Mgogoro wa Marekani na Iran, Trump atoa kauli kali

Trump Haki miliki ya picha EPA

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa kauli kali kuhusu kauli aliyodai kuwa ya ''kijinga na ya matusi'' iliyotolewa na Iran baada ya Rais Trump kutangaza vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo la Mashariki ya Kati.

Kauli zilitolewa kwenye kurasa za twitter zilikuja baada ya Rais wa Iran Hassan Rouhani kusema kuwa hatua ya Marekani inadhihirisha kuwa Ikulu ya Marekani ''ina taahira ya akili''.

Trump amesema inaonyesha kuwa viongozi wa Iran ''hawaelewi uhalisia''.

Aliweka wazi vikwazo siku ya Jumatatu, akisema kuwa ni matokeo ya ''tabia za kiburi'' ambazo Iran imeonyesha.

Trump asitisha mashambulizi dhidi ya Iran 'dakika za mwisho'

Trump aionya Iran juu ya ‘maangamizi’ vita vitakapotokea

Vikwazo vimewagusa watu kadhaa, ambao Marekani imesema wamehusika na vitendo vya kiburi dhidi ya Marekani, akimlenga Kiongozi wa juu wa taifa hilo Ayatollah Khamenei.

Marekani imedai Khamenei amekuwa akivisaidia vikosi vya kijeshi vya Iran, Marekani imedai kuwa kiasi cha pauni bilioni 75 zimetumika kuliwezesha jeshi hilo.

Bwana Rouhani amehoji iweje Marekani inamlenga mtu mmoja ''ambaye anamiliki eneo moja la ibada na nyumba ya kawaida?, '' akiita vikwazo hivyo ni ''vya kijinga''.

Pia amesema madai ya kuwa Marekani inataka mazungumzo na Iran ni uongo mtupu.

Rais Trump ametamba kuwa Iran ilichoelewa ni ''nguvu na mamlaka'' na kuwa Marekani ina vikosi vyenye nguvu zaidi duniani

Haki miliki ya picha AFP/EPA

Je ni nani anayeathiriwa?

Wizara ya fedha nchini Marekani imesema kuwa makamanda wanane wa Iran ambao husimamia kitengo kinachoshauri vitendo vya jeshi kuu la {Islamic Revolution Guard Corps} IRGC walikuwa wanalengwa katika vikwazo hivyo vipya.

Iliongezea kuwa agizo la rais Trump pia litaunyima uongozi wa Iran kupata raslimali za kifedha mbali na kuwalenga watu walioajiriwa na kiongozi huyo wa dini katika afisi kadhaa ama nyadhifa tofauti mbali na taasisi za kigeni za kifedha ambazo huwasaidia kufanya biashara.

Marekani imedai kwamba Ayatollah Khamenei ana utajiri mkubwa ambao unafadhili jeshi la IRGC.

Mwaka 2018 waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema kwamba kiongozi huyo ana utajiri wenye thamani ya $95b ambao hutumika kulifadhili jeshi hilo.

Haki miliki ya picha AFP

Kwa nini kuna mvutano?

Mgogoro ambao umekuwepo baina ya nchi hizo mbili tangu mwaka jana wakati rais Trump alipojitoa katika mkataba wa kimataifa wa mwaka 2015 uliolenga kumaliza mpango wa nyuklia nchini Iran.

Jambo la kuona makubaliano hayo kuwa na kasoro, Trump aliamua kuweka vikwazo.

Iran iliamua kuacha kutekeleza kile ambacho iliahidi kufanya mwanzoni mwa mwezi wa Mei na kutishia kuanza kutengeneza tena nyukilia.

Kumekuwa na mashambulizi dhidi ya meli za mizigo na mafuta katika eneo la ghuba ya Omani, ambapo Marekani na Saudi Arabia zinaishutumu Iran kuyatekeleza. Iran hata hivyo inakanusha.

Tayari Marekani imeshaongeza uwepo wa majeshi yake na vifaa vya kivita katika eneo hilo la Mashariki ya Kati, hali inayoonesha kuwa mzozo huo si wa kuisha leo au kesho.

Mada zinazohusiana