Tanzania Kenya zalalamika kuhusu matamshi ya 'chuki' ya mbunge Jaguar

Jaguar Haki miliki ya picha Citizen TV

Hisia tofauti zimeibuka kufuatia matamshi aliyotoa mbunge wa Kenya dhidi ya wachuuzi wa kigeni wanaoendehsa biashara nchini Kenya.

Katika kanda ya video iliosambazwa pakubwa nchini Kenya na katika nchi jirani Tanzania, mbunge huyo Charles Njagua Kanyi, alisema hawatokubali watu wa nje waje kuendesha biashara nchini.

"...Ukiangalia soko zetu, Watanzania na Waganda wamechukua biashara zetu, sasa sisi tumesema enough is enough".

Licha ya Serikali ya Tanzania kuwaomba raia wake kuwa na utulivu na serikali ya Kenya kujitenga na matamshi ya mbunge huyo, bado gumzo linaendelea katika mitandao ya kijamii huku baadhi wakimtaka mbunge huyo aombe radhi kwa matamshi yake:

Wengine wakikejeli jinsi Wakenya wanavyotishiwa na ufanisi wa watanzania,

Katika ufafanuzi aliotoa mwenyewe mbunge huyo katika mtandao wa kijamii Twitter, Jaguar amesema hisia alizotoa zilidhamiriwa kwa raia wa Kichina waliovamia masoko nchini Kenya na kufanya vigumu kwa wananchi kuendesha biashara.

Ameongeza kwamba hapingi ushirikiano wa kieneo ulionuiwa kushinikiza biashara za ndani ya nchi na kieneo.

Serikali ya Kenya imesema imeshutumu 'vikali' matamshi hayo.

Kadhalika serikali imesizitiza katika taarifa yake kwamba wageni wote wanaotaka kuwekeza nchini watakuwa salama.

Baadhi ya Watanzania wamelizungumzia suala hilo katika mitandao kama Twitter kulalamika kuhusu matamshi ya mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki.

Jabir Saleh amesema: "Bahati nzuri sikuwahi mkubali Jaguar tangu anaanza muziki ...'....pengine alikua msanii mbovu kuliko wote niliowahi wasikia from Kenya...'.

Mwingine anagusia muda unapotokea mvutano huu, wakati Kenya na Tanzania zinaelekea kupambana kesho Alhamisi katika mashindano ya kombe la matiafa ya Afrika.

Ben Kolowa anasema: "Natamani kesho mchezaji mmoja wa #TaifaStars afunge goli alafu aoneshe TSHIRT yenye ujumbe kwa Wakenya "Hi Jaguar".

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii