AFCON 2019: Bongo Zozo awasisimua watanzania kwa ushabiki sugu kwa Taifa stars

@nickbongozozo Haki miliki ya picha @nickbongozozo

Vioja vya shabiki sugu wa timu ya taifa Tanzania katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika - Bongo Zozo amewaacha wengi hoi katika mitandao ya kijamii nchini humo baadhi wakiguswa na ushabiki wake kwa timu hiyo.

Ametoa matumaini kwa baadhi ya mashabiki wa soka nchini humo licha ya kipigo cha 2-0 walichopokea Taifa Stars katika mashindano ya Afcon 2019 nchini Misri dhidi ya Senegal siku ya Jumapili.

Bongo Zozo, kama anavyojiita katika mitandao ya kijamii ikiwemo You Tube, anaonekana katika mojawapo ya kanda ya video iliosambaa mitandaoni akitembea mjini Cairo akiwa amevaa jezi huku akipeperusha bendera ya Tanzania huku akizungumzwa kiswahili na mashabiki wengine wa Tanzania.

Nchini kwenye Tanzania kwenyewe, picha zake zimesambazwa katika mitandao ya kijamii ikiwemo hata makundi ya Whatsapp.

Baadhi wakifurahia namna Bongo Zozo anavyozungumza kiswahili na kuimba wimbo wa taifa.

Ni swali wanaloniuliza watu wengi "Mzungu mswahili ametuzidi uzalendo" baadhi wakiandika katika mitandao ya kijamii.

Bongo Zozo - ambaye jina lake halisi ni Nick Reynolds - alizaliwa Zimbabwe na kuwahi kuishi Tanzania kabla ya kuhamia Uingereza.

Ameeleza kwamba anazipenda Tanzania na Zimbabwe mataifa yalio karibu sana moyoni mwake.

"Mimi ni shabiki wa timu mbili Ya Zimbabwe na timu ya Tanzania'

Anasema anaishabikia Zimbabwe sababu ndiko alikolizaliwa Zimbabwe, na Tanzania kwa upendo alio nao kwa taifa hilo.

'Napenda na navutiwa sana na mpira wa Afrika lakini sanasana mpira wa Tanzania, sababu kuna fujo isiyoumiza. Yaani watu tuna kelele sana kuliko (mashabiki wa timu nyingine) watu.'

Hatahivyo anaongeza kuwa Kenya pia ni timu anayoishabikia kwasababu zote ni timu za Afrika mashariki kiashiria cha kwamba watu wote ni wamoja.

"Nimeishi Tanzania kwa muda wa miaka kumi na minane tangu mwaka 98 hivi, nilikutana na mwanamke nikamuoa alafu basi nimekuwa Mtanzania," amesema.

Anasema anafurahia sana Tanzania kufuzu katika mashindano ya kombe la mataifa mwaka huu baada ya kusubiri kwa miaka 39."

Je kura anaitupa wapi katika mpambano wa Alhamisi wa Taifa stars dhidi ya Harambee stars ya Kenya?

'Tanzania lazima tuwakung'ute (Kenya)'.

'Sema nitalia machozi hata ya damu kama ni droo - sababu kama tunashindwa kuwafunga Kenya, naombeni mutufunge sababu ikiwa droo basi hatufuzu sisi (Tanzania) na Kenya haiwezi kufuzu' anaeleza Nick.

Bashiri mechi zinazowadia
19/07/2019
Timu
Senegal vs Algeria
  • Unabashiri Senegal ita shinda dhidi Algeria.
  • Unabashiri Senegal itatoka sare dhidi Algeria.
  • Unabashiri Senegal ita shindwa na Algeria.
Muda unaoneshwa ni GMT+2 na kuna uwezekano wa kubadilika. BBC haitahusika na mabadiliko yeyote.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii