Kwa nini baadhi ya wazazi nchini Kenya huficha hali yao ya HIV?

Brian Omondi
Image caption Brian Omondi anasema ni vigumu sana kuishi na virusi vya HIV jamii ya Wakenya

Baadhi ya wazazi nchini Kenya huweka siri hali yao ya HIV, hadi wanapofariki na kuwaacha duniani watoto wakiwa wagonjwa.

Brian Omondi, ambaye alizaliwa akiwa na virusi vya HIV, alianza kutumia dawa ya kudhibiti makali ya Ukimwi (ARV) akiwa na miaka 10.

Lakini mama yake alipofariki akiwa na miaka 14 ndipo aligundua dawa alizokuwa anameza ni za nini.

Brian ambaye sasa ana maika 22, ni mwanaharakati wa HIV anasema alipata virusi hivyo wakati wa kuzaliwa.

Anasema kuwa anakumbuka akiwa mdogo kuna wakati alikuwa mganjwa karibu kila wakati: ''Hali yangu ilipokuwa mbaya zaidi mama aliamua kunipeleka hospitali nikafanyiwe uchunguzi''

Alipatikana na virusi vya HIV na akaanza kutumia dawa lakini mamayake hakumwambia alikuwa anaugua nini.

''Mama alipofariki nilenda kuishi na shangazi yangu na ni hapo majirani wa karibu walijua hali yangu ya HIV''anasema Brian.

Watu walianza kumkejeli na hata baadhi ya wazazi wakawazuia watoto wao kutocheza nae

"Nakumbuka kuna msichana wa niliekutana nae aliyeniita: 'Wewe mtu wa Ukimwi.' iliniumiza sana."

Tiba ya usiku

Japo idadi kubwa ya vijana wanansemekana kuwa na virusi hivyo nchini Kenya na maeno ya Kusini mwa Jangwa Sahara, badhi ya wale waliozaliwa na virusi hivyo wanaishi navyo bila kujua.

Huwezi kusikiliza tena
Nimejikubali nina virusi vya Ukimwi na kujifunza kuishi navyo

Baadhi ya wagonjwa wanalazimika kuficha dawa zao na, kama Bw. Omondi, huamua kumeza dawa hizo nyakati za usiku.

Winnie Orende, ambaye sasa ana miaka 27, anaelezea alivyoshtuka alipogundua ana HIV akiwa na miaka 12.

"Mama yangu alipofariki, miezi miwili baadae, daktari alipigia simu dada yangu [mkubwa] na kumwagiza niende kumuona hospitali peke yangu,".

Daktari alijua kuwa mama yake alifariki kutokana na Ukimwi - na alitaka kumfanyia uchunguzi kubaini hali yake ya HIV. Alipatikana na virusi hivyo.

"Nikiwa na umri huo mdogo nilichanganyikiwa sana. Sijawahi kufanya mapenzi na mimi sio kahaba, kwa hivyo nawezaje kuwa na HIV?"

Cha kusikitisha yeye ndiye ailikuwa mdogo katti ya ndungu zake na ni yeye tu aliyepatikana na virusi vya HIV.

"Nilishangaa mbona iwe mim? Hali hiyo iliniathiri sana kwa muda."

'Shule nzima iligundua nilikua na Ukimwi'

Alikataa kutumia dawa hadi akalazwa hospitali mara kadhaa.

Daktari wake alimfahamisha mwalimu mkuu wa shule kuhusu hali yake na kumweleza kuwa siku zingine atakosa kuja shule kwa sababu atahitajika kuenda kufanyiwa vipimo vya kimatibabu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanaharakati wanawahimiza Wakenya umuhimu wa kujadili wazi wazi kuhusu HIV

Baadhi ya walimu walifahamishwa nia baada ya siku kadhaa shule nzima ilijua kuhusu hali yake ya HIV-na kutoka wakati huo maisha katika shule hiyo yalibadilika kabisa mpaka wa leo.

"Nilinyanyapaliwa na jami ninayoishi nayo katika mtaa wa Kongowea, Mombasa Pwani ya Kenya. Tatizo lilianza pale walipojua hali yangu ya hiv. Watu walikuwa wakiniita kila aina ya majina ," anasema Bi Orende, ambaye kwa sasa ni mhudumu wa kujitolea wa afya ambaye huwapa ushauri nasaha wagonjwa wa UKimwi.

"Nilijihisi vibaya. Ingelikuwa vyema kama wangenifahamisha hali yangu ya HIV,kuliko niambiwe na mtu mwingine. Nilitamani kujitoa uhai, lakini nilipomkumbuka mateso yatakayomkabili dada yangu mdogo anaenitegemea. Nilijiepusha na mawazo hayo mabaya.

Wanaharakati wanatoa wito kwa asasi za elimu nchini kuwahamasisha watoto kuhusu ugonjwa huo na pia kuwapa maelezo kuhusu HIV kupitia elimu ya msingi.

Dr Griffins Mang'uro anasema ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwa wazi na kuwaambia ukweli watoto wao kuhusu hali yo ya HIV wakiwa kati ya miaka 9 hadi 11.

"Mtoto akipata uelewa wa HIV na Ukimwi ni nini huo ndo wakati mwafaka wa kumwelezea kuwa ameathirika na anahitaji kutumia dawa.

"Mtoto akianza kumeza dawa ni muhimu ajue ni anaugua nini na kwamba dawa anazotumia ni za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa huo .

Anaonya kuwa kuweka siri masuala kama hayo kunawaweka katika hatari ya kutotumia dawa inavyostahili.

"au watakuwa na machungu wakijua baadae hali yao kwasababu hawakuambiwa mapema."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii