Je Wakenya wana uhusiano wa mapenzi na chuki na wafanyabiashara wa Kichina?

Women wakiwa wamekusanyika katika soko la Gikomba Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Soko la ni moja kati ya masoko makubwa ya wazi katika eneo la Afrika Mashariki

Katika msururu wetu wa barua kutoka kwa waandishi wa habari wa Afrika tunaangazia jinsi kuwasili kwa wafanyabiashara wa Kichina katika soko maarufu la Gikomba ni baraka na laana kwa Wakenya.

Wakati mmoja ilikuwa huwezi kusikia Mchina anafanya biashara katika soko lolote la Kenya.

Lakini mwaka huu limekuwa ni jambo la kawaida kuwaona sokoni - kitu ambacho kinasababisha malumbano na wajasiliamali wadogoambao wanahisi kuwa maisha yao yanatishiwa.

Hali hiyo iliangaziwa mapema mwezi huu na gazeti la masuala ya kibiashara la KenyaKenya's Business Daily newspaper reported ambalo liliripoti juu ya kuingia kwa wafanyabiashara wa Kichina ambao wameweka biashara zao katika soko la Gikomba, moja ya masoko makubwa ya wazi katika mji mkuu Nairobi.

Umaarufu wa soko umetojkana na uuzwaji wa nguo za mitumba- na pesa nyingi hupatikana katika soko hilo.

Gikomba inadaiwa kuwa ni soko la pili kwa ukubwa la mitumba -na kuelewa namna nguo hizi ni maarufu nchini Kenya, mtu anaweza kuangalia takwimu: Wafanyabiashara waliagiza tani 177,160 za nguo hizi mnamo mwaka 2018 zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 17 sawa na dola milioni 166.

Kwa mujibu wa ofisi ya taifa la Kenya ya takwimu kiwango hicho kimepanda kutoka tani 135,868 zilizoagizwa mwaka 2017 na tani 106,974 zilizoagizwa mwaka 2014 - kwa hiyo mitumba ina soko linalokuwa kwa kasi.

Haki miliki ya picha SIMON MAINA
Image caption Soko la Gikombo limekuwani kivutio kwa wafanyabiashara kwa miongo kadhaa

Kufuatia taarifa ya gazeti la Business Daily , ambayo ilihusisha picha za wafanyabiashara wa Kichina, kulikuwa na hisia kali kwenye mitandao ya kijamii , huku baadhi wakihoji ni kwa vipi waliruhusiwa kuanzisha maduka yao Gikomba.

Siku tatu baadae, waziri wa mambo ya ndani alitangaza kuwa Wachina saba waliionekana wakifanya biashara Gikomba wamerudishwa kwao kwasababu hawakuwa na kibali cha kufanya kazi nchini Kenya na hawakutakiwa kufanya kazi katika sekta ambayo imetengwa kwa ajili ya raia.

Huenda alikuwa anazungumza kulingana na Sheria ya Kenya ya Maendeleo ya Uwekezaji, ambayo inaweka masharti kwa wawekezaji wa kigeni inayosema kuwa lazima uwekezaji wao unapaswa kuwa ni wa kuwaongezea ujuzi Wakenya na matumizi ya raslimali za ndani ya nchi katika shughuli zao.

Huku wafanyabiashara hawa wa kigeni wanaweza kusema kuwa walishirikiana na wafanyabiashara wa ndani kuwasaidia na kwamba jukumu lao lilikuwa tu ni kuleta bidhaa- mtu anaweza kusema kuwa hakuna sheria inayozuwia biashara ya uchumi huria nchini Kenya

Kusema ukweli kuna hali ya pengo la kisheria.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Watu husafiri kutoka maeneo ya mbali na karibu kununua bidhaa katika soko la Gikomba

Ndio maana haishangazi kwamba wiki mbili baadae, hakuna ushahidi thabiti unaothibitisha kuwa Wafanyabiashara wa Kichina hawakuwa na vibali sahihi, au kama ni kweli walirudishwa kwao.

Balozi mpya wa Uchina nchini Kenya , Wu Peng, aliiambia televisheni ya Citizen nchini humo kuwa serikali bado haijatoa maelezo juu ya tukio na akawataka maafisa kushirikisha ubalozi hofu zao ili usaidie kuzuwia ukiukwaji wowote wa sheria za Kenya.

Aidha alitetea uwepo wa raia wa Uchina nchini Kenya, akisema kuwa kando na raia wachache waliopo nchini humo kinyume cha sheria, wengi wako Kenya kisheria na wanasaidia kuinua uchumi.

Mzozo huu unafichua uhusiano wa mapenzi na chuki ambao kenya inao na wawekezaji wa Kichina.

Mikaka kadhaa iliyopita walianza kuingiza bidhaa zao kwa wingi, wakiziuza kwa wafanyabiashara wadogo kwa bei yenye punguzo kuanzia bidhaa zao za jumla za ujenzi katika eneo la viwanda mjini Nairobi na zenye ubora zaidi kuliko hata zinazoagizwa kutoka Ulaya.

Wakati huo wafanyabiashara wa ndani walisherehekea kuwa waliweza kutengeneza faida katika maduka yao - na Wateja wa Kenya walinufaika pia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Soko pia lilikabiliwa na mashambulio ya moto pamoja na wanamgambo

Lakini hii imegeuka kuwa uhasama sasa kwasababu wawekezaji wa Kichina wanalenga maduka ya kawaida na kuuza moja kwa moja bidhaa zao kwa wateja biashara za aina zote kuanzia nguo za mitumba, vifaa vya matumizi ya nyumbani na vya Kielekroniki .

Wafanyabiashara wa kenya wanahofia ushindani wa moja kwa moja wa Wachina na sio kwamba tu ni watu kutoka nje, lakini pia ni kwasababu wanaonekana kuwa na pesa nyingui, wanawapunguzia wateja wao bei na wanafanya vema katika uagizaji wa bidhaa zinazohitajika kutokana na mitandao bora zaidi ya uagizaji wa bidhaa.

Baadhi ya wafanyabiashara wanadaiwa kuwa wanaungwa mkono na watengenezaji wa bidhaa nchini kwao Uchina na wanaonekana kupitisha bidhaa zao kwa urahisi zaidi katika bandari za Kenya.

Kuna hofu kuwa ikiwa mkwaruzano huu wa kibiashara haushughulikiwi vizuri, unaweza kusababisha ubaguzi, jambo ambalo halitakuwa jema kwa taifa ambalo linajinadi kuwa ndio kitovu kikuu cha uwekezaji wa kigeni kinachopendelewa na mataifa ya kigeni katika eneo la Afrika Mashariki.

Wale wanaopinga kuingia kwa Wachina katika biashara ndogo wameiomba serikali kuingilia kati, lakini inaaminiwa kuwa rais Uhuru Kenyatta hatachukua hatua zozote kali kwasababu kenya inategemea ufadhili kutoka Uchina kukamilisha miradi yake ya miundombinu

Miradi hii ni pamoja na :

  • Ujenzi wa Kilomita 485 za leri ya kisasa kutoka eneo la mwambao wa kenya hadi katika mji mkuu Nairobi
  • Kilomita 50 za barabara ya Thika super highway inayounganisha mji mkuu na mji wa Thika (ambayo pia ni sehemu ya barabara ya A2, ya Capetown hadi Cairo)
  • Mradi wa dola bilioni 25 wa ujenzi wa bandari ya Lamu inayopitia Sudan Kusini wa (Lapset), ambao utakuwa na bandari,leri ya mafuta, na leri zitakazounganisha mataifa ya Ethiopia, Uganda na Sudan Kusini.

Mchoraji wa vibonzo nchini Kenya alilionyesha mtizamo wa rais Kenyatta akiwataka Wakenya waliangalie suala la wafanyabiashara wa Kichina kwa mapana:

Uchina inaaminiwa kuwa mkopeshaji mkuu wa Kenya, ikikadiriwa kutoa 72% ya mkopo wa ushirikiano kufikia mwezi machi 2018, kwa mujibu wa waraka wa muweka hazina wa serikali uliobainiwa na gazeti la Business Daily.

Hii huenda ilichochewa na hasira ya watumiaji wa mitandao ya kijamii dhidi ya Wachina , hisia ambayo serikali ilisababishwa na serikali kufanya mkataba mbaya na Beijing na wakati walipakodi ndio watakaoishia kulipa deni hilo.

Hakuna data zilizopo kuonyesha ni wachina wangapi wanaoishi nchini Kenya- au ni Wakenya wangapi wanaofanya kazi nchini Uchina kuona ikiwa wanaouza biashara zao nchini Uchina.

Kile kinachofahamika ni kwamba Kenya iliagiza bidhaa za thamani ya dola bilioni 3.6 mwaka jana, huku mauzo ya bidhaa za kenya za thamani ya dola milioni milioni 111 zikipelekwa Uchina.

Uwiano huo wa kibiashara unaweza kuwa ndio sababu hivi karibuni kenya ilipata ruhusa ya kuuza Uchina Parachichi zilizohifadhiwa kwenye friji na waziri wa biashara alitangaza kuwa Kenya itafungua kituo cha usambazaji wa maua yake katika mji wa Kusini mwa Uchina wa Hunan.

Kwa Kenya , hii inaweza kuwa mfano wa methali ya Kichina isemayo : "Safari ya maili 1,000 kuanza na hatua ya kwanza".

Lakini kwa mambo yalivyo, Wakenya wanahisi taifa hilo tajiri zaidi mashariki mwa Asia linapasw akuangaliwa kama taifa rafiki kwa mataifa madogona sio tu benki au mshirika wa kibiashara.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii