Je unafahamu uwezo wa Jeshi la Iran Revolutionary Guard ?

Jeshi la IGRC linakadiriwa kuwa na wanajeshi 150,000 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi la IGRC linakadiriwa kuwa na wanajeshi 150,000

Jeshi la Iran la Islamic Revolution Guards Corps (IRGC) lilianzishwa miaka 40 iliopita ili kulinda mfumo wa Kiilsmu wa taifa hilo mbali na kutoa usaidizi kwa jeshi la kawaida.

Tangu wakati huo jeshi hilo limekuwa kubwa kisiasa pamoja na kiuchumi likiwa na ushirikiano wa karibu na kiongozi wa dini nchini humo Ayatollah Ali Khamenei, pamoja na viongozi wengine wakuu.

IRGC linadaiwa kuwa na wanajeshi 150,000 , likijigamba kuwa na vikosi vyake vya ardhini , wanamaji wake na wanaanga na husimamia silaha za kimkakati za Iran.

Pia linadhibiti jeshi la Basij ambalo limesaidia kukabiliana na utovu wa nidhamu ndani ya nchi hiyo pamoja na Bonyads ama wakfu unaoendesha kiwango kikubwa cha uchumi wa taifa hilo.

IRGC lina ushawishi kwengineko katika eneo la mashariki ya kati kwa kutoa fedha , silaha teknolojia, mafunzo na ushauri kwa serikali walishirika na makundi ya kivita kupitia operesheni zake za ugenini kupitia kikosi chake cha The Quds huko Jerusalem.

Ni mienendo kama hiyo ambayo imeilazimu Marekani kulitangaza jeshi hilo kama shirika la kigaid.

Iran imekana kuunga mkono magaidi na kusema kwamba Marekani inajaribu kuliyumbisha eneo la mashariki ya kati.

Walinzi wa mapinduzi

Kabla ya mapinduzi ya 1979 , Shah Muhammad Reza Pahlavi alitegemea uwezo wa jeshi hilo ili kuhakikisha kuwa kuna usalama wa kitaifa na kulinda utawala wake.

Baadaye, utawala mpya wa Kiislamu ulioongozwa na Ayatollah Khomeini, uligundua kwamba pia nao ulithitaji jeshi lenye uwezo ili kulinda uongozi wao na sera zao za mapinduzi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jeshi hilo liliunda ili kukabiliana na mapinduzi

Viongozi hao wa dini walitoa katiba mpya ambayo pia inahakikisha kuwa kuna jeshi la kawaida kwa jina Artesh linalinda mipaka ya Iran na kuweka amani ndani ya nchi pamoja na walinzi tofauti ili kulinda mfumo wa Kiislamu.

Lakini jukumu hilo la kuweka amani pia limechukuliwa na IRGC ambalo pia limeanzisha jeshi lake, wanamaji na wanaanga.

Licha ya kumiliki wanajeshi 300,000 ikilinganishwa na jeshi la kawaida , IRGC ndio jeshi kuu nchini Iran na ndio linalohusika na operesheni nyingi za taifa hilo.

Jeshi la IRGC limepatiwa jukumu la kupiga doria katika mkondo muhimu wa bahari ya Hormuz , eneo jembamba la maji linalounganisha Ghuba na bahari hindi ambapo asilimia 20 ya mafuta duniani yanapitia .

Maboti madogo ya jeshi hilo yamezuia meli za kivita za Marekani ambazo inasema zimekaribia himaya ya maji ya Iran mbali na kuzizuia meli za kimataifa ama hata kuzilazimu kubadili safari.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Silaha za masafa marefu za IRGC

Jeshi la IRGC la angani ambalo halina ndege za kivita ndio linalohusika na silaha za Iran.

Marekani imesema kuwa Iran ina silaha nyingi za masafa marefu katika eneo la mashariki ya kati, likiwa na mifumo 10 ya kurushia silaha za masafa marefu katika utengenezaji mbali na hifadhi kubwa ya mamia ya silaha.

Mwaka 2018, makombora ya masafa marefu yalirushwa yakilenga waasi wa Iran wa kikurdi waliopiga kambi Iraq kaskzini na kundi la Islamic State nchini Syria.

Lakini wapiganaji wanaoshirikiana na IRGC ambao wanajulikana sana ni wale wa Kikurdi ambao serikali ya Iran inawatumia kutekeleza malengo ya sera yake ya kigeni.

Iran inatambua jukumu la wapiganaji wa Quds katika mzozo wa Syria, ambapo imevishauri vikundi vya wapiganaji vinavyomtii rais Bashar al -Assad na kuwapatia silaha maelfu ya wapiganaji wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia wakishirikiana nao katika vita hivyo na Iraq, ambapo inaunga mkonow apiganaji wa Shia ambao wamesaidia kuwashinda wale wa Islamic State.

Mzozo huo umemfanya kamanda wake kwa jina jenerali Qasem Soleimani kuwa mtu maarufu nchini Iran.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jenerali Qasem Soleimani analiongoza jeshi hilo

Utawala wa rais Donald Trump umedai kwamba wapiganaji wa Quds pia wanatumiwa na Iran kama njia mojawapo ya kuwasaidia magaidi katika eneo la mshariki yakati-ikiwemo kundi la Hezbollah nchini Lebanon pamoja na kundi la Palestina Islamic Jihad -kwa kuwapatia fedha , mafunzo, silaha na vifaa.

Wapiganaji wa Quds pia wametuhumiwa na Marekani kwa kupanga njama kutekeleza mashambulio ya kigiaidi , moja kwa moja ama kupitia washirika wake katika mabara matano kati ya saba.

Wapiganaji wa Quds walidai kuhusika katika njama ya kumuua balozi wa Saudia nchini Marekani kwa kulipua mgahawa mjini Georgetown.

Na mwaka uliopita , mahakama nchini Ujerumani ilimuhukumu mwanachama wa wapiganaji wa Quds kwa kumpeleleza kiongozi wa kundi la Ujerumani na Isra na watu wakaribu.

Uwezo wa kiuchumi

Jeshi la IRGC pia lina uwezo mkubwa katika taasisi za kiraia nchini Iran.

Linadhibiti jewshi la Basij Resistance Force , jeshi la kiislamu la kujitolea lenye takriban wanajeshi 100,000 wanaume na wanawake.

Basij ni wastaafu ka uongozi wa mapinduzi ambao huitwa katika barabra za miji ili kutumia nguvu kuwatuliza raia.

IRGC na Basij yalikuwa majeshi yenye umaarufu mkubwa katika kuzima maandamano yaliozuka 2009 baada ya uchaguzi uliokumbwa na hitilafu wakati wa uongozi wa rais Mahmoud Ahmadinejad.

Uwezo wa jeshi hilo ukiongezwa na uungwaji mkono kutoka kwa Ayatollah Khamenei umelifanya kuwa kiungo muhimu katika siasa za Iran.

Haki miliki ya picha Anadolu Agency
Image caption President Hassan Rouhani amewahi kukosana na kamanda wa IRGC jenarali Mohamad Ali Jafari

Kamanda mkuuu meja jenerali Ali Jafaari, alipinga wazi makubaliano yaliofanywa na rais hasdsan Rouhani wakati wa majadiliano hao yaliosababisha mpango wa kinyuklia wa Ira kuafikiwa.