Iran 'imeongeza urutubishaji wa uranium' baada ya vikwazo vya Marekani

File photo showing showing the reactor building at the Bushehr nuclear power plant in southern Iran (26 October 2010)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kinu cha Bushehr kinaweza kutumia madini ya uranium kama nishati

Iran imekiuka makubalino ya kiwango inachopaswa kurutubisha cha madini ya uranium kwa mujibu wa mkataba wa 2015 ulioidhinishwa na mataifa yenye nguvu duniani, vyombo vya habari Iran vinaripoti.

Shirika la habari la Isna limemnukuu waziri wa mambo ya nje nchini humo aliyethibitisha kuwa taifa hilo limerutubisha zaidi ya kilo 300 zilizotakiwa

Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki limesema litwasilisha ripoti.

Iran imeshinikiza urutubishaji huo wa uranium inayotumika kama nishati na pia silaha za nyuklia kufuatia kuidhinishwa upya vikwazo vya marekani dhidi yake.

Mataifa ya Ulaya yameonya kuwa ukiukaji wowote utakuwa na athari zake.

Iwapo hilo litathibitishwa na shirika la IAEA, linatoa fursa kuidhinishwa upya kwa vikwazo vilivyoondolewa kwa misingi ya Iran kupunguza shughuli zake za nyuklia.

"Kutokana na nilichoambiwa, Iran imezidisha zaidi ya kiwango cha kilo 300 kwa mujibu wa mpango uliofikiwa. Tulitangaza awali." waziri wa mambo ya nje Mohammad Javad Zarif alinukuliwa na Isna Leo Jumatatu mchana.

Awali shirika la habari la, Fars lilimnukuu duru aliyesema kuwa maafisa wa IAEA walipima akiba Jumatatu na kuthibitisha kwamba taifa hilo limepitisha kiwango cha urutubishaji.

Msemaji wa IAEA ameieleza BBC kwamba imesikia kuhusu taarifa hiyo na kuongeza: "Maafisa wetu wapo huko na wataripoti kwa makao makuu punde tu watakapothibitisha kiwango cha uranium kilichopo."

Hatua hii inajiri katika wakati ambapo kuna wasiwasi mwingi katika enoe la mashariki ya kati huku Iran ikiidungua ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani katika hali ya kutatanisha, na Marekani kuishutumu Iran kuhusuika na mashambulio mawili dhidi ya meli za mafuta.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kabla ya urutubishaji, uranium ore hugeuzwa kuwa gesi ya uranium hexafluoride

Nini urutubishaji wa madini uranium?

Madini ya Uranium yaliorutubishwa hutengenezwa kwa kuweka gesi ya uranium hexafluoride ndani ya mashine ya kuzunguka ijulikanayo kama centrifuges kwa lengo la kutenganisha viini muhimu vya kutengeneza nyuklia vijulikanavyo kama U-235.

Chini ya mkataba huo makubaliano ya nyuklia , Iran inaruhusiwa kutengeneza kiwango kidogo cha madini yaliorutubishwa ya uranium yalio na asilimia kati ya 3- 4 ya U-235, na yanaweza kutumika kutengeneza nishati kwa vinu vya nyuklia.

Viwango vya kutengeneza silaha-ni 90% ya uranium iliyorutubishwa au zaidi.

Makubaliano hayopia yanaizuia Iran kuweka akiba inayozidi 300kg ya madini hayo yaliorutubishwa kwa kiwango kidogo.

Iran imekuwa ikikana inarutubisha madini hayo kwa minajili ya kujenga zana za nyuklia.

Kwanini Iran imeongeza viwango vya urutubishaji?

Mapema mwezi Mei, Trump aliweka shinikizo zaidi kwa Iran kwa kuidhinisha upya marufuku kwa matiafa yanayonunua mafuta kutoka kwa Iran.

Hatua hiyo ilinuiwa kusitisha kipato kikuu kwa serikali ya Iran.

Rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kuwa nchi yake inarudi nyuma katika ahadi zake katika makubaliano hayo.

Hii ikiwa ni pamoja na kutotiii sheria kuhusu akiba yake ya urutubishaji mdogo wa madini ya Uranium kiwango kilichowekwa kikwa ni - 300kg na tani 130 - na kusitisha uuzaji wa akiba ya ziada katika mataifa ya nje.

Rouhani pia ameyapatia mataifa hayo ya Ulaya siku 60 kulinda mauzo ya mafuta ya Iran. Iwapo yatashindwa kufanya hivyo , Iran itakiuka masharti ya urutubishaji Uranium na kusitisha uundwaji upya wa kinu cha Arak, ambacho mafuta yake yaliotumika yana plutonium yalio na uwezo wa kuunda mabomu.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Iran limesema limeongeza mara nne uzalishaji wa madini ya uranium

"Katika siku 10 zijazo' ... tutaongeza kiwango cha urutubishaji ," Behrouz Kamalvandi amesema.

"Hii inatokana na kifungo 26 na 36 ya makubaliano ya nyuklia na hili litasitishwa iwapo tu pande nyingine zitawajibika,"ameongeza akitaja vifungu vinavyoeleza namna Iran na washirika wengine watakavyojibu ukiukaji.

"Muda bado upo kwa mataifa ya Ulaya ... lakini mataifa hayo yameeleza sio moja kwamoja kushindwa kwao kuwajibika. Yasifikirie kwamba baada ya siku 60 kutakuwana siku nyingine 60 za ziada ."