Mtu mmoja tu ruhsa kupata huduma za mtandaoni Nchi nzima,Kivipi?
Huwezi kusikiliza tena

Wakili mmoja MSudan ameruhusiwa kurudishiwa huduma ya mtandao ambao ulikuwa umefungwa!

Wakili mmoja wa huko Sudan ameielezea BBC jinsi alivyoweza kurudishiwa huduma ya mtandao ambapo nchi nzima ni kama imefungiwa huduma hiyo.

Huduma hiyo ilifungwa yapata wiki tatu zilizopita kukabiliana na wimbi la maandamano yaliyofanikiwa kumng'oa madarakani rais Omar Al Bashiri hapo April mwaka huu.

Ndipo wakili huyo Abdel-Adheem Hassan alipopeleka kesi mahakamani kutaka huduma ya internet irudishwe na akashinda kesi hiyo dhidi ya wamiliki wa mtandao wa Zain Sudan.

Hata hivyo ruhusa hiyo itamhusu yeye tu.

"Kesho tunarudi tena mahakamani, natumai kutakuwa na uamuzi mzuri ambao utaruhusu kufunguliwa kwa huduma za mtandaoni kwa watu wengine millioni moja katika siku chache zijazo. " Bw Abdel-Adheem ameelezea.

Hatua hiyo ya kukata huduma za mtandao ilichukuliwa na watawala wa wanajeshi ambao ni watawala wa sasa nchini Sudan. Ilikusudiwa kukabiliana na ghasia zilizojiri baada ya jeshi kuingilia kati na kuwauwa zaidi ya watu 100.

Waandamanaji wanataka kuwe na utawala wa kiraia nchini Sudan,hatua ambayo haijatekelezwa na baraza hilo la kijeshi licha ya shinikizo pia la jamii ya kimataifa.