Nguo ya ndani Kimono aliyozindua Kim Kardashian West yashutumiwa Japan

Women waliovalia kimono wakiwa wamesimama katika mtaa wa Asakusa wakati wa tamasha la Sanja lililofanyika Mei 19, 2019 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kimono ni vazi la kitamadunii la Japan la karne nyingi

Kim Kardashian West amewaudhi watu wa Japan kwa kuanzisha mtindo wake wa vazi la kimomo unaobana maumbile ya mwili, aliouita Kimono Intimates.

Nyota huyo wa kipindi cha maisha halisi nchini Marekani amesema kuwa nembo ya nguo hiyo itakayozinduliwa Jumanne ni ya kipekee kwa ajili ya " kusherehekea na kuonyesha umbo la mwanamke ".

Haki miliki ya picha KimonoIntimates/Sato
Image caption Wataalamu wa Japan wanasema kuwa nguo yake ya Kimomo ya ndani haifanani na kimomo cha kitamaduni cha Japan kimono

Lakini wajapan kwneye mitandao ya kijamii wamesema kuwa nembo hiyo ni ya kukosea heshima vazi lao la kitamaduni.

Kimono, ambayo ni nguo iliyouachilia mwili ambayo kwa kawaida hufungwa na mkanda mkubwa ni vazi lilianza kuvaliwa nchini Japan katika karne ya 15.

Vazi hilo ambalo linachukuliwa kama vazi la kitaifa la Japan, kwa sasa huvaliwa katika matukio maalumu.

"Tunavaa vimomo tukiadhimisha afya, ukuaji wa watoto, harusi, mahafari, katika mazishi. Ni nguo ya sherehe na hurithishwa kwa familia kupitia vizazi ," mmoja wa wanawake wa Japan Yuka Ohishi, aliiambia BBC.

"[Hizi] nguo za kubana maumbile hata hazifanani na kimomo -aliamua tu kuchagua neno ambalo lina Kim ndani yake - hakuna heshima kwa maana ya utamaduni wetu ya vazi ."

Nembo ya Kardashian West- Kimono brand mwaka jana nchini Marekani. Pia ameanzisha nembo ya "Kimono Body", " kimomo intimate" na "Kimono World".

nguo hiyo ya ndani , imetengenezwa kwa njia ya kuzuwia upinde wa nguo ya ndani kutoonekana , na inapatikana kwa rangi tofauti.

Kardashian West amesema kwenye ukurasa wa Tweeter kuwa ni mara nyingi amekuwa akikosa nguo inayoonyesha umbo lake la mwili ya rangi ambayo inaendana na rangi ya mwili wake kwa hiyo tunataka suluhu ya yote tatizo hili".

Watu wengi wamelichukulia suala hili kwa uzito mkubwa kwasababu alitumia jina la nembo yanguo yenye maana kubwa kwa utamaduni wa Wajapan . Wengine walikerwa kwamba nguo ya kitamaduni sasa ina jina sawa na nembo ya nguo ya ndani.

Wengine walihofia kuwa watu wataanza kuhusisha kimomo na Kardashian West, badala ya Japan.

"Ninadhani Kim ana ushawishi mkubwa katika utamaduni wa pop, ninahofu kuwa kutakuw ana watu ambao wanafahamu jina kimomo pekee kama nembo yake ,"alisema Bi Ohishi.

"Ninahisi itakuw ana athari kwa watu wanaotafuta matokeo na , hashtag , kama nembo itakuwa maarufu kamamambo yake mengine ."

Lakini mmoja wa wataalamu wa kimono amesema kuwa ni wazi kwamba Kimomo kinatambuliwa chenyewe kwa nguo ambazo ni kinyume na nguo ya maumbile.

Haki miliki ya picha Sato Kimono/Twitter
Image caption kimono kinavaliwa na wanawake kuzuwia mwili wake usionekane

"Umaana wa kimomo ni baraka, nadhibu na upole. Hakimaanishi kuonyesha umbo au kubana- umbo . Humfunika mvaaji ili kuficha umbo lake," alisema Profesa Sheila Cliffe kutoka Chuo kikuu cha wanawake cha alipozungumza na BBC BBC.

"Kama nikitengeneza sidiria na nikaita sari... baadhi ya watu wataudhika sana. Inaonyesha ukosefu mkubwa wa heshima ... Kimono] inaelezea utambulisho wa Wajapan. Hilo neno si la Kim Kardashian."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii