Burundi: Kwa nini Rais Pierre Nkurunziza amedilisha majina ya maeneo ya kihistoria

President Pierre Nkurunziza, Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Nkurunziza yupo mamlakani Burundi toka 2005

Rais wa Burundi President Pierre Nkurunziza amebadilisha majina ya maeneo ya kihistoria ya nchi hiyo kuashiria jinsi jamii ya Wahutu walio wengi walivyochangia historia hiyo.

Lengo la kubadilisha jina la Uwanja wa Kitaifa, Ikulu ya Rais pamoja na Uwanja Mkuu wa ndege ni "kuwakumbusha Warundi historia yao," alisema katika hotuba yake ya siku ya Uhuru.

Wakosoaji wake hata hivyo wanasema hatua hiyo ni ya kufuta mchango wa historia ya jamii ya Watutsi walio wachache.

Burundi iliadhimisha miaka 57 ya Uhuru wake Julai mosi.

Tangu ilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1962, taifa hilo la linalopatikana katika eneo la maziwa makuu limekumbwa na mzozo wa kikabila kati ya Wahutu na Watutsi.

Bw. Nkurunziza, ambaye ni kiongozi wa zamani wa waasi wa Kihutu alikuwa rais wa pili kuchaguliwa kidemokrasia. Alichaguliwa mwaka 2005 alipokomesha mapigano mabaya ya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 2015 Burundi ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa baada ya hatua ya Bw. Nkurunziza kugombea urais kwa muhula wa tatu kusababisha maandamano ya wafuasi wa upinzani, wakisema kuwa amekiuka katiba.

Mwezi Machi mwka 2018, Chama tawala cha CNDD-FDD kilimtawaza Bw Nkurunziza kuwa ''kiongozi wa milele wa taifa''.

Huwezi kusikiliza tena
Rwanda,Uganda,Tanzania,Burundi na DRC kujadili jinsi ya kupambana na makundi ya waasi

Miezi miwili baadae taifa hilo liliandaa kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katibu ambayo yalimwezesha rais Nkurunziza kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Katika hotuba yake ya siku ya Uhuru, kingozi huyo wa miaka 54 alisema mpango wa kubadilisha majina ya maeneo ya kihistoria ya nchi hiyo ilikuwa njia moja ya kukabiliana na usaliti:

"Hatua hii pia inalenga kufuta majina yaliotokana na kuibuka kwa usaliti na tabia mbaya iliyoletwa na ukoloni," alisema.

Haya ni baadhi ya maeneo aliyobadilisha jina:

Uwanja wa Kitaifa wa mpira

Uwanja mkuu ulioko katika mji mkuu wa Bujumbura, na ambao huchezewa mpira na kuandaliwa sherehe za kitaifa ,sasa unaitwa Uwanja wa Mashujaa.

Ulikuwa ukiitwa uwanja wa Louis Rwagasore, mmoja wa watu mashuhuri katika historia ya Burundi.

Picha yake pia pia imechapishwa katika sarafu za nchi hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Timu ya Taifa ya Soka sasa itacheza mechi zake za nyumbani katika uwanja wa Mashujaa

Alihudumu kama Waziri Mkuu wa kwanza wa Burundi lakini aliuawa kabla nchi hiyo ijipatie uhuru wake mwaka 1962.

Kila tarehe tatu mwezi Oktoba nchi hiyo husherehekea kwa kukumbuka mmchango wake .

Japo jina hilo limefutwa katika Uwanja wa Kitaifa wa Michezo, Rais Nkurunziza amesema majengo mapya ya bunge ambayo yanatarajiwa kujengwa katika mji wa Gitega yatapewa jina la Rwagasore.

Uwanja wa ndege waa Kimataifa wa Burundi

Uwanja mkuu wa ndege wa mjini Bujumbura sasa utafahamika kama Merchior Ndadaye kumuenzi rais wa kwanza wa taifa hilo aliyechaguliwa kwanjia ya kidemokrasia.

Jiongozi huyo kutoka jamii ya Wahutu aliongoza kwa miezi mitatu mwaka 1993 kabla ya kuuawa baada ya sera yake ya mageuzi kuonea jeshi lililokuwa na idadi kubwa ya Watutsi.

Haki miliki ya picha Alamy

Mauaji yake yalisababisha mapigano mapya yaliyoitumbukiza Burundi katika ghasia na mgogoro wa kikabila ulisababisha vita vya watu 300,000.

Barabara yaSeptemba 3

Hadi wa leo siku hiyo ni kumbukumbu ya jinsi kiongozi wa zamani wa kijeshi Pierre Buyoya alivyomng'oa madarakani ndugu yake rais Jean-Baptiste Bagaza mwaka 1987.

Bw. Buyoya, kutoka jamii ya Watutsi aliingia madarakani na kuahidi kuwa kuwaleta pamoja Warundi lakini badala yake uongozi wake ulikuwa wa kidhalimu ambao ukuja kupipingwa vikali na Wahutu mwaka 1989.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lutenit Jenerali Nshimirimana, ambaye aliuawa mwaka 2015, alikuwa kiongozi mwenye utata

Barabara hiyo maarufu mjini Bujumbura sasa imepewa jina la will now bear the name of Lt-Gen Adolphe Nshimirimana, an ally of President Nkurunziza, who was assassinated in 2015 months after an attempted coup against the government.

Luteni Jenerali Nshimirimana alikuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi ambaye alikuwa akiogopewa kutokana na jinsi alivyokua akiendesha shughuli zake kwa njia ya kikatili.

Ikulu ya Rais

Ikulu mpya ya rais sasa imepewa jina la mfalme Ntare Rushatsi.

Iligharimu dola milioni 22 sawa na (£19m) na ujenzi wake ulikuwa zawadi kutoka China.

Haki miliki ya picha You Tube/ Courtesy

Mfalme Rushatsi anaenziwa kwa kuwa mwanzilisha utawala wa kifalme nchi Burundi miaka ya 1500.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii