Veronica Nkundya: Aeleza yaliomkuta mumewe Raphael Ongangi alipotekwa Tanzania
Veronica Nkundya: Aeleza yaliomkuta mumewe Raphael Ongangi alipotekwa Tanzania
Leo ni siku ya saba tangu kutekwa kwa raia mKenya na mfanyabiashara anayeishi nchini Tanzania Raphael Ongangi. Raphael Ongangi alitekwa nyara akiwa na mke wake maeneo ya Oysterbey jijini Dar es Salaam alipokua akitoka katika kikao cha wazazi katika shule ya mtoto wao.
Lakini tukio hilo lilitokea vipi hasa? Mkewe Bi Veronica Nkundya anasimulia anachokumbuka:
Wiki moja imetimu toka mfanyabiashara raia wa Kenya na mshirika wa Zitto Kabwe kutekwa Tanzania
Kumekuwa na ukimya kutoka kwa vyombo vya dola nchini Tanzania na serikali ya Kenya juu ya tukio hilo.