Ipi hatma ya tendo la ndoa wakati watoto wanatengezwa katika maabara?

Kwa nini tunashiriki ngono?

Majibu mengi yatahusiana na kutafuta watoto - kwa kuwa tendo la ngono ndio sababu kuu ambayo watoto hupatikana.

Lakini Je tungefikiria nini kuhusu tendo la ngono iwapo swala la kupata watoto lisingalikuwepo?

Tangu kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza wa maabara 1978, takriban watoto milioni nane wamezaliwa kupitia mfumo wa kiteknolojia wa IVF ambapo yai la mama na mbegu za kiume huchanganywa nje ya kizazi cha mama anayebeba mimba kabla ya kudungwa katika kizazi chake.

Na idadi hiyo huenda ikaongezeka katika siku zijazo huku vifaa vya kubaini hatari ya magonjwa ya jeni katika viini tete ikiwa kitendawili.

Ubashiri wangu ni kwamba katika siku za usoni bado watu wataendelea kufanya tendo la ngono - lakini sio kwa lengo la kutengeza watoto.

Henry T Greely, mtunzi wa kitabu kwa jina The End of Sex And The Future of Human Reproduction, anasema kuwa katika kipindi cha kati ya miaka 20 na 40 , watu wengi duniani walio na afya njema watachagua kupata ujauzito katika maabara.

Kitabu cha Greely kwa sasa kinatathmini baadhi ya changamoto zinazokabili mpango huo wa kimaabara .

Kwa sasa kutakuwa na ukosoaji wa hali ya juu lakini kadri siku zinavyosonga mbele huku watoto wanaokuzwa katika maabara wakionekana bila tatizo lolote la kuwa na vichwa viwili au mkia, umma utapendelea kupata watoto kupitia njia zisizoshirikisha tendo la ngono.

Katika ulimwengu huo ambapo watoto huzaliwa katika maabara , ujauzito kupitia tendo la ngono ni chaguo, ambapo maadili ya ngono hayahusiani na kutafuta watoto - Je tendo la ngono litakuwa na umuhimu gani?

''Lengo la ngono ni nini?''

Kibailojia kuna sababu moja ilio wazi kuhusu ngono ya binadamu.

Tunashiriki ngono kwa sababu inatimiza malengo yetu ya kibaiolojia ikiwemo lile la kutafuta watoto na upendo.

Hizi ndio sababu mbili muhimu .

Hivyobasi mapenzi ni kushiriki ngono kulingana na asli ya hisia za kimapenzi.

Sababu kuu inayowafanya watu kushiriki ngono kulingana na Aristotole sio kwa sababu tunataka kushiriki ngono bali kwa sababu tunataka kupenda na kupendwa.

Ngono sio kitu bali kitu chengine , kitu kilichopo juu, kitu kizuri.

Kama watu wengine, Aristotle anachukulia tendo la ngono kwenda sambamba na mapenzi.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kwa nini tunashiriki tendo la ngono basi? Kwa lengo la kutafuta watoto. Kuhusiana sio.

Lakini hayo ni majibu mawili pekee yanayoweza kutolewa. Katika utamaduni wake , tendo la ngono linazidi sababu zake.

Fikiria kuhusu chakula. Kuhusiana na mukhtadha wa kuishi, inaleta maana kwa nini tunakula na kwamba tunakula pamoja.

Tofauti iliopo kati yetu sisi binadamu na wanyama ni kwamba tunafurahi kufanya vitu vibaya.

Tunavifanya kwa sababu tunavifurahia kwa kuwa kushiriki katika vitendo kama hivyo kunatupatia raha.

Nadhani ni wakati kukiri kwamba tunashiriki tendo la ngono kwa lengo la kujiridhisha ama kujifurahisha.

Kwa kweli kuna umuhimu wa kushiriki tendo la ndoa la sivyo tungekua tukifanya mambo mengine.

Lakini miongo michache iliopita imetufanya kukabiliana na mafikra kwamba tendo la ngono linafaa kufanywa kwa malengo fulani pekee.

Mwaka 2015 katika utafiti wake, Jean M Twenge profesa wa saikolojia katika chuo kikuu cha San Diego ,alichunguza tabia za raia wa Marekani kuhusu tendo la ndoa kati ya 1970 hadi 2010.

Aligundua kwamba kati ya 1970 na 2010, raia wa Marekani walianza kukubali kushiriki katika tendo la ngono nje ya ndoa.

Haki miliki ya picha Getty Images

Sambamba na tafiti zilizopita kupungua kwa imani za kidini na ongezeko la sifa za kibinafsi, Wamarekani wengi wanaaamini kwamba ngono haipaswi kuzuiwa na mikusanyiko ya kijamii.

Vizazi vya hivi karibuni pia vimeanza kuwa na imani kama hiyo, vikiripoti kiwango cha juu cha washirika wa tendo la ngono nje ya ndoa kama vile watu wazima na wengi wanazidi kushiriki ngono nje ya ndoa zaidi ya wale waliozaliwa mapema karne ya 20.

Kutakuwa na mawazo mapya kuhusu utambulisho wa ngono.

Ikiwa ngono haina maana yoyote isipokuwa ngono; ikiwa watoto hawapatikani kwa kuwa na "tofauti" ya kijinsia; ikiwa uzazi unafanyika katika maabara; Je! watu wa baadaye watajisikia huru kufanya ngono na wanaume na wanawake kwa mapenzi?

Kuna sababu nyingi za kukubalika kwa mapenzi ya jinsia moja yapo , ikiwa ni pamoja na vile waandishi habari wanavyoangazia kwa uzuri watu wa jinsia hiyo, usaidizi wa umma, mashirika ya matibabu na kisaikolojia, ni ukweli kwamba watu wengi wanajua watu wa LGBT.

Haki miliki ya picha Getty Images

Au wanaweza kujisikia vizuri kukuza tamaa zao za ngono? Ni dhana ya mwelekeo wa ngono na utambulisho unaohusishwa na wazo la kizazi cha uzazi? Katika siku zijazo, je, maneno kama "ushujaa wa kiume" na "mapenzi ya jinsia moja" yatasikika tu katika historia?

Twenge anasema kwamba katika idadi ya watu , tabia hutofautiana kwa sababu ya miaka , jinsia, dini na imani, lakini utafiti unaonyesha kwamba mabadiliko makubwa kuhusu tendo la ngono kati ya vizazi yamefanyika kwa muda.

Hivyobasi maono yetu kuhusu tendo la ndoa yanatokana na eneo na muda. Maadili yetu ya tendo hilo hayana muda, yanabadilika na yataendelea kubadilika. Pengine kwa kasi zaidi ya tulivyojiandaa.