisi ya Kenya.

Olomide alisafirishwa na shirika la ndege la Kenya Airways, kutoka uwanja wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa tano unusu asubuhi.

Mwanamuziki huyo alikuwa amekabiliwa na shutuma baada ya kanda ya video kusambaa mtandaoni ikionekana kumuonyesha akimshambulia mwanamke uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Ijumaa asubuhi, muda mfupi baada ya kuwasili.

Pia anasakwa na polisi nchini Zambia kwa kumpiga mwandishi mpigapicha wa Rwanda mjini Lusaka mnamo mwaka 2012.

Tuhuma na mashtaka aliyokabiliana nayo Koffi Olomide:

  • 2018 Zambia iliagiza akamatwe baada ya kutuhumiwa kumshambulia mpiga picha
  • 2016 alikamatwa na kutimuliwa baada ya kumshambulia mojawapo ya wanenguaji wake Kenya
  • 2012 alishtakiwa DR Congo kwa kumshambulia(mzalishaji wa muziki wake) produza wake na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu ambacho angefungwa iwapo angetekeleza uhalifu mwingine
  • 2008 alishutumiwa kumpiga teke mpiga picha katika kituo cha Televisheni DR Congo RTGA na kuivunja kamera yake katika tamasha , lakini walipatanishwa baadaye.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Koffi Olomide atoa wimbo mpya kuwaomba msamaha akina mama Afrika

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii