Jinsi Viagra ya wanawake inavyofanya kazi

Dawa hiyo hutumika kupitia sindano inayodungwa tumboni Haki miliki ya picha Getty Images

Shirika linalohusika na udhibiti wa chakula na dawa nchini Marekani FDA hivi majuzi liliidhinisha dawa mpya kutibu tatizo la ukosefu wa hisia za kingono miongoni mwa wanawake ambao hawajafikia ukomo wa hedhi.

Ukosefu wa hisia hizo husababishwa na mwanamke kutoshiriki katika vitendo vinavyoweza kuvutia hisia za ngono bila ya kuhisishwa na tatizo lolote.

Kemikali kwa jina Vyleese imejaribiwa kutengeneza kile ambacho kinaweza kuitwa Viagra ya kike.

Hili ni swala tata , kwa kuwa baadhi ya wataalam wanahoji asli ya tatizo la hisia za kingono na kukosoa ukosefu wa msisimko wa mapema wakati mwathiriwa anapotumia.

Sindano au tembe

Ikiwa imetengenezwa na kampuni ya Teknolojia ya Palatin Technologies na kuruhusiwa kuuzwa na Amag Pharmaceuticals, dawa hiyo mpya hutumika kupitia sindano ambayo husisimua njia ya akili inayotumika katika hisia za ngono na itapatikana katika baadhi ya maduka ya dawa kuanzia mwezi Septemba.

Ikilinganishwa na dawa nyengine, dawa hiyo haifanyi kazi katika mfumo wa mishipa, lakini huongeza hamu ya tendo la ngono katika mfumo wa neva.

Vyleesi itashindana na Addyi ya watengenezaji dawa wa Sprout, dawa ya kila siku ambapo iliidhinishwa 2015 na kwamba watumiaji hawafai kutumia pombe wakati wanapoitumia.

Addyi iliidhinishwa baada ya kampeni ya kukata na shoka licha ya kukosolewa na wanasayansi wa FDA ambao wanaitambua kuwa na utendakazi wa kadri na isio salama.

Jinsi waathiriwa wanavyoathirika polepole

Haki miliki ya picha Getty Images

Kwa upande wake Vyleesi haizuii matumizi ya pombe na inadaiwa kutoa fursa kubwa ikilinganishwa na mshindani wake, ikiwa na athari za chini, utendakazi wa hali ya juu na sio lazima kuitumia kila siku.

Athari zilizoonekana wakati wa majaribio yake ni pamoja na kichefuchefu ambacho hakikuchukua zaidi ya saa mbili na kilitokea baada ya matumizi ya dawa hizo, kulingana na kampuni hiyo ya utengenezaji wa dawa ya Amag.

Asiliami 40 ya wagonjwa walihisi kichefuchefu.

Dawa hiyo hutumika kupitia sindano tumboni dakika 45 kabla ya tendo la ngono.

FDA inapendekeza kwamba wagonjwa hawawezi kudungwa zaidi ya dozi moja katika saa 24 na sio zaidi ya dozi 8 kwa mwezi.

Wachanganuzi wanakadiria kwamba dawa ilio salama yenye uwezo wa kutibu ukosefu wa hisia inaweza kupata mapato ya hadi $ 1 billion katika soko.

Baadhi ya sekta fulani katika jamii zina matatizo makubwa ya swala hilo na wengine wanakadiria kwamba mmoja kati ya wanawake 10 huathirika.

Nchini Marekani , kwa mfano tatizo hilo linawaathiri wanawake milioni sita , lakini ni wachache wanaotafuta tiba kulingana na Reuters.

''Wanawake hao huathirika polepole hivyobasi hakuna soko la tayari kwa sasa'', alisema William heiden, afisa mkuu mtendaji Amag alinukuliwa na Reuters.

Utata

Hatahivyo shirika hilo linatambua kwamba halijui jinsi Vyleesi inavyofanya kazi akilini ili kusisimua hisia za kingono.

Kuna maono tofauti kwamba dawa ndio suluhu ya tatizo hilo.

Upungufu wa hisia za kingono unaweza kusababishwa na matatizo ya nje, kimaungo na kiakili, kulingana na wataalam tofauti.

Utendakazi wa dawa hiyo ya Vyleesi pamoja na usalama wake ulijaribiwa katika wiki 24 ukishirikisha zaidi na wanawake 1200 ambao hawajafikia ukomo wa hedhi.

Wagonjwa wengi walitumia dawa hiyo mara mbili au tatu kwa mwezi lakini sio zaidi ya mara moja ka wiki.

Takriban asilimia 25 waliripoti kupanda kwa hisia za ngono ikilinganishwa na zaidi ya asilimia 17 miongoni mwa wanawake.

Athari zilizorekodiwa wakati wa majaribio hayo ni pamoja na kichwa kuuma kuwa na madoa doa mekundu usoni na katika ngozi kichefuchefu.