AFCON 2019: Wachezaji wa Uganda Cranes wasusia mazoezi wakidai malipo

Patrick Kaddu celebrates scoring Uganda's opening goal of the 2019 Africa Cup of Nations Haki miliki ya picha Reuters

Wachezaji wa Uganda walisusia mazoezi Jumanne katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwasbababu ya mzozo wa malipo, kwa mujibu wa shirikisho la soka nchini humo (FUFA).

Ni mzozo wa hivi karibuni kutokea katika mashindnao hayo kufuatia hali kama hiyo kujiri kwa wachezaji wa timu za Zimbabwe, Nigeria na Cameroon.

Timu hiyo ya Cranes iliibuka nafasi ya pili katika kundi lake na inajitayarisha kukabiliana na Senegal katika timu 16 bora Ijumaa.

FUFA linasema wachezaji hao wanajaribu kujadili upya masikizano katika mkataba uliosainiwa kati yao.

Linasema kuwa makubaliano yalifikiwa kabla ya mahsindnao na limetaja malipo ambayo tayari yametolewa kwa wachezaji hao.

"Kufikia tarehe 2 Julai 2019, kila mchezaji alikuwa amepokea hadi $14,600 ... na marupurupu ya ziada ya kila siku na kitita cha ushindi kinachowasubiri," taarifa hiyo imesema.

Bashiri mechi zinazowadia
19/07/2019
Timu
Senegal vs Algeria
  • Unabashiri Senegal ita shinda dhidi Algeria.
  • Unabashiri Senegal itatoka sare dhidi Algeria.
  • Unabashiri Senegal ita shindwa na Algeria.
Muda unaoneshwa ni GMT+2 na kuna uwezekano wa kubadilika. BBC haitahusika na mabadiliko yeyote.

"Tunatarajia wachezaji watabadili uamuzi wao na warudi uwanjani Jumatano," msemaji wa FUFA ameiambia BBC.

wachezaji hao hawajatoa kauli kufikia sasa.

Nigeria, Zimbabwe na Cameroon pia zimekabiliwa na hali hiyo katika kuelekea kwa mahsindano hayo nchini Misri 2019 au tangu mashindano hayoyaanze.

Visa vyote hivyo vilitatuliwa pasi kutatuza mashindano hayo.

Samahani, kisakuzi chako hakiwezi kufungua ukurasa huu

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea