Uharamia Afrika Magharibi: Je ndio bahari hatari zaidi duniani?

An anti-piracy team watches over a cargo ship off the coast of West Africa. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meli zinazobeba mafuta na gesi ni kivutio cha utajiri kwa maharamia

Bahari kutoka pwani yenye utajiri wa mafuta Afrika magharibi sasa ndio hatari zaidi duniani kwa ubaharia, kwa mujibu wa ripoti mpya.

One Earth Future, ambayo hutoa taarifa ya kila mwaka kuhusu uharamia baharini, inasema kwamba licha ya kupungua kwa mashambulio kwa kiasi kikubwa katika baadhi ya maeneo duniani, visa hivyo vimekuwa vikiongezeka Afrika magharibi na sasa vimekithiri kuliko sehemu nyingine yoyote duniani.

Lakini kwanini kuna ongezeko hilo na ni nani anayelengwa?

Uharamia ni nini?

Ufafanuzi wa uharamia baharini unajumuisha meli zinazoshambuliwa katika bahari kuu - hiyo ikiwa ni zaidi ya maili 12 kutoka pwani na sio chini ya himaya ya taifa lolote.

Kaika maji ya mataifa na katika maenoe ya bandari , mashambulio hayo hutajwa kama wizi wa mabavu baharini.

Hatahivyo, data tulizotumia kutoka ripoti hii mpya zinajumuisha seti mbili za picha kamili ya visa vya katika maji ya ndani na ya nje baharini.

Mnamo 2018, kumekuwa na visa 112 kam ahivyo katika bahari ya Afrika magharibi.

Na sio meli kubwa pekee zinazosafirisha mafuta na gesi kutoka Nigeria na Ghana zinazolengwa.

Huwezi kusikiliza tena
Sababu ya visa vya uharamia kuanza kuongezeka Somalia

Meli za biashara kutoka matifa madogo pia zinalengwa na maharamia.

Katika tamasha la hivi karibuni mjini London, Rais Faure Gnassingbé wa Togo - taifa lililo katikati ya maaifa mawili makubwa kieneo - aliangazia wasiwasi wake kuhusu ongezeko la mashambulio katika ubaharia wa kieneo.

"Eneo letu linatofautishwa kwa kuzuka upya kwa uhalifu wa biana ya mataifa katika bahari kuu katika ghuba ya Guinea," ameeleza bwana Gnassingbé.

Kwanini mashambulio yanaongezeka?

Baadhi ya mashambulio yamekuwa dhidi ya meli zinazosafirisha mafuta na gesi, kama vile matanka, meli za kubeba mizigo na matagi. Vyombo vya uvuvi pia vimelengwa.

Pwani kutoka Nigeria imeshuhudia mashambulio zaidi mnamo 2018. Sehemu ya sababu ya hii ni uharamia unaolenga matanka yanayotoka katika visima tajiri vya mafuta na gesi Nigeria.

Kulishuhudiwa pia visa wakati wa upakiaji na kutia nang'a katika bandari ya Lagos.

Uharamia wa utekaji nyara na kuitisha vikombozi ulikuwa wa kawaida kutoka pwani za Benin, Ghana, Nigeria, Congo-Brazzaville na Cameroon.

Ghasia za kisiasa, ukosefu wa utekelezaji sheria na umaskini vyote ni mambo yanayochangia kuongezeka kwa uharamia.

Mabaharia wengi hawatoki katika enoe hilo. Karibu nusu wanatoka Ufilipino, ikifuatwa na India, Ukraine na Nigeria.

Mojawapo ya kwanini sasa Afrika magharibi inaongoza katika uharamia ni kutokana na kwamba kunakiliwa kupungua kwa visa hivyo kwengineko duniani.

Njia za ubaharia Afrika mashariki katika pwani ya Somalia zimekuwa zikishuhudia mashambulio, na wizi huo.

Lakini tangu kiwango cha juu zaidi kushhudiwa mnamo 2011, viwango vya uharamia katika enoe hilo vimepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.

Hii kwa ukubwa inatokana na matokeo ya jitihada ya pamoja ya matiafa kupiga doria katika bahari na kuchukua hatua kali dhidi ya visa vya uharamia.

Jitihada za ndani ya nchi Somalia kubadili mitazamo katika kuruhusu uharamia na kujenga uwezo kisheria kuweza kuwashtaki wahalifu pia zimesaidia kuiimarisha hali.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Upembe wa Afrika ulikuwa na tatizo kubwa la uharamia , lakini kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa

Huko Asia, katika bahari ilio na shughuli nyingi za kibiashara Malacca Strait, kati ya Malaysia na Indonesia, kumeshuhudiwa mashambulio mengi mnamo 2015.

Hatua za pamoja ya vikosi vya baharini zimepunguza tatizo hilo huko lakini uharamia unasalia.

Mashambulio dhidi ya meli za katika visiwa vya Caribbean na ktoka pwani ya Amerika kusini hatahivyo yameongezeka.

Venezuela zaidi, imelengwa sana kwa uharamia.

"Matatizo ya kisiasa na kiuchumi ni chanzo kikuu huko," anasema Lydelle Joubert, mtaalamu kuhsu masuala ya uharamia katika shirika la One Earth Future.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii