Wema Sepetu aachiwa kwa dhamana

Wema Sepetu Haki miliki ya picha Wema Sepetu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania imemuachia huru kwa dhamana na kumuonya msanii wa Filamu nchini humo, Wema Sepetu(30), kutokiuka masharti ya dhamana, vinginevyo haitasita kumfutia dhamana yake.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde wakati akitoa uamuzi kuhusu mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana.

Juma lililopita, Mahakama hiyo iliamuru mshtakiwa huyo kupelekwa rumande kwa siku saba, ili iweze kutoa uamuzi baada ya mshtakiwa huyo kujisalimisha mahakamani hapo.Limeripoti gazeti la Mwananchi la nchini humo.

Wema alijisalimisha mahakamani juma lililopita baada ya mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa huyo baada ya kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa.

Mahakama ya Kisutu, ilitoa hati ya kumkamata Wema, Juni 11, 2019 baada ya mshtakiwa huyo kukiuka masharti ya dhamana.

Wema Sepetu ahukumiwa Tanzania

Mahakama yatoa agizo la Wema kukamatwa

"Mahakama inatoa onyo la mwisho kwa mshtakiwa, ikitokea mshtakiwa huyu amevuja sheria kwa kutokufika mahakamani bila taarifa, Mahakama hii haitasita kumfutia dhamana." Alisema hakimu Kasonde.

Mahakama ilielekeza kwamba Wema Sepetu azuiwe kwa siku 7 wakati ikisubiriwa kutoa hukumu katika kesi ambapo alishtakiwa kwa kusambaa kwa kanda ya video inayodaiwa kukiuka maadili kati yake na mwanamume mmoja katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania.

Hati ya kukamatwa kwake ilitolewa baada ya mshtakiwa pamoja na mdhamini wake kutofika mahakamani walipohitajika wakati wa kusililizwa ushahidi wa kesi hiyo.

Wakili wa Wema, Ruben Simwanza alieleza kuwa mteja wake alikuwemo mahakamani, lakini aliugua na akalazimika kuondoka - ufafanuzi ambao haukuiridhisha mahakama.