Kizaazaa: wajeruhiwa wakikwepa haja ndogo

Daraja la Jannowitz Haki miliki ya picha Google Maps

Mtu mmoja aliyejisaidi akiwa kwenye daraja mjini Berlin azua kizaazaa baada ya kusababisha watu kujeruhiwa, kwa mujibu wa idara ya zima moto mjini humo.

Mtu huyo ambaye hakujulikana alijisaidia haja ndogo kwenye eneo la mteremko wa daraja la Jannowitz kisha mkojo ukatiririka mpaka kwenye boti iliyokuwa imebeba watalii ikipita chini ya daraja.

Watu kadhaa waliokuwa kwenye boti hiyo waliruka ghafla, wakajigonga vichwa vyao wakati boti ilipokuwa inapita chini ya daraja.

Mwanaume ashikiliwa kwenye Gereza la wanawake

Video za ngono zilivyokatisha maisha ya binti

Watu wanne walipelekwa hospitali kwa gari la kubeba wagonjwa wakiwa na mikwaruzo kichwani.

Haijajulikana kama mtu huyo alitozwa faini au alikamatwa.

Kitendo cha mtu huyo kilikosolewa kwenye mitandao ya kijamii.

Mtu mmoja aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: ''Wanyama kwenye bustani yao wana tabia njema.''

Mada zinazohusiana