Macron amtuza Elton John tuzo ya heshima ya juu kwa kuwa sauti ya wapenzi wa jinsia moja

Mwanamuziki Elton John(kushoto) akipewa tuzo na Emmanuel Macron katika kasri ya rais Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamuziki Elton John(kushoto) akipewa tuzo na Emmanuel Macron katika kasri ya rais

Sir Elton John amezawadiwa tuzo ya juu kabisa ya raia mwema zaidi nchini Ufaransa , inayofahamika kama Legion d'Honneur.

Mwanamuziki huyo maarufu wa Uingereza alikabidhiwa tuzo hiyo na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika sherehe iliyofanyika katika kasri ya rais ya Élysée .

Ofisi ya rais Macron ilimsifu sana Sir Elton, mwenye umri wa miaka 72, na kumtaja kama "muimbaji mwenye akili" na mmoja wa wasanii wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kuwapatia sautu wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia zao - LGBT.

Alitumia hotuma yake ya shukrani ya tuzo hiyo kunadi kazi yake ya msaada

Shirika la mwanamuziki huyo la msaada ambalo linawasaidia walioambikia virusi vya Ukimwi -The Elton John Aids Foundation, limeweza kuchangisha pauni zaidi ya milioni 310 zinazotumika katika kuzuwiana maambukizi ya HIV na kutoa elimu na usaidizi kwa watu walioathiriwa na virusi vya HIV

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Elton John na Emmanuel Macron

Wakati wa hotuba yake alielezea namna vita dhidi ya ukimwi vilivyo muhimu kwake : "Kama ilivyo kwa Muziki , vita dhidi ya Ukimwi vimekuwa ni jambo ninalolipenda kwa miaka mingi.

"Na kama ilivyo kwa muziki, vita hivi vinanikumbusha mimi kila siku juu ya nguvu za kiroho alizonazo mwanadamu.

"Na mambo hayo yanayotuunganisha yana nguvu zaidi ya yanayotutenganisha . Ni katika roho hii ya ubinadamu itakayoniwezesha kuwa miongoni mwa wajumbe wa Legion d'Honneur."

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sir Elton na rais Macron walikumbatiana wakati wa sherehe

Aliongeza kuwa: "Nina mapenzi makubwa na Ufaransa: Nina nyumba hapa, Nimekuwa wakati wote nikipenda kuja hapa , Ninapenda utamaduni wa uhuru wa Wafaransa , jinsi wanavyoishina watu wa Ufaransa ."

Sir Elton John amepewa tuzo hilo la heshima mwezi mmoja kabla ya kutoa filamu ya maisha yake inayofahamika kama Rocketman biopic.

Sir Elton alikiuwa nchini Ufaransa kama sehemu ya maonyesho yake ya mwisho.

mwaka jana mwanamuziki huyo maarufu ambaye ni mpenzi wa jinsia moja alitangaza kuwa anaacha kufanya matamasha ya muziki katika maeneo mbali mbali ili awe na muda wa kutosha wa kuwa na familia yake.

Alisema kuwa atasema kwaheri kwa mashabiki wake kwa safari zake za mwisho za kimuziki duniani-Farewell Yellow Brick Road, ambayo yatajumuisha zaidi ya matamasha 300 katika mabara matano.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii