Mgahawa wa Ufaransa ndio bora zaidi duniani

Mirazur, unaendeshwa na mpishi wa Argentina Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Mgahawa wa Mirazur, unaendeshwa na mpishi wa Argentina

Mgahawa wa Mirazur nchini France imevishwa taji la mgahawa bora zaidi duniani katika sherehe iliyofanyika nchini Singapore.

Mgahawa huo wa chakula wa Ufaransa unaofahamika pia kama French Riviera umechukua nafasi ya kwanza katika shindano la mwaka lililoandaliwa na Migahawa 50 Bora zaidi Duniani.

Mirazur, unaendeshwa na mpishi wa Argentina, ambaye alisifiwa kwa chakula chake mbali mbali, mkiwemo kiazi chekundu kilichotiwa chumvi (beetroot) kutoka kwenye bustani ya mgahawa huo huo.

Tuzo hizi, zilianza kutolewa tangu mwaka 2002, ambaye sasa ni mshindani wa Michelin stars, ingawa baadhi ya wataalamu wanahoji mbinu zilizotumiwa kutoa kumpata mshindi.

Orodha iliyokusanywa kulingana na matokeo yaliyotangazwa na wataalamu 1000 wa mapishi.

Uhispania ilikuwa na migahawa mitatu katika migahawa 10 bora, huku Ufaransa, Denmark na Peru zote zikiwa na migahawa miwili kila nchi katika 10 bora.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Upishi wa kisasa wa pweza wavuma Dar

Nini kilichoufanya mghahawa wa Mirazur kuwa mgahawa bora zaidi duniani?

Migahawa 50 Bora zaidi Duniani, ambayo huchapishwa na chombo cha habari chenye makao yake nchini Uingereza-William Reed Business Media, imesema Mirazur ulitoa "uzoefu bora zaidi wa mgahawa".

Majaji walivutiwa zaidi na "mitizamo isiyo na kifani ya mgahawa wa huo wa Ufaransa, aina tatu za bustani za mboga zinazozalisha mboga tamu na timu ya wapishi wenye vipaji vya kupindukia pamoja na wahudumu wanaokaribisha wateja.

Mpishi wa Argentina Mauro Colagreco amesema kwa alihisi kama "yuko angani", limeripoti shirika la habari la Reuters.

Alisema kuwa kushinda kwake tuzo la kifahari "inaonyesha dunia kuwa unapokuwa na ndoto kila kitu kinawezekana".

Image caption Wakosoaji wa shindano wanasema kuwa hakukuwa na vigezo vilivyoelezewa bayana vya tathmini ya migahawa iliyohusika katika shindano la mapishi

Mgahawa huo ulianzishwa mwaka 2006, na sasa una matawi matatu.

Vipi kuhusu ukosoaji?

Orodha ya migahawa 50 bora ilichaguliwa kwa misingi ya kura ambazo hazijulikali za wataalamu wa upishi duniani.

Wakosoaji walisema kuwa hakukuwa na vigezo vilivyoelezewa bayana vya tathmini ya migahawa.

Sheria pia zilibadilishwa mwaka huu ili kuiondoa migahawa ambayo awali ilichukua nafasi za kwanza kumi za migahawa bora zaidi duniani.

Unaweweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Godfrey Kasaya: Alazimika kula mboga za kiasili baada ya kupatwa na maradhi

Ni akina nani wengine walioingia katika orodha ya 10 bora?

Hii hapa orodha:

1.Mirazur, Menton (Ufaransa)

2.Noma, Copenhagen (Denmark)

3.Asador Etxebarri, Axpe (Uhispania)

4.Gaggan, Bangkok (Thailand)

5.Geranium, Copenhagen (Denmark)

6.Central, Lima (Peru)

7.Mugaritz, San Sebastián (Uhispania)

8.Arpège, Paris (Ufaransa)

9.Disfrutar, Barcelona (Uhispania)

10.Maido, Lima (Peru)

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Kwanini ni marufuku kula mchana wa Ramadhani Zanzibar

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii