Riyad Mahrez na mkewe Rita waamrishwa kumlipa yaya wao wa zamani

Riyad Mahrez asherekea na mkewe Rita baada ya kushinda taji la mchezaji bora wa ligi ya EPL 2015-16 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Riyad Mahrez asherekea na mkewe Rita baada ya kushinda taji la mchezaji bora wa ligi ya EPL 2015-16

Mchezaji huyo wa Manchester City na Algeria Riyad Mahrez pamoja na mkewe Rita wameamrishwa kulipa zaidi ya £3,600 kama mshahara ambao hawakumlipa yaya wao wa zamani.

Wanandoa hao walimkata fedha hizo mwanamke huyo kwa jina Catalina Miraflores bila idhini yake, aliamuru jaji wa mahakama ya ajira.

Pia wameagizwa kulipa zaidi ya dola 150 kama fidia ya hasara aliyopata yaya huyo baada ya kutomlipa fedha hizo.

Bi Miraflores aliambia gazeti la The Sun: Nilifanya kazi kwa bidii kulipwa fedha hizo.

Man City ilivunja rekodi yake kwa kumsaini winga huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa dau la £60m kutoka klabu ya Leicester 2018.

Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Man City kilichoshinda mataji matatu ya Uingereza mwaka huu.

The Sun liliripoti kwamba bi Miraflores aliajiriwa mwaka 2018 na mchezaji huyo ambaye anadaiwa kupokea mshahara wa £200,000 kwa wiki - ili kuwaangalia watoto wake wawili wa kike.

Katika uamuzi uliochapishwa , jaji John Sherrat alisema: Watuhumiwa walikata mshahara wa kijakazi huyo na sasa wanaagizwa kulipa £3,612. Kwa kukiuka kandarasi ya yaya huyo , walishinda kulipa gharama ya mlalamishi na sasa wameagizwa kumlipa fidia ya £150. yaya huyo".

Malalamishi ya kufutwa kazi kwa uonevu yaliowasilishwa na bi Miraflores yalikataliwa na jopo hilo kwa madai kwamba hakuwa na uzoefu wa miaka miwili.

BBC iliwasiliana na ajenti wa Mahrez ili kutoa tamko.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Winga huyo kwa sasa anaiwakilisha Akgeria katika kombe la Afcon bara Afrika